Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb25 Mei kur. 10-11
  • Juni 9-15

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Juni 9-15
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2025
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2025
mwb25 Mei kur. 10-11

JUNI 9-15

METHALI 17

Wimbo 157 na Sala | Utangulizi (Dak. 1)

HAZINA ZA NENO LA MUNGU

Wenzi wa ndoa katika Israeli la kale wakifurahia kula mkate katika nyumba yao isiyo ya kifahari.

Wenzi wa ndoa Waisraeli wakifurahia mlo mwepesi katika mazingira yenye amani

1. Furahia Amani Katika Ndoa Yako

(Dak. 10)

Kudumisha amani kunahitaji jitihada nyingi, lakini mkifanya hivyo mtanufaika (Met 17:1; ona picha)

Epuka kubishana kuhusu mambo madogo-madogo (Met 17:9; g 9/14 11 ¶2)

Dhibiti hisia zako (Met 17:14; w08 5/1 10 ¶6–11 ¶1)

Wenzi wa ndoa matajiri katika nyakati za Biblia na wasio na furaha, wameketi kwa ajili ya mlo wenye mambo mengi. Wote wawili wamekunja mikono yao, na mke anatazama upande mwingine kwa dharau mume wake anapozungumza.

2. Hazina za Kiroho

(Dak. 10)

  • Met 17:24—Ni katika njia gani “macho ya mpumbavu hutangatanga mpaka kwenye miisho ya dunia”? (it-1 790 ¶2)

  • Ungependa kushiriki nasi hazina gani kutoka kwenye usomaji wa Biblia wa juma hili?

3. Usomaji wa Biblia

(Dak. 4) Met 17:​1-17 (th somo la 10)

BORESHA HUDUMA YAKO

4. Kuanzisha Mazungumzo

(Dak. 3) MAHUBIRI YASIYO RASMI . (lmd somo la 3 jambo kuu la 5)

5. Kuanzisha Mazungumzo

(Dak. 4) MAHUBIRI YA UMMA . Anzisha funzo la Biblia. (lmd somo la 6 jambo kuu la 4)

6. Hotuba

(Dak. 5) ijwbv makala ya 60—Kichwa: Ni Nini Maana ya Methali 17:17? (th somo la 13)

MAISHA YA MKRISTO

Wimbo 113

7. Sitawisha Mazoea Yatakayokusaidia Kuwa na Mawasiliano Mazuri

(Dak. 15) Mazungumzo.

Ni muhimu kuwa na mawasiliano mazuri ili uwe na familia yenye furaha. Washiriki wa familia wanapowasiliana waziwazi, wanaweza kutimiza malengo yao pamoja na kutegemezana wanapokabili hali ngumu. (Met 15:22) Unaweza kufanya nini katika familia yako ili kila mtu ajihisi huru kueleza mawazo na hisia zake waziwazi?

Tumieni wakati pamoja. (Kum 6:​6, 7) Washiriki wa familia wanapofanya kazi, wanaposhiriki katika utendaji wa kiroho, na kufurahia pamoja, wanakuwa na uhusiano wa karibu zaidi, wanapendana na kuaminiana. Pia, hilo linatokeza nafasi za kuwa na mazungumzo yenye kustarehesha. Pindi nyingine, huenda ukahitaji kuwa tayari kufanya jambo ambalo wengine katika familia wangependa, badala ya kile ambacho wewe ungependa, kufanya hivyo kutakuwa na manufaa ya muda mrefu! (Flp 2:​3, 4) Mnawezaje kutumia muda wenu vizuri mkiwa pamoja?—Efe 5:​15, 16.

Picha kutoka kwenye video yenye kichwa “Fuata Ramani Inayoongoza Familia Iwe na Maisha Yenye Amani​—⁠Boresha Mawasiliano.” Familia ikifurahia mlo pamoja.

Onyesha VIDEO Fuata Ramani Inayoongoza Familia Iwe na Maisha Yenye Amani—Boresha Mawasiliano. Kisha waulize wasikilizaji:

  • Matumizi mabaya ya vifaa vya kielektroni yanawezaje kuathiri mawasiliano katika familia?

  • Umejifunza nini kingine kuhusu kuwa na mawasiliano mazuri katika video hii?

Uwe msikilizaji mzuri. (Yak 1:19) Mara nyingi watoto wanakuwa huru zaidi kueleza hisia zao, ikiwa hawaogopi kueleweka vibaya au kuhukumiwa. Hivyo, jitahidi usikasirike ikiwa mtoto wako atasema jambo linalokuhangaisha. (Met 17:27) Badala yake, msikilize kwa huruma. Jitahidi kuelewa mawazo na hisia zake ili umhakikishie au kumsaidia kwa njia ya upendo.

8. Funzo la Biblia la Kutaniko

(Dak. 30) bt sura ya 27 ¶19-22, sanduku uk. 212

Umalizio (Dak. 3) | Wimbo 35 na Sala

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki