Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha
© 2024 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
NOVEMBA 4-10
HAZINA ZA NENO LA MUNGU ZABURI 105
it-2 1201 ¶2
Neno
Uumbaji wenye uhai na usio na uhai unaongozwa na neno la Mungu, naye anaweza kuutumia kutimiza kusudi lake. (Zb 103:20; 148:8) Neno lake ni lenye kutegemeka; Mungu anapotoa ahadi hasahau kuitekeleza. (Kum 9:5; Zb 105:42-45) Kama tu Mungu mwenyewe alivyosema, neno lake “linadumu milele”; haliwezi kurudi kwake bila kutimiza kusudi lake.—Isa 40:8; 55:10, 11; 1Pe 1:25.
NOVEMBA 18-24
HAZINA ZA NENO LA MUNGU ZABURI 107-108
Hazina za Kiroho
it-2 420 ¶4
Moabu
Baadaye, Daudi alipotawala akiwa mfalme, kuliendelea kuwa na vita kati ya Israeli na Moabu. Daudi aliwatiisha Wamoabu, nao walimletea ushuru. Yaelekea mwishoni mwa vita hivyo, Daudi aliua theluthi mbili ya wanaume Wamoabu walioenda vitani. Huenda aliwaambia walale chini ardhini katika mstari mmoja na kupima urefu wa mstari huo kisha akakadiria urefu wa theluthi mbili na kuwaua. Alihifadhi theluthi moja ya wanaume waliobaki. (2Sa 8:2, 11, 12; 1Nya 18:2, 11) Inawezekana kwamba wakati wa vita hivyo ndipo Benaya mwana wa Yehoyada “aliwaua wana wawili wa Arieli wa Moabu.” (2Sa 23:20; 1Nya 11:22) Ushindi huo dhidi ya Moabu ulikuwa utimizo wa unabii wa Balaamu uliotolewa miaka 400 kabla: “Nyota itatoka kwa Yakobo, na fimbo ya ufalme itainuka katika Israeli. Naye hakika atapasua paji la uso la Moabu na fuvu la kichwa la wana wote wa vurugu.” (Hes 24:17) Pia, kuhusu ushindi huo, yaelekea mtunga-zaburi alirejelea Moabu kuwa “beseni [la Mungu] la kuogea.”—Zb 60:8; 108:9.
NOVEMBA 25–DESEMBA 1
HAZINA ZA NENO LA MUNGU ZABURI 109-112
Hazina za Kiroho
it-1 524 ¶2
Agano
Agano la Kuwa Kuhani Aliye Kama Melkizedeki. Agano hili linapatikana kwenye Zaburi 110:4. Kwenye Waebrania 7:1-3, 15-17 mwandikaji wa kitabu cha Waebrania anaonyesha mstari huo unamhusu Kristo. Ni agano kati ya Yehova na Yesu pekee. Yesu alilirejelea alipokuwa akifanya agano kwa ajili ya ufalme kati yake na wafuasi wake. (Lu 22:29) Yehova aliapa kwamba Yesu Kristo, Mwana wake wa kimbingu, angekuwa kuhani aliye kama Melkizedeki. Melkizedeki alikuwa mfalme na kuhani wa Mungu duniani. Yesu Kristo pia angewekwa kuwa Mfalme na Kuhani Mkuu mbinguni, si duniani. Aliwekwa rasmi aliporudi mbinguni. (Ebr 6:20; 7:26, 28; 8:1) Agano hilo linatumika milele, kwa kuwa Yesu atatenda chini ya mwelekezo wa Yehova akiwa Mfalme na Kuhani milele.—Ebr 7:3.