MALAKI YALIYOMO 1 Yehova anawapenda watu wake (1-5) Makuhani watoa dhabihu zisizofaa (6-14) Jina la Mungu litakuwa kuu miongoni mwa mataifa (11) 2 Makuhani washindwa kuwafundisha watu (1-9) Midomo ya kuhani inapaswa kulinda ujuzi (7) Watu wawataliki wake zao bila msingi (10-17) “‘Ninachukia talaka,’ asema Yehova” (16) 3 Bwana wa kweli aja kutakasa hekalu lake (1-5) Mjumbe wa agano (1) Washauriwa wamrudie Yehova (6-12) Yehova habadiliki (6) “Nirudieni, nami nitawarudia” (7) ‘Leteni sehemu yote ya kumi, na Yehova atawamwagia baraka’ (10) Mwadilifu na mwovu (13-18) Majina yaandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha Mungu (16) Tofauti kati ya mwadilifu na mwovu (18) 4 Kuja kwa Eliya kabla ya siku ya Yehova (1-6) “Jua la uadilifu litawaangazia” (2)