Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr19 Oktoba uku. 1
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2019
  • Vichwa vidogo
  • OKTOBA 14-20
Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2019
mwbr19 Oktoba uku. 1

Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

OKTOBA 14-20

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-2 565 ¶3

Mwangalizi

Mwangalizi Mkuu Zaidi. Ni wazi kwamba 1 Petro 2:25 inanukuu andiko la Isaya 53:6 kuhusiana na wale ambao ‘kama kondoo walipotea njia,’ kisha Petro akasema: “Lakini sasa mmerudi kwa mchungaji na mwangalizi wa nafsi zenu.” Bila shaka, maneno hayo yanamrejelea Yehova Mungu, kwa kuwa wale ambao Petro aliwaandikia hawakuwa wamepotea na kumwacha Yesu Kristo, badala yake, kupitia Yesu, walikuwa wameongozwa kurudi kwa Yehova Mungu ambaye ndiye Mchungaji Mkuu wa watu wake. (Zab 23:1; 80:1; Yer 23:3; Eze. 34:12) Yehova pia ni mwangalizi, yeye ndiye anayetuchunguza. (Zab 17:3) Uchunguzi (Kig., e·pi·sko·peʹ) anaofanya unaweza kuhusianishwa na jinsi anavyotekeleza hukumu, kama ilivyokuwa katika karne ya kwanza W.K. Yerusalemu liliposhindwa kutambua wakati wake wa “kukaguliwa [Kig., e·pi·sko·pesʹ].” (Lu 19:44) Au uchunguzi huo unaweza kuleta matokeo mazuri, kama itakavyokuwa kwa wale watakaokuwa wakimtukuza Mungu katika siku “ya ukaguzi wake [Kig., e·pi·sko·pesʹ].”—1Pet 2:12.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki