Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • yb15 uku. 24-uku. 27 fu. 1
  • Mkutano Mkubwa Zaidi wa Mashahidi wa Yehova

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mkutano Mkubwa Zaidi wa Mashahidi wa Yehova
  • 2015 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
  • Habari Zinazolingana
  • Mashahidi wa Yehova Tengenezo Linalotegemeza Jina
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Video Mpya kwa Ajili ya Kuanzisha Mafunzo ya Biblia
    Huduma Yetu ya Ufalme—2014
  • Programu za Kusanyiko la Eneo Ambazo Watu ‘Wanasikia na Kuona’
    Jinsi Michango Yako Inavyotumiwa
  • Jitihada Yake Ilileta Thawabu
    Amkeni!—2002
Pata Habari Zaidi
2015 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
yb15 uku. 24-uku. 27 fu. 1
Picha katika ukurasa wa 24

MATUKIO MUHIMU YA MWAKA ULIOPITA

Mkutano Mkubwa Zaidi wa Mashahidi wa Yehova

JUMAMOSI, Oktoba 5, 2013, watu 257,294 kutoka nchi 21 walihudhuria mkutano wa 129 wa kila mwaka wa Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania. Baadhi ya wasikilizaji hao walikuwepo kwenye mkutano huo na wengine walisikiliza moja kwa moja kupitia Intaneti. Mwisho juma uliofuata, Mashahidi wengine waliokusanyika walitazama rekodi ya programu hiyo. Kwa ujumla, watu 1,413,676 kutoka nchi 31 walisikiliza programu hiyo—hakujawahi kuwa na mkutano mkubwa hivyo wa Mashahidi wa Yehova.

Tangu miaka ya 1920, Mashahidi wa Yehova wametangaza programu za makusanyiko kupitia simu na vituo vya redio kwa wasikilizaji walio maeneo mbalimbali duniani. Sasa, teknolojia ya Intaneti imefanya iwe rahisi hata kwa watu wanaoishi mbali sana kusikiliza na kuona matukio yanapofanyika au baadaye kidogo.

Washiriki wa ofisi kadhaa za tawi walifanya kazi kwa zaidi ya mwaka ili kuunda mfumo wa kupeperusha video kupitia Intaneti. Katika mwisho juma wa mkutano huo wa mwaka, mafundi wa mitambo walielekeza mfumo wa kupeperusha programu hiyo wakiwa jijini Brooklyn, New York, na walifanya kazi usiku na mchana kwa kuwa programu hiyo ilionyeshwa katika maeneo 15 mbalimbali duniani yanayotofautiana kwa saa.

Taarifa Fupi—Maeneo Yaliyounganishwa kwa Intaneti

  • Ulipofanyika: Jumba la Kusanyiko la Mashahidi wa Yehova la Jersey City, New Jersey, Marekani Hudhurio: 4,732

  • Wahudhuriaji wengi zaidi: Jiji la Perth, Australia Hudhurio: 7,186

  • Upande wa kaskazini: Fairbanks, Alaska, Marekani Hudhurio: 255

  • Upande wa kusini: Jiji la Invercargill, New Zealand Hudhurio: 190

  • Eneo la mbali zaidi: Perth, Australia, umbali wa kilometa 18,700 hivi kutoka Jersey City

Jinsi Mfumo Huo Unavyofanya Kazi

  1. Kamera kadhaa hunasa video za programu.

  2. Video hutumwa kwenye kifaa cha kuchuja video, na video bora huchaguliwa.

  3. Kisha video zilizochaguliwa hupitishwa kwenye kompyuta iliyo kwenye kituo cha mafundi wa mitambo.

  4. Mawimbi ya video yenye ubora wa chini, ubora wa kati, na bora zaidi ya programu hiyo yanaandaliwa.

  5. Video hizo zinagawanywa katika vipande vya sekunde kumi-kumi.

  6. Kisha vipande hivyo vinapakiwa kwenye Intaneti kupitia mfumo wa Mitandao ya Intaneti.

  7. Katika kila eneo ambako programu hiyo inatazamwa, kuna kifaa kinachopakua vipande vya video kutoka kwenye Intaneti na kuvihifadhi. Kisha kifaa hicho huunganisha tena vipande vya video hizo ili zicheze kwa mtiririko mzuri.

  8. Wahudhuriaji wanaona na kusikiliza programu.

Mchoro katika ukurasa wa 26, 27
    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki