Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • wp20 Na. 3 kur. 14-15
  • Furahia Baraka za Muumba Wetu Milele

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Furahia Baraka za Muumba Wetu Milele
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2020
  • Habari Zinazolingana
  • Miujiza ya Yesu Unaweza Kujifunza Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Miujiza na Mizuka—Kwa Nini Haihitajiwi
    Amkeni!—1990
  • Tunaweza Kujifunza Nini Kutokana na Miujiza ya Yesu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2023
  • Aliwapenda Watu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2020
wp20 Na. 3 kur. 14-15
Watu wa jamii mbalimbali wakifurahia kuwa pamoja katika dunia paradiso.

“Dunia itatoa mazao yake; Mungu, Mungu wetu, atatubariki.”​—ZABURI 67:6

Furahia Baraka za Muumba Wetu Milele

Mungu alimwahidi nabii Abrahamu kwamba mmoja kati ya wazao wake atayaletea “mataifa yote ya dunia” baraka. (Mwanzo 22:18) Mzao huyo ni nani?

Karibu miaka 2,000 iliyopita, Mungu alimpa Yesu, mzao wa Abrahamu, uwezo wa kufanya miujiza. Miujiza hiyo ilithibitisha kwamba ahadi ambayo Abrahamu alipewa, kwamba mataifa yote yangebarikiwa, ingetimizwa na Yesu.​—Wagalatia 3:14.

Miujiza ambayo Yesu alifanya ilithibitisha kwamba amechaguliwa na Mungu kuwabariki wanadamu, na pia ilionyesha jinsi Mungu atakavyomtumia kuwabariki wanadamu milele. Miujiza ambayo alifanya ilifunua sifa zake nzuri. Kwa mfano:

Aliwajali watu—Yesu aliwaponya wagonjwa.

Siku moja mtu fulani mwenye ukoma alimwomba Yesu amponye. Yesu akamgusa na kumwambia: “Ninataka!” Mara moja ule ukoma ukaisha.​—Marko 1:40-42.

Ukarimu—Yesu aliwalisha wenye njaa.

Yesu hakutaka watu wawe na njaa. Katika nyakati tofauti, Yesu alifanya miujiza ya kuwalisha maelfu ya watu kupitia vipande vichache vya mikate na samaki. (Mathayo 14:17-21; 15:32-38) Watu walikula na kushiba, na chakula kingi kilibaki.

Huruma​—Yesu aliwafufua watu waliokufa.

Mjane fulani alifiwa na mwana wake na hakuwa na mtu mwingine wa kumtunza. Yesu alipomwona mjane huyo akiomboleza, ‘akamsikitikia’ na kumfufua mwana wake.​—Luka 7:12-15.

BARAKA ZA MILELE DUNIANI

Tayari Yesu amethibitisha kwamba Mungu ana uwezo wa kuwaletea wanadamu baraka. Hivi karibuni, Yesu atakaporudi kama alivyoahidi, Mwenyezi-Mungu atamtumia kufanya miujiza mikubwa zaidi duniani pote!

Maisha yatakuwaje duniani Mungu atakapotimiza ahadi aliyompa Abrahamu? Wale wanaompenda na kumheshimu Mungu “wataimiliki dunia, nao watafurahia kwelikweli wingi wa amani.” (Zaburi 37:11) “Kifo hakitakuwapo tena, wala maombolezo wala kilio wala maumivu hayatakuwapo tena.”​—Ufunuo 21:4.

Tutafurahia kuishi milele kwenye ulimwengu wenye amani! Tunakualika ujifunze mengi zaidi kuhusu baraka ambazo utawala wa Mungu utaleta hivi karibuni. Utapata habari hizo kwenye tovuti ya www.jw.org/sw.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki