Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr19 Agosti kur. 1-2
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2019
  • Vichwa vidogo
  • AGOSTI 12-18
  • AGOSTI 19-25
  • AGOSTI 26–SEPTEMBA 1
Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2019
mwbr19 Agosti kur. 1-2

Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

AGOSTI 12-18

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | TITO 1–FILEMONI

“Waweke Rasmi Wazee”

w89 5/15 31 ¶5

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Kwa uhakika hakuwa akikubaliana na msemo wowote wenye ubaguzi wa rangi au wenye ukabila kwa kuwahusisha ndani Wakrete wote kwa ujumla. Tunaweza kuwa na uhakika wa jambo hilo, kwa maana Paulo alijua kwamba katika Krete walikuwako Wakristo wazuri sana ambao Mungu alikuwa amewakubali na kuwapaka mafuta kwa roho takatifu Yake. (Matendo 2:5, 11, 33) Walikuwako Wakristo wenye ujitoaji ambao walitosha kufanyiza makundi katika “kila mji” [jiji baada ya jiji, NW]. Ingawa Wakristo hawakuwa wanadamu wakamilifu, tunaweza kuwa na uhakika kwamba hawakuwa waongo na walafi wavivu; au sivyo, wasingeendelea kuwa na kibali cha Yehova. (Wafilipi 3:18, 19; Ufunuo 21:8) Na kama vile sisi leo tunavyopata katika mataifa yote, inaelekea kwamba katika Krete walikuwako watu wenye mioyo ya ufuatiaji haki waliohuzunishwa na viwango vya chini vya kiadili ambavyo viliwazunguka na wakawa tayari kuuitikia ujumbe wa Kikristo.—Ezekieli 9:4; linganisha Matendo 13:48.

AGOSTI 19-25

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-1 1185 ¶1

Mfano

Je, sikuzote Yesu amemwiga Baba yake kwa kiwango kilekile?

Mwana mzaliwa wa kwanza wa Mungu, ambaye baadaye alikuja kuwa mwanadamu Yesu, ni mfano wa Baba yake. (2Ko 4:4) Ni wazi kwamba Mungu alikuwa akiongea na Mwana huyo aliposema, “Na tufanye mtu kwa mfano wetu,” na tangu Mwana alipoumbwa alikuwa katika mfano wa Baba yake, Muumba. (Mwa 1:26; Yoh 1:1-3; Kol 1:15, 16) Alipokuwa duniani akiwa mwanadamu mkamilifu, alionyesha sifa na utu wa Baba yake kwa kiwango kikubwa zaidi iwezekanavyo kwa mwanadamu kuonyesha, na ndiyo sababu angeweza kusema “yeyote ambaye ameniona mimi amemwona Baba pia.” (Yoh 14:9; 5:17, 19, 30, 36; 8:28, 38, 42) Hata hivyo, bila shaka walifanana hata zaidi wakati ambapo Baba yake, Yehova Mungu, alimfufua Yesu na kumpa uhai wa roho pamoja na “mamlaka yote mbinguni na duniani.” (1Pe 3:18; Mt 28:18) Kwa kuwa Mungu wakati huo alimkweza Yesu na kumpa “cheo cha juu zaidi,” sasa Mwana wa Mungu alionyesha utukufu wa Baba yake kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko alivyofanya kabla ya kutoka mbinguni na kuja duniani. (Flp 2:9; Ebr 2:9) Kwa hiyo, sasa yeye ni “mfano kamili wa utu [wa Mungu].”—Ebr 1:2-4.

it-1 1063 ¶7

Mbingu

Maneno ya Zaburi 102:25, 26 yanamhusu Yehova Mungu, lakini mtume Paulo anayanukuu akimrejelea Yesu Kristo. Hii ni kwa sababu Mwana mzaliwa-pekee alikuwa Wakili wa kibinafsi ambaye Mungu alimtumia alipokuwa akiumba ulimwengu. Paulo anaonyesha tofauti iliyopo kati ya umilele wa Mwana na uumbaji wa asili, ambao Mungu, ikiwa angependa, angeweza “[kuukunja] kama kanzu” na kuuweka kando.—Ebr 1:1, 2, 8, 10-12; linganisha 1Pe 2:3, maelezo ya chini.

AGOSTI 26–SEPTEMBA 1

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-1 1139 ¶2

Tumaini

Tumaini hilo la uzima wa milele na tazamio la uhai usioweza kuharibika kwa wale walio “washiriki wa mwito wa mbinguni” (Ebr 3:1) lina msingi imara na ni kitu ambacho mtu anaweza kukitegemea kabisa. Linategemezwa na mambo mawili ambayo haiwezekani kwa Mungu kusema uwongo, yaani, ahadi na kiapo chake, na tumaini hilo linamtegemea Kristo, ambaye sasa amepewa uhai usioweza kufa huko mbinguni. Hivyo tumaini hilo linatajwa kuwa “nanga ya nafsi, likiwa hakika na imara, nalo huingia ndani ya pazia [kama kuhani mkuu alivyoingia Patakatifu Zaidi katika Siku ya Kufunika Dhambi], ambamo mtangulizi ameingia kwa ajili yetu, Yesu, ambaye amekuwa kuhani mkuu milele kama Melkizedeki.”—Ebr 6:17-20.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki