Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w92 1/15 uku. 31
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Habari Zinazolingana
  • Gharika Kuu
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Alilindwa Akiwa “Salama Pamoja na Wengine Saba”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Sababu Gani Hua?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
w92 1/15 uku. 31

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Ni kwa nini Noa alimtoa kunguru na kisha njiwa nje ya safina?

Biblia haitoi maelezo mengi kuhusu hilo. Hata hivyo, yaonekana kuna usababu wa kiakili katika mwendo wa Noa.

Kwa siku 40 mchana na usiku, dunia ilipatwa na mvua nyingi mno, ikisababisha gharika iliyofunika hata vilele vya milima kwa muda wa miezi mitano. Kisha “safina ikatua juu ya milima ya Ararati.” (Mwanzo 7:6–8:4) Miezi kadhaa baadaye, baada ya ‘vilele vya milima kuonekana,’ Noa “akatoa kunguru, naye akatoka akaenda huko na huko [akawa akienda na kurudi, NW].”—Mwanzo 8:5, 7.

Kwa nini kunguru? Ndege huyo ni mrukaji mwenye nguvu, na aweza kula vyakula vya aina nyingi, kutia na mnofu uliokufa. Noa huenda ikawa alimtoa kunguru ili aone kama angerudi au kubaki mbali na safina, labda akila mabaki ya mizoga iliyopata kufunuliwa wakati maji yalipopunguka na bara likatokea. Hata hivyo, kunguru huyo hakukaa mbali. Biblia husema kwamba alirudi, lakini haisemi kwamba alirudi kwa Noa. Labda alirudi kupumzika juu ya safina kati ya pindi za kuruka kutafuta chakula kilichokuwa kikielea kwenye maji yaliyokuwa mengi bado.

Baadaye, Noa aliamua kumtoa njiwa. Twasoma hivi: “Yule njiwa hakuona mahali pa kutua kwa wayo wa mguu wake, akamrudia Nuhu [Noa, NW] safinani.” (Mwanzo 8:9) Hilo ladokeza kwamba kwa njia yake mwenyewe, njiwa huyo angeweza kutumikia katika kuhakikisha kama maji ya furiko yalikuwa yamepunguka. Njiwa huonyesha kutumaini kwingi wanadamu. Noa angeweza kutazamia kwamba njiwa huyo angerudi, si tu kupumzika juu ya safina, bali kumrudia Noa mwenyewe.

Inasemwa kwamba njiwa hutua kwenye ardhi kavu tu, wanajulikana kuwa huruka chini sana katika mabonde, na kwamba hula mboga. (Ezekieli 7:16) Grzimek’s Animal Life Encyclopedia husema hivi: “Kama ilivyo kweli kuhusu hua na njiwa wote wanaokula mbegu na njugu, kuna tatizo la kula wakati theluji [au maji] inapoendelea kuifunika ardhi kwa zaidi ya siku moja, kwani kingi cha kile kiwezacho kuwa chakula chao hupatikana kwenye ardhi.” Kwa hiyo huenda njiwa huyo akamletea Noa uthibitisho fulani kwamba alipata ardhi kavu au mimea iliyochipuka. Mara ya kwanza ya Noa kumtoa, njiwa huyo alirudi tu kwa Noa safinani. Mara ya pili, njiwa huyo alirudi akiwa na jani la mzeituni. Mara ya tatu, hakurudi, ikitoa ushuhuda kwamba ingewezekana na ilikuwa salama kwa Noa kuondoka safinani.—Mwanzo 8:8-12.

Ingawa wengine huenda wakaona hayo kuwa maelezo ya nasibu, uhakika wa kwamba usimulizi huo ni mahususi sana, bila jitihada ya kutoa maelezo kamili, yaonyesha kuaminika kwa Biblia. Yatupa sisi sababu zaidi za kukubali usimulizi huo, si ukiwa umefanyizwa au kutungwa, bali ukiwa wenye usahihi kikweli. Ukosefu wa maelezo na mambo mengi madogomadogo huonyesha pia ni mambo gani yenye kupendeza ambayo Wakristo waaminifu waweza kutazamia kumwuliza Noa anapofufuliwa na kuweza kueleza yeye mwenyewe sababu za matendo yake.—Waebrania 11:7, 39.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki