Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb21 Machi uku. 15
  • Chagua Marafiki Wako kwa Hekima

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Chagua Marafiki Wako kwa Hekima
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2021
  • Habari Zinazolingana
  • Tii Vielelezo vya Kuonya Leo
    Huduma Yetu ya Ufalme—2002
  • Je, Unaweza Kuwa Kama Finehasi Unapokabili Hali Ngumu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Chagua Marafiki Wako kwa Hekima
    Furahia Maisha Milele!—Masomo ya Kujifunza Biblia
  • Je, Mtu Mmoja Anaweza Kubadili Mambo?
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2021
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2021
mwb21 Machi uku. 15
Wanawake Wamoabu wakiwaalika wanaume Waisraeli wawafuate.

MAISHA YA MKRISTO

Chagua Marafiki Wako kwa Hekima

Kilichowapata Waisraeli kwenye nyanda za Moabu ni kielelezo cha kuonya kwa Wakristo. (1Ko 10:6, 8, 11) Baadhi ya Waisraeli walishawishiwa kutenda dhambi nzito kwa sababu walianza kushirikiana na wanawake Wamoabu waliokuwa na maadili mapotovu na walioabudu sanamu. Hilo lilisababisha madhara makubwa. (Hes 25:9) Tumezungukwa na wafanyakazi, wanafunzi, majirani, watu wa ukoo, na marafiki ambao hawamwabudu Yehova. Tunaweza kujifunza nini kutokana na simulizi hili la Biblia kuhusu hatari za kushirikiana kwa ukaribu na watu kama hao?

TAZAMENI VIDEO YENYE KICHWA VIELELEZO VYA KUONYA LEO—KISEHEMU, KISHA MJIBU MASWALI YAFUATAYO:

  • Picha kutoka kwenye video ‘Vielelezo vya Kuonya Leo​—Kisehemu.’ Zimri akimweleza Yamini pamoja na wengine kuhusu wanawake Wamoabu.

    Zimri na wengine walimwonyesha Yamini mtazamo gani mbaya?

  • Picha kutoka kwenye video ‘Vielelezo vya Kuonya Leo​—Kisehemu.’ Finehasi akizungumza na Yamini.

    Finehasi alimsaidiaje Yamini kuwa na mtazamo unaofaa?

  • Kuna tofauti gani kati ya kumwonyesha mtu ambaye si mwamini urafiki na kuwa rafiki yake?

  • Kwa nini tunapaswa kuwa waangalifu tunapochagua marafiki hata kutanikoni?

  • Kwa nini tunapaswa kuepuka vikundi vya mazungumzo kwenye mitandao ya kijamii na watu tusiowafahamu?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki