Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr19 Novemba uku. 1
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2019
  • Vichwa vidogo
  • NOVEMBA 4-10
  • NOVEMBA 11-17
Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2019
mwbr19 Novemba uku. 1

Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

NOVEMBA 4-10

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-1 862 ¶5

Msamaha

Ni jambo linalofaa kumwomba Mungu msamaha kwa niaba ya wengine, hata kwa niaba ya kutaniko zima. Musa alifanya hivyo kuhusu taifa la Israeli, aliungama dhambi ya taifa zima na kuomba msamaha, na Yehova alikubali sala yake. (Hes 14:19, 20) Pia, Sulemani, alipokuwa akiweka hekalu wakfu, alisali akimwomba Yehova awasamehe watu wake wanapotenda dhambi kisha wageuke na kuacha mwenendo wao mbaya. (1Fa 8:30, 33-40, 46-52) Ezra alitenda kama mwakilishi wa Wayahudi waliorudishwa alipoungama waziwazi dhambi zao. Sala yake ya kutoka moyoni yenye kutia moyo iliwachochea watu kuchukua hatua na kupokea msamaha wa Yehova. (Ezr 9:13–10:4, 10-19, 44) Yakobo aliwatia moyo wote kwamba ikiwa yeyote ni mgonjwa awaite wazee wa kutaniko nao wasali kwa ajili yake, na “ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.” (Yak 5:14-16) Hata hivyo, kuna “dhambi ambayo huleta kifo,” dhambi dhidi ya roho takatifu, kuzoea kufanya dhambi kimakusudi ambako hakuna msamaha. Mkristo hapaswi kusali kwa ajili ya wale wanaotenda dhambi kwa njia hiyo.—1Yo 5:16; Mt 12:31; Ebr 10:26, 27; ona DHAMBI, I; ROHO.

NOVEMBA 11-17

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-2 279

Karamu za Upendo

Biblia haielezi jinsi karamu hizo za upendo zilivyofanywa na pia haionyeshi zilifanywa mara ngapi. (Yuda 12) Hazikuamriwa na Bwana Yesu Kristo wala mitume wake, na ni wazi kwamba hazipaswi kuonwa kuwa takwa wala jambo la kudumu. Baadhi ya watu wanasema kwamba karamu hizo zilifanywa na Wakristo waliokuwa matajiri na wakawaalika waamini wenzao ambao walikuwa maskini. Wote pamoja, watoto ambao hawakuwa na baba, wajane, matajiri, na maskini walikula pamoja kwenye meza iliyokuwa na vyakula vingi wakifurahia undugu wao.

it-2 816

Mwamba

Neno lingine la Kigiriki, spi·lasʹ, linarejelea mwamba au matumbawe yaliyofichika majini. Yuda aliyatumia kuwafafanua watu fulani ambao waliingia kutanikoni wakiwa na nia mbaya. Kama vile miamba iliyojificha ilivyo tishio kwa meli, vivyo hivyo wanaume hao walikuwa hatari kwa kutaniko. Alisema hivi kuhusu watu wa namna hiyo: “Hao ndio miamba iliyo chini ya maji katika karamu zenu za kuonyesha upendo wanapokula nanyi.”—Yuda 12.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki