Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • wp20 Na. 3 kur. 4-5
  • Muumba Wetu Mwenye Upendo Anatujali

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Muumba Wetu Mwenye Upendo Anatujali
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2020
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • 1. MUUMBA WETU HUFANYA JUA LIANGAZE
  • 2. MUUMBA WETU HUFANYA MVUA INYESHE
  • 3. MUUMBA WETU HUTUANDALIA CHAKULA NA MAVAZI
  • Mahubiri ya Mlimani—Msihangaike
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Thamini Mvua
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Kwa Sababu Gani Ushukuru Muumba?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Tafuta Ufalme, Si Vitu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2016
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2020
wp20 Na. 3 kur. 4-5
Jua linachomoza milimani.

Muumba Wetu Mwenye Upendo Anatujali

1. MUUMBA WETU HUFANYA JUA LIANGAZE

Je, unafikiri ingewezekana kuishi duniani bila mwanga wa jua? Jua hutoa nishati ambayo husaidia miti kutokeza majani, maua, matunda, kokwa, na mbegu. Pia, husaidia mizizi ya miti kufyonza maji kutoka kwenye ardhi, kupeleka kwenye majani na kisha maji hayo hugeuka kuwa mvuke.

Picha ya shamba la chai lililo milimani.

2. MUUMBA WETU HUFANYA MVUA INYESHE

Mvua ni zawadi bora kutoka kwa Mungu ambayo huwezesha dunia kuzalisha chakula kwa ajili yetu. Mungu hutupatia mvua kutoka mbinguni na majira ya mavuno, akitushibisha kwa chakula na kuijaza mioyo yetu furaha.

Ndege aliyetua kwenye tawi la mti, akijaribu kudaka tunda linalodondoka.

3. MUUMBA WETU HUTUANDALIA CHAKULA NA MAVAZI

Mara nyingi, akina baba huhangaika sana ili kupata chakula cha kutosha na mavazi kwa ajili ya familia zao. Maandiko yanasema hivi: “Waangalieni kwa makini ndege wa angani; hawapandi mbegu, hawavuni, wala kukusanya ghalani, na bado Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, ninyi si wenye thamani kuliko wao?”—Mathayo 6:25, 26.

“Jifunzeni kutoka kwa mayungiyungi ya shambani, jinsi yanavyokua . . . ; lakini ninawaambia hata [Mfalme] Sulemani katika utukufu wake wote hakupambwa kama maua hayo. Basi, ikiwa Mungu huivika hivyo mimea ya shambani . . . , je, hatawavika vizuri zaidi?”—Mathayo 6:28-30.

Kwa kuwa Mungu ana uwezo wa kutuandalia chakula na mavazi, bila shaka atatusaidia kupata mahitaji mengine maishani. Ikiwa tutajitahidi kufanya mapenzi ya Mungu, atabariki jitihada zetu za kuzalisha chakula, au atatusaidia kupata kazi ambayo itatuwezesha kupata mahitaji yetu.—Mathayo 6:32, 33.

Kwa kweli, tuna sababu nzuri za kumpenda Mungu tunapochunguza jua, mvua, ndege wa angani na maua. Makala inayofuata itazungumzia jinsi Muumba wetu anavyowasilisha ujumbe wake kwa wanadamu.

Muumba wetu “[huangaza] jua lake . . . na hunyesha mvua.”​—MATHAYO 5:45

Muumba wetu anatupenda sana na kutujali. Kama baba mwenye upendo, Muumba wetu huitunza familia yake. Maandiko Matakatifu yanasema kwamba Mungu ni mkarimu, naye ‘anajua kile tunachohitaji hata kabla hatujamwomba.’​—Mathayo 6:8.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki