Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w04 2/15 uku. 31
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Habari Zinazolingana
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Sababu Gani Hua?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
  • Mzeituni Unaostawi Katika Nyumba ya Mungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Gharika Kuu
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
w04 2/15 uku. 31

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Baada ya Gharika, Noa alimtuma njiwa nje ya safina ambaye alirudi na “jani bichi la mzeituni.” Njiwa huyo alipata wapi jani hilo?

Biblia hutuambia kwamba ‘maji yalizidi mno duniani hivi kwamba milima yote mirefu ambayo ilikuwa chini ya mbingu zote ilifunikwa.’ (Mwanzo 7:19) Maji ya Gharika yalipopungua, Noa alimtuma njiwa mara moja kila juma, kwa muda wa majuma matatu. Mara ya pili, njiwa huyo alirudi akiwa na ‘jani bichi la mzeituni lililokuwa katika mdomo wake. Hivyo, Noa akajua kwamba maji yalikuwa yamepungua kutoka juu ya dunia.’—Mwanzo 8:8-11.

Bila shaka, sasa hatuna namna ya kujua muda ambao maji yalifunika sehemu fulani za dunia, kwa kuwa ni wazi kwamba Gharika ilibadilisha sura ya dunia. Hata hivyo, inaonekana kwamba maji yalifunika sehemu nyingi kwa muda mrefu hivi kwamba miti mingi ilikufa. Lakini yaonekana miti fulani haikufa, na hivyo ikatokeza miche tena maji yalipopungua.

Kichapo, The New Bible Dictionary, kinasema hivi kuhusu mzeituni: “Unapokatwa, miche mipya huchipuka kutoka kwenye shina, hivi kwamba visiki vitano vipya hivi vinaweza kumea. Kwa kawaida, mizeituni [iliyo karibu kufa] hutokeza miche kwa njia hiyo.” Ni “kana kwamba miti hiyo haiwezi kufa,” chasema kichapo The New Schaff-Herzog Encyclopedia of Religious Knowledge. Leo hakuna binadamu anayejua kikamili kuhusu kiasi cha chumvi na joto la maji ya gharika. Hivyo, hatuwezi kuwa na hakika kuhusu jinsi maji hayo yangeweza kuathiri mizeituni na mimea mingine.

Hata hivyo, mzeituni-mwitu hauwezi kustahimili hali ya baridi, kama ile inayopatikana milimani. Kwa kawaida, miti hiyo humea katika maeneo yaliyo chini ya meta 1,000, ambako wastani wa joto ni zaidi ya nyuzi 10 Selsiasi. Kitabu The Flood Reconsidered kinasema, “Hivyo Noa angeweza kujua kutokana na jani lililokuwa limetoka tu kuchumwa kwamba mabonde ya chini yalikuwa yamekauka.” Noa alipomwachilia njiwa juma moja baadaye, njiwa huyo hakurudi, ikionyesha kwamba kulikuwa na mimea mingi zaidi na angeweza kupata mahali pa kutulia.—Mwanzo 8:12.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki