HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MATENDO 23-24
Ashtakiwa Kuwa Msumbufu na Kuchochea Uasi
Wayahudi jijini Yerusalemu “[walijifunga] kwa kiapo cha laana” kusudi wamuue Paulo. (Mdo 23:12) Hata hivyo, mapenzi ya Yehova yalikuwa kwamba Paulo aende Roma kutoa ushahidi. (Mdo 23:11) Mpwa wa Paulo alisikia kuhusu njama hiyo naye akaripoti kuihusu na hivyo kuzuia Paulo asife mapema. (Mdo 23:16) Simulizi hili linakufundisha nini kuhusu . . .
jaribio lolote la kuzuia kusudi la Mungu?
njia ambayo Mungu anaweza kutumia kutusaidia?
ujasiri?