Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g90 5/8 kur. 5-6
  • Afya Ni Nini?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Afya Ni Nini?
  • Amkeni!—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Afya na Mtindo-Maisha
  • Dumisha Imani na Afya Yako ya Kiroho
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Afya Njema—Waweza Kuifanyia Nini?
    Amkeni!—1990
  • Sisi Ni Wenye Afya Kiasi Gani?
    Amkeni!—1990
  • Uwe na Maoni Yanayopatana na Maandiko Kuhusu Matibabu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1990
g90 5/8 kur. 5-6

Afya Ni Nini?

JE! KWELI mtu ana afya njema kwa sababu tu hahisi akiwa mgonjwa? Basi, ni mara ngapi wewe umesikia juu ya watu mmoja mmoja walioelekea kuwa na maungo yenye afya kabisa lakini kwa ghafula wakafa kwa kisababishi kisichotarajiwa? Ripoti zaonyesha kwamba karibu sehemu moja kwa tano za wale wanaokufa kwa ugonjwa wa moyo kila mwaka hawakuonyesha kidalili chochote cha kwamba walikuwa na kasoro. Ni wazi kwamba kuhisi vema au hali nzuri hakuthibitishi kabisa kwamba mtu ana afya njema.

Kielelezo ni mchezaji mmoja wa miaka 22 wa mpira wa vikapu katika koleji. Kulingana na viwango vyote vya kawaida, yeye angefikiriwa kuwa mtu mwenye afya katika muda wa usitawi wake. Lakini usiku mmoja akafa—kwa ghafula. Uchunguzi ulifunua kwamba kisababishi cha kifo kilikuwa kuzidisha kipimo cha dawa. Ingawa alikuwa katika hali nzuri kabisa, je! alikuwa akiishi maisha yenye afya? Sivyo.

Basi, afya ni zaidi ya kutokuwa mgonjwa tu. Bila shaka, urithi na mazingira vyahusika, lakini chini ya hali za kawaida, labda njia yetu ya maisha ndilo jambo moja la maana zaidi linaloongoza afya yetu. Tulacho au tunywacho, kadiri ya utendaji wetu, kadiri ya pumziko tupatalo, jinsi tuitikiavyo mkazo, na tabia nyingine za kibinafsi ama zitaongezea ama zitaharibu afya yetu. Hivyo, kwa kadiri kubwa, afya yetu huwa vile sisi twaifanyiza. Kanuni ya Biblia, “Cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna,” yatumika pia kwa afya yetu ya kimwili.—Wagalatia 6:7.

Afya na Mtindo-Maisha

Mathalani, yajulikana vizuri kwamba katika kampuni nyingi za Kijapani, wafanya kazi huwa na kawaida za mazoezi makali sana kila siku. Tokeo? “Upo uthibitisho mwingi wa takwimu za kuthibitisha lile oni la kwamba wafanya kazi Wajapani ndio wenye afya zaidi ya wengine ulimwenguni,” lasema gazetihabari Asiaweek. Kwa upande mwingine, ripoti hiyo yaonyesha kwamba katika Japani “kansa ndicho kisababishi cha kifo kama kimoja hivi katika vinne; shambulio-moyo na kamata ni kifo kimoja katika vitano, na kimoja katika kumi na viwili ni ugonjwa wa kupumua. Mwanamume mmoja katika kila 52 hujiua mwenyewe (kwa wanawake, visa vya kujiua ni kimoja katika 70).”

Je! taarifa hizi zaelekea kutopatana au hata kupingana? Sivyo hasa, tuchunguzapo mambo ya uhakika. Ikiwa na asilimia 40 ya ngumbaru wote wenye kupuliza sigareti milioni elfu 300 kwa mwaka, Japani ndiyo ya pili ulimwenguni pote (kwa kufuata Ugiriki) katika wastani wa kila mtu mwenye kutumia sigareti. Zaidi ya hilo, kila mwaka wanaume Wajapani hunywa chupa milioni elfu 8 za pombe na kwati milioni elfu 1.6 za pombe ya mchele-chachu. Hii yalingana na kutwaa karibu nusu ya kwati moja ya alkoholi safi kwa kila mtu kwa juma. Lingekuwa jambo la kushangaza sana kama mazoea hayo yenye madhara hayakuwa na athari juu ya afya ya watu.

Ingawa huenda ikabishwa kwamba Wajapani ndio wenye tarajio kubwa zaidi la kuishi maisha marefu kuliko watu wengine wowote na kwamba kadiri zao za kutumia tumbako na alkoholi ziko chini kuliko za baadhi ya wengine, ulinganisho huo mwishowe hauna maana yoyote. Uhakika ni kwamba watu wanakufa bila kukomaa na isivyo lazima. Huenda wakaonekana kuwa wenye afya kuliko wengine, lakini je! kwa kweli ni wenye afya?

Basi, ni wazi kwamba afya yetu huonyesha ujumla wa mtindo-maisha wetu na tabia zetu za siku kwa siku. Afya njema yahusisha njia ya maisha yenye usawaziko ambayo hutokeza halinjema yetu ya kimwili, kiakili, kihemko, na kijamii, ikituwezesha tukabiliane na mazingira yetu na kupata shangwe na uradhi wa kiasi kutokana na utendaji wetu wa kila siku. Twaweza kufanya nini ili tuipate?

[Blabu katika ukurasa wa 6]

Urithi na mazingira vyahusika, lakini labda njia ya maisha yetu ndilo jambo moja la maana zaidi linaloongoza afya yetu

[Picha katika ukurasa wa 5]

Kuonekana mwenye afya njema huenda kukadanganya

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki