Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w25 Januari uku. 32
  • Chora Picha Ili Zikusaidie Kukumbuka

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Chora Picha Ili Zikusaidie Kukumbuka
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2025
  • Habari Zinazolingana
  • “Kumkaribia Mungu Ni Jambo Jema” Kwetu!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2025
  • Unaweza Kuboresha Kumbukumbu Lako!
    Amkeni!—2009
  • Jinsi ya Kuboresha Kumbukumbu Lako
    Amkeni!—1995
  • “Hakuwa Akisema Nao Bila Mfano”
    ‘Njoo Uwe Mfuasi Wangu’
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2025
w25 Januari uku. 32

DOKEZO LA KUJIFUNZA

Chora Picha Ili Zikusaidie Kukumbuka

Kama wengi wetu, huenda ni vigumu kwako kukumbuka mambo unayojifunza. Lakini je, umetambua kwamba ni rahisi kukumbuka mambo ambayo Yesu alifundisha kwa sababu mara nyingi alitumia mifano? Unaweza kuwazia mifano hiyo akilini, na hilo linakusaidia kukumbuka. Vivyo hivyo, unaweza kukumbuka mambo mengi zaidi unayojifunza kwa kuyawazia au kwa kupiga picha akilini mambo hayo. Unawezaje kufanya hivyo? Kwa kuchora picha unapojifunza.

Watu wanaochora picha za mambo mapya wanayojifunza, mara nyingi huyakumbuka vizuri zaidi. Njia hii ya kuchora huwasaidia kukumbuka maneno na mambo makuu waliyojifunza. Picha zao si kazi za sanaa, badala yake wanachora picha rahisi tu. Na uthibitisho unaonyesha kwamba watu wenye umri mkubwa hasa wanaweza kunufaika na mbinu hii.

Wakati ujao unapojifunza, unaweza kujaribu kuchora picha za mambo utakayojifunza. Utashangaa kuona jinsi utakavyokumbuka mambo mengi!

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki