Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 1/22 kur. 24-25
  • Georgia—Urithi wa Kale Uliohifadhiwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Georgia—Urithi wa Kale Uliohifadhiwa
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Mnyanyaso wa Kidini Huko Georgia Utaendelea Hadi Lini?
    Amkeni!—2002
  • Maandishi ya Kale Yenye Thamani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • “Miujiza” Miwili Kwenye Kusanyiko Moja Huko Georgia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
  • Nilihisi Nimefanikiwa Maishani
    2017 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 1/22 kur. 24-25

Georgia—Urithi wa Kale Uliohifadhiwa

NA MLETA-HABARI WA AMKENI!

JE! UNGEPENDEZWA kuishi katika nchi yenye mabonde yaliyo na rutuba yaliyopakata miongoni mwa milima yenye theluji, iliyo na urefu wa meta 4,600, ambapo watu fulani huishi kufikia umri wa miaka 100 na zaidi? Kwa wakazi wa Georgia, hii si ndoto tu. Ni jambo halisi.

Georgia iko kandokando ya mpaka wa kijiografia na kitamaduni kati ya Ulaya na Asia. Katika nyakati za kale, Georgia ilikuwa mahali pa tukio la maana kwenye ile Barabara ya Hariri yenye sifa, ileile ambayo Marco Polo alishika kwenda China. Georgia ilinufaika kiuchumi na kitamaduni kutokana na uhusiano huu kati ya Mashariki na Magharibi, lakini nyakati nyingine wavamizi pia walipata kuwa inastahili kupita njia hii. Kulingana na kadirio moja, jiji kuu la Georgia, Tbilisi, limeharibiwa mara 29! Leo, Tbilisi ni jiji lenye pilikapilika na changamfu, likijisifia treni ya chini kwa chini na majengo ya kisasa yaliyochangamana na nguzo za ukumbusho zilizodumu muda mrefu.

Baadhi ya asilimia 87 ya mandhari ya Georgia ni yenye milima. Kutoka nyanda za juu zenye kufunikwa na barafu na zilizo ukiwa kupitia nyanda za chini hutiririka mito 25,000 mingi ikiwa imejaa samaki. Zaidi ya thuluthi ya nchi ni yenye misitu au imefunikwa na kichaka. Safu ya milima ya Caucasus kwenye mpaka wa kaskazini wa Georgia hukinga bara ya nchi lisipatwe na halihewa baridi inayokuja kutoka kaskazini. Hali hii huruhusu kupashwa joto kwa magharibi mwa Georgia na hewa nyevunyevu kutoka kwenye Bahari Nyeusi—sababu moja ifanyayo Georgia iwe kikomo cha safari chenye kupendwa sana na waenda-likizoni. Tabia ya nchi yenye kupendeza imechangia pia mojawapo ya mapokeo ya kale zaidi na bora zaidi katika utengenezaji wa divai. Kwa kweli, Georgia hutokeza zaidi ya unamna-namna 500 wa zabibu na divai!

Hata hivyo rasilimali kubwa kupita zote za Georgia, ni watu wake. Wamejulikana kupitia enzi kwa ajili ya ushujaa wao, akili zao, na ukunjufu wa moyo katika ukaribishaji-wageni, vilevile kwa ajili ya ucheshi wao na kupenda maisha. Utamaduni wao ni wenye utele katika wimbo na dansi, na nyimbo za kitamaduni bado huimbwa mara nyingi wakati watu waketipo kuzunguka meza baada ya milo katika nyumba za Georgia.

Georgia pia ina historia ndefu ya maandishi, inayoanzia karne ya tano. Kigeorgia ni mojawapo lugha za mapema zaidi ambayo katika hiyo Biblia ilitafsiriwa, ikitumia ile alfabeti ya Kigeorgia iliyo ya kipekee na maridadi. Utamaduni huu wote hufanyiza unganisho halisi na historia iliyopita ya Georgia—urithi wa kale uliohifadhiwa katika nchi ya kisasa.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 24]

Pat O’Hara/Corbis

[Picha katika ukurasa wa 25]

1. Biblia ya Kigeorgia

2. Wakazi fulani huishi kufikia umri wa miaka 100 na zaidi!

3. Barabara yenye shughuli nyingi katika Tbilisi

[Hisani]

Dean Conger/Corbis

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki