Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 10/02 uku. 7
  • Tii Vielelezo vya Kuonya Leo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Tii Vielelezo vya Kuonya Leo
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2002
  • Habari Zinazolingana
  • Yehova Anawabariki Walio Waaminifu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Chagua Marafiki Wako kwa Hekima
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2021
  • Video Inayopaswa Kufikiriwa kwa Uzito
    Huduma ya Ufalme—2006
  • Jifunze Kutokana na Makosa ya Waisraeli
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—2002
km 10/02 uku. 7

Tii Vielelezo vya Kuonya Leo

Sisi sote twaweza kuimarisha azimio letu la kubaki tukiwa waaminifu kwa kutii masomo yapatikanayo kwenye kitabu cha Hesabu sura ya 25. Tafadhali soma Hesabu sura ya 25 na habari inayohusiana nayo kwenye Insight on the Scriptures, Buku la 2, ukurasa wa 419, fungu la 3-5, au Kila Andiko, ukurasa wa 34-35, fungu la 27, 28 na 36. Kisha ujibu maswali haya: Wamoabi walikuwa nani, na kwa nini Yehova alimwambia Musa asipigane nao? (Kum. 2:9) Balaamu alitungaje mbinu ya kutumia Wamoabi waliharibu taifa la Israeli? Kwa nini hatupaswi kusahau kwamba Waisraeli wengi walishindwa na jaribu muhimu kabla tu ya kuingia Bara Lililoahidiwa?—1 Kor. 10:11, 12.

Fikiria sehemu nne zifuatazo za maisha ambazo lazima tuzitilie sana maanani leo ikiwa twataka kuwa waaminifu na kufurahia kibali cha Mungu. (1) Mtazamo: Waisraeli wengine walionyeshaje mtazamo mbaya kuelekea Yehova na mipango yake? Badala yake, twapaswa kujitahidi kuonyesha mtazamo gani? (2) Mashirika: Kwa nini Yehova hakutaka Waisraeli wafanye urafiki na Wamoabi? (Kut. 34:12; Mit. 13:20) Kwa nini tuchague marafiki zetu kwa hekima? (3) Maadili: Mashirika mabaya yalifanya Waisraeli wapatao 23,000 watumbukie katika dhambi gani? (1 Kor. 10:8) Baadhi ya watu wa Mungu leo wameshawishiwaje wakatumbukia katika ukosefu wa maadili, lakini twaweza kujilindaje? (4) Ibada: Waisraeli walijaribiwaje kuhusiana na usafi wa ibada yao? Ni ibada gani ya sanamu yenye ujanja ambayo huenda wengine leo wakajihusisha nayo, lakini twaweza kuiepukaje?—Kol. 3:5.

Katika drama tuliyoona kwenye kusanyiko lililopita, Yamini alibarikiwaje kwa uaminifu wake wa maadili? Tunapopokea video Warning Examples fanya mpango ili wewe na familia yako mwitazame tena na tena.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki