Iache Biblia Ijisemee Yenyewe
Je! Mariamu Alikuwa Mama wa Mungu?
“Kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu [si Mungu].”—Luka 1:35.
Je! Mariamu Alizaliwa Bila Dhambi?
“Mwanamke akitunga mimba na kuzaa mtoto mume, ndipo atakuwa yu najisi siku saba; . . . Kisha hizo siku za kutakaswa kwake zitakapotimia, . . . ataleta mwana-kondoo . . . mlangoni pa hema ya kukutania, na kumpa kuhani . . . Kama mali yake huyo mwanamke haimfikilii mwana-kondoo, hapo ndipo atakapochukua hua wawili, au makinda mawili ya njiwa; mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa, na wa pili kuwa sadaka ya dhambi; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atakuwa safi.” (Mambo ya Walawi 12:2, 6, 8) “Kisha, zilipotimia siku za kutakasika kwao, kama ilivyo torati ya Musa, [Yusufu na Mariamu] walikwenda naye hata Yerusalemu, wamweke kwa Bwana . . . wakatoe na sadaka, kama ilivyonenwa katika sheria ya Bwana, Hua wawili au makinda ya njiwa wawili [mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa, na wa pili kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya Mariamu].”—Luka 2:22, 24.
Baada ya Kuzaliwa kwa Yesu, je! Mariamu Aliendelea Kuwa Bikira?
”[Yusufu] akamchukua mkewe; asimjue kamwe [“hakuwa amefanya ngono pamoja naye”—Jerusalem Bible ya Kikatoliki] hata alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU.”—Mathayo 1:24, 25.
Je! Mariamu Alizaa Watoto Wengine Baada ya Kuzaliwa Yesu?
“Akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto.” (Luka 2:7) “Huyu si mwana wa seremala? mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze [Kigiriki: adelphoi “ndugu,” si syngenes, “ukoo” wala “binamu”] si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda? Na maumbu [akina dada] yake wote hawapo hapa petu?”—Mathayo 13:55, 56.
Kwa Kusema “Nduguze,” Ingeweza Kuwa Kwamba Biblia Inamaanisha Wanafunzi wa Yesu, Ndugu Zake za Kiroho?
“Baada ya hayo akashuka mpaka Kapernaumu, yeye na mama yake na ndugu zake na wanafunzi wake.” (Yohana 2:12) “Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa, uende Uyahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya. Maana hata nduguze hawakumwamini.”—Yohana 7:3, 5.
Je! Mwili wa Asili wa Mariamu Ulipelekwa Mbinguni?
“Kadhalika na kiyama [ufufuo] ya wafu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika; hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ndugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu.”—1 Wakorintho 15:42, 44, 50.
Je! Sala Zipelekwe kwa Mariamu?
“Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.”—Yohana 14:6, 13.