HAZINA ZA NENO LA MUNGU | ISAYA 34-37
Hezekia Alithawabishwa kwa Sababu ya Imani Yake
Mfalme Senakeribu wa Ashuru alimtuma Rabshake Yerusalemu akawaambie watu wa jiji hilo wasalimu amri. Waashuru walitoa hoja mbalimbali za kuwafanya Wayahudi wasalimu amri bila kupigana.
Hakuna atakayewasaidia. Misri haitawasaidia.—Isa 36:6
Shaka. Yehova hatawapigania kwa sababu mmemuudhi.—Isa 36:7, 10
Vitisho. Hamwezi kulishinda jeshi lenye nguvu la Waashuru.—Isa 36:8, 9
Vishawishi. Kujisalimisha kwa Waashuru kutaboresha maisha yenu.—Isa 36:16, 17
Hezekia alikuwa na imani thabiti katika Yehova
Alifanya yote awezayo kutayarisha jiji kwa ajili ya kuzingirwa
Alimwomba Yehova awakomboe na aliwatia moyo watu wafanye hivyo pia
Imani yake ilithawabishwa Yehova alipomtuma malaika na kuwaua mashujaa 185,000 wa Ashuru katika usiku mmoja