Sababu Gani Hua?
Mara Yesu alipokwisha kubatizwa katika maji, “[roho takatifu ikashuka] juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua.” (Luka 3:22) Labda kushuka huku kwa roho kulifananishwa na kupigapiga kwa mabawa ya hua au njiwa anapokaribia kituo chake.
Hua au njiwa walitumiwa na Waisraeli wa kale kwa makusudi ya dhabihu. (Marko 11:15; Yohana 2:14-16) Ndege huyo alifananisha hali ya kutokuwa na hatia na hali ya kutokuwa na uchafu, kama aliyeachiliwa na Nuhu kutoka safinani aliyerudi akiwa na jani la “Iweni . . . wapole kama hua” au njiwa. (Mt. 10:16) Alikuwa njiwa aliyeachiliwa na Nuhu kutoka safinani aliyerudi akiwa na jani la mzeituni, kuonyesha kwamba maji ya gharika yalikuwa yakipunguka. (Mwa. 8:11) Hii ilionyesha kwamba wakati wa pumziko na amani ulikuwa karibu, kwa maana ilikuwa imetabiriwa kwa habari ya Nuhu hivi: “Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani [Yehova].” (Mwa. 5:29) Basi, wakati wa kubatizwa kwa Yesu, yule hua au njiwa aliweza kuvuta fikira kwa kufaa kwenye daraka la Yesu kama Masihi, Mwana wa Mungu aliye safi na asiye na dhambi. Na kutoa kwake uhai kwa ajili ya wanadamu kuliweka msingi wa kipindi cha pumziko na chenye amani wakati wa utawala wake kama ufalme.