Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • yb17 kur. 132-133
  • Nilihisi Nimefanikiwa Maishani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Nilihisi Nimefanikiwa Maishani
  • 2017 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
  • Habari Zinazolingana
  • Georgia—Urithi wa Kale Uliohifadhiwa
    Amkeni!—1998
  • Mnyanyaso wa Kidini Huko Georgia Utaendelea Hadi Lini?
    Amkeni!—2002
  • Niliona kwa Macho Yangu Mwenyewe Kile Ambacho Biblia Inasema!
    2017 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
  • Kutafuta Mwongozo wa Yehova
    2017 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
Pata Habari Zaidi
2017 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
yb17 kur. 132-133

GEORGIA

Nilihisi Nimefanikiwa Maishani

Madona Kankia

  • ALIZALIWA 1962

  • ALIBATIZWA 1990

  • HISTORIA FUPI Mwanzoni alikuwa mwanachama wa chama cha Kikomunisti nchini Georgia, lakini baadaye alisaidia watu wengi kujifunza kweli. Mwaka 2015, alihitimu darasa la kwanza la Shule ya Waeneza-Injili wa Ufalme jijini Tbilisi.

Madona Kankia

NILIPOSIKIA kuhusu kweli kwa mara ya kwanza, mwaka 1989, nilikuwa na cheo cha juu katika Chama cha Kikomunisti katika mji nilioishi wa Senaki, na nilishiriki kwa ukawaida kwenye Kamati Maalumu ya Muungano wa Sovieti nchini Georgia, ambayo ilifanana na bunge leo. Pia, nilikuwa ninachumbiwa na kijana fulani, kwa hiyo nilihisi nimefanikiwa maishani.

Baba na Mama walinizoeza kumpenda Mungu. Hivyo, niliamini kuna Mungu, ingawa nilikuwa Mkomunisti. Nilipoanza kujifunza Biblia, nilipata majibu yenye kuridhisha ya maswali yangu yote, kwa hiyo nikaamua kujiweka wakfu kwa Yehova. Lakini familia, marafiki, wafanyakazi wenzangu, na mchumba wangu hawakukubaliana na uamuzi niliofanya.

Imani yangu mpya ilifanya watu wa familia wanitenge, na vilevile haikupatana na mambo ya kisiasa. Hivyo, niliamua kuondoka nyumbani, kuvunja uchumba, kuacha kazi, na kujiuzulu kwenye chama na Kamati Maalumu ya Muungano wa Sovieti. Baada ya kubatizwa, mkazo kutoka kwa marafiki na familia uliongezeka. Kwa kuwa nilifahamika sana katika eneo nililokuwa nikiishi, niliamua kuhamia jiji la Kutaisi, na mara moja nikaanza upainia.

Watu wanaponiuliza ikiwa imani yangu ni yenye thamani sana hivi kwamba nivumilie changamoto nilizokabili, mimi huwajibu bila kusita kwamba nafurahia kabisa uamuzi niliofanya. Ingawa wazazi wangu hawakuelewa maamuzi niliyofanya, ninashukuru kwamba walinizoeza kumpenda Mungu na jirani. Hilo limenisaidia sana maishani.

Madona Kankia akiongoza funzo la Biblia na mwanamke fulani
    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki