Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w22 Februari uku. 31
  • Je, Wajua?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Wajua?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2022
  • Habari Zinazolingana
  • Anafikiria Kupungukiwa Kwetu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Je, Wajua?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2017
  • Kuchungua Mafumbo ya Uhamaji
    Amkeni!—1995
  • Hata Ndege ‘Wanajua Wakati Wao’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2022
w22 Februari uku. 31

Je, Wajua?

Kwa nini kutoa njiwa tetere na hua kama matoleo yanayokubalika ulikuwa mpango wenye manufaa?

CHINI ya Sheria ya Musa, njiwa tetere na hua walikubalika kuwa matoleo kwa Yehova. Sikuzote ndege hao wawili walitajwa pamoja katika sheria kuhusu dhabihu na mmoja angeweza kutumiwa badala ya mwingine. (Law. 1:14; 12:8; 14:30) Kwa nini hilo lilikuwa na manufaa? Sababu moja ni kwamba njiwa tetere hawakupatikana kwa urahisi nyakati zote. Kwa nini?

Njiwa tetere

Njiwa tetere ni ndege wanaohamahama ambao katika miezi ya joto wanapatikana katika maeneo yote nchini Israeli. Katika mwezi wa Oktoba, wanahamia kusini katika nchi zenye joto zaidi, na kurudi Israeli wakati majira ya kuchipua. (Wim. 2:11, 12; Yer. 8:7) Katika Israeli la kale, hilo lilimaanisha kwamba haikuwa rahisi kwa Waisraeli kutoa dhabihu ya njiwa tetere wakati wa majira ya baridi.

Hua

Kwa upande mwingine, kwa kawaida hua hawahami, hivyo walipatikana nchini Israeli mwaka mzima. Zaidi ya hilo, hua walikuwa ndege waliofugwa. (Linganisha Yohana 2:14, 16.) Kulingana na kitabu Bible Plants and Animals, “vijiji na miji yote huko Palestina ilikuwa na hua waliofugwa. Kila nyumba ilikuwa na tundu au kiota cha njiwa kwenye ukuta, ambamo njiwa wangeishi.”​—Linganisha Isaya 60:8.

Hua kwenye kiota chake

Hivyo, Yehova alionyesha kwamba ni mwenye upendo na usawaziko kwa kukubali matoleo ya ndege ambao walipatikana kwa urahisi mwaka mzima katika nchi ya Israeli.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki