Vijana Wauliza . . .
Ni Lini Wazazi Wangu Wataniruhusu Nijipake Virembeshi?
Amkeni!: “Msichana anapaswa awe na umri gani kabla hajaruhusiwa kujipaka virembeshi?
Juliea: Ningesema miaka 13.
Amkeni!: Kwa nini?
Julie: Sijui.
Amkeni!: Miaka 12 ni uchanga zaidi?
Julie: Ndiyo.
Amkeni!: Lakini 13 ni umri wa kutosha?
Julie: Ndiyo.
Sallie: Mimi nafikiri kwamba ikiwa msichana ajua kujipaka vizuri na asionekane ni kama yuko katika bendi ya muziki wa roki au mahali pa namna hiyo, anapaswa kuruhusiwa kujipaka virembeshi.
John: Mimi nafikiri wanapaswa kujipaka ikiwa tu hawaonekani vizuri bila kujipaka.
Gloria: Ndiyo, virembeshi huongezea uzuri wa sura yako ya asili.
Larry: Lakini kwa nini mtu yeyote atake ‘kuongezea uzuri wa sura yake’ akiwa na miaka 13? Ninamaanisha, si lazima wafanye hivyo bado! Nafikiri wasichana wanapaswa kuwa na umri wa miaka 18 kabla hawajaanza kujipaka virembeshi.
KATIKA United States, matineja hutumia zaidi ya dola elfu tano milioni kwa mwaka kununua visaidia-urembo na vipamba-mwili. Kwa kueleweka, basi, huenda wewe ukahisi kwamba una haki kupaka rangi za midomo, rangi nyekundu ya mashavuni, au wanja wa macho ikiwa unataka hivyo. Hata hivyo, wazazi wako huenda wakaona mambo katika njia tofauti kabisa.
“Nilimwuliza mama yangu kama ningeweza kuvitumia nilipokuwa na miaka 13,” akumbuka Nina wa miaka 17. “Alisema, ‘Nina, wewe huvihitaji sasa.’” Shelly aliye mchanga alipata mwitikio-tendo kama huo kutoka kwa wazazi wake. “Niliomba ruhusa nilipokuwa na karibu miaka 13, nao wakaniambia kwamba singevitumia mpaka niwe na umri wa miaka 15. Nikasema, ‘Kwa nini sivyo?’”
Virembeshi—Kwa Nini Ni vya Maana kwa Wasichana
Kama vile mazungumzo yale ya mwanzoni yanavyotoa kielezi, kuna maoni mengi yanayotofautiana juu ya jambo hilo hata kati ya matineja. Haishangazi, basi, kwamba wewe na wazazi wako huenda mkapata tatizo la kupatana! Na bado, kukatazwa kabisa na wazazi wako huenda kukaonekana kuwa ukali usio na sababu. “Unatazama wasichana shuleni,” akumbuka mwanamke mchanga aitwaye Monica, “na wao wote wanaitumia.” Huenda pia ukashangaa jinsi inaweza kuwa SAWA kwa mama yako, lakini si SAWA kwako wewe! Isitoshe, wewe unaongezeka umri, na sura yako inazidi kuwa jambo la maana sana kwako kuliko hapo mbeleni.
Ubalehe umeanzisha mbadiliko fulani katika kimo chako, uzito, na umbo. Kama vile kitabu The Secret of a Good Life With Your Teenager kisemavyo, “mabadiliko haya yanaacha [vijana] wakihangaika juu ya uvutio wao kuliko wakati mwingine wowote . . . Wao pia wahangaikia kufanya ujinsia wao utambuliwe. Wanataka waonekane wakiwa kama mtu wa kike au wa kiume.” Au kama vile mwandikaji mmoja alivyoweka jambo hilo, unataka “kuanza kufanyiza mtindo ambao utakuwa wako . . . [ambao] unakudhihirisha wewe kama ambavyo wapenda zaidi na wajisikia wastareheka zaidi.”—Changing Bodies, Changing Lives, na Ruth Bell.
Kwa wasichana wengi, virembeshi ni njia moja ya kuimarisha mtindo huo wa kibinafsi na kuhisi kuwa mwanamke au mwenye kuvutia. “Nijipakapo virembeshi, mimi huhisi nikiwa mwenye uhakika zaidi, “akaeleza msichana mmoja tineja. Nina, aliyenukuliwa mwanzoni, aongezea: “Kuna wasichana wengi warembo, na kutumia virembeshi hunifanya nihisi vizuri zaidi juu yangu mwenyewe.”
Kutumia virembeshi pia ni kama tendo la kuingia kwenye utu mzima. Kama vile tineja mmoja alivyoliweka jambo hilo: “Hutaki ufikiriwe kama mtoto tena.” Wengine hutumaini kwamba wakionekana wakubwa zaidi itawapa heshima—au hata wavutie wavulana wakubwa zaidi. Kwa wengine, kujipaka virembeshi ni njia moja ya kufaana na marika tu. Asema Diane: “Kwa kadiri uonekanavyo una umri mkubwa zaidi, ndivyo vijana wale wengine hukufikiria wewe kuwa bora zaidi.”
Lakini vijana wengi wanataka kutumia virembeshi kwa sababu halisi kabisa: kulainisha ngozi isiyolainika, kufunika rangi ya uso yenye visehemu visivyopatana, kufunika rangi mbaya ya ngozi au kovu, kukazia sehemu za kuvutia, au kufunika sehemu za uso zisizovutia sana. Hata iwapo hivyo, ombi la ruhusa ya kutumia virembeshi huenda likawasha ubishano katika familia. Kwa nini wazazi mara nyingi hutenda katika njia hiyo hasi?
Kwa Nini Huenda Wakasema Sivyo
Ni kweli kwamba wakati mwingine wazazi wanatatizika kushughulikia uhakika wa kwamba watoto wao wanakua. Hivyo huenda wengine wakaelekea kuweka vizuizi vinavyozidi kidogo. Hata hivyo, wazazi wengi wanataka yaliyo bora zaidi tu kwa watoto wao. Ndiyo sababu Biblia husihi: “Wanangu, yasikilizeni mausia ya baba yenu, tegeni masikio mpate kujua ufahamu.” (Mithali 14:1) Wazazi wako huenda wasiwe wastadi katika kuweka hisi zao katika maneno. (“Wazazi wangu hawakutaka kuniacha nijipake maskara,” akumbuka msichana tineja mmoja, “lakini hawakunipa sababu.”) Yaelekea wana sababu nzuri za kuhisi wasiwasi juu ya jambo hilo.
Huenda wewe ukaelekea kuona kujipaka virembeshi kama jambo fulani la haki yako, jambo ambalo unapasishwa moja kwa moja unapofika “umri wa maajabu,” kama 13. Lakini kama vile mwandishi wa safu Elizabeth Winship aonyesha: “Hakuna sheria yoyote kuhusu umri hususa ambao utumizi wa virembeshi unakubalika. Inategemea mazoea ya familia na jumuiya.” Huenda wazazi wako wakahisi kwamba kutumia virembeshi katika umri wako kunaweza kuonekana vibaya kwa jumuiya au Wakristo wenzi. Wazazi wako watakuwa hasa wanahangaishwa kupatana na kufikiri huku ikiwa wao ni Mashahidi wa Yehova, kwa kuwa hawatapenda mapambo yako yapunguze sifa za huduma yako ya Kikristo.—2 Wakorintho 6:3.
Huenda pia wazazi wako wakahisi kwamba kujipaka virembeshi hakungekuwa kwa lazima na hakungefaa katika wakati huu wa maisha yako. Na hata hivyo, ujana una uzuri wao wenyewe, fahari ambayo hupita upesi sana. (Zaburi 90:10; Mithali 20:29) Huenda wakasababu, ‘Kwa nini afanye jambo ambalo litaficha au libadilishe sura yake ya uchanga?”
Wazazi wako huenda wakawa pia wanajua kutokana na mambo waliyoona wao binafsi jinsi “tamaa za ujanani” zilivyo za kudanganya. (2 Timotheo 2:22) Huenda hata wakaogopa kwamba utarudia baadhi ya makosa ambayo walifanya walipokuwa wachanga, na wanataka wakulinde. Msichana mmoja tineja hukumbuka hivi: “Mama alianza kujipaka virembeshi akiwa mchanga sana. Yeye akawa akifanya mambo ya kupita kiasi na kuvalia marinda mafupi sana na virembeshi vya aina nyingi. Hakutaka mimi niwe hivyo.”
Si kwamba utakuwa mwanamke asiye na tabia kwa kuweka rangi kidogo tu mdomoni. Hata hivyo, huenda wao wakaogopa kwa haki kwamba kutumia virembeshi kunaweza kukufunua kwa mikazo ambayo hauko tayari kuikabili. Baba ya wasichana wawili matineja ananukuliwa na mwandishi Ruth Bell akisema: “Inasisimua kuona watoto wakibadilika kuwa watu wazima. . . . Lakini wakati ninapowatazama na kuona wasichana wangu wadogo, wakati ninapojisemeza, ‘Hao ni watoto wangu na wanakuwa watu wakubwa na itawabidi kukabiliana na ulimwengu wa nje bila ya mimi kuwepo niwalinde,’ ndipo mimi huanza wasiwasi wa hisia-moyo. . . . Ulimwengu huu umechafuka na wanaweza kuumia.”
Ni jambo moja kuonekana mtu mzima. Lakini kutenda kama mtu mzima na kukabiliana na mikazo ya utu mzima kunaweza kuwa jambo jingine kabisa. Je, kweli uko tayari kukabiliana na uvutio ambao utapata kutoka kwa wavulana matineja—au hata wanaume wa umri mkubwa zaidi—ambao huenda wakavutiwa ikiwa virembeshi vinakufanya uonekane mkubwa kuliko vile ulivyo hasa?—Linganisha Mwanzo 34:1, 2.
Kuitumia Hali Vizuri Kabisa
Mambo yote yakiisha fikiriwa, bado huenda ukahisi kwamba uko tayari kujipaka virembeshi, na labda ni hivyo. Unapaswa ufanye nini? Msichana mmoja tineja aliungama hivi: “Mimi nilianza tu kujipaka. Nilipaka wanja kidogo machoni, na Mama yangu akaona ilionekana vizuri.” Kutumia virembeshi bila ruhusa, hata hivyo, ni hatari! Mithali 13:10 huonya: “Kiburi huleta mashindano tu.” Kama vile msichana mmoja alivyofikiri: “Nilijua wazazi wangu wangeghadhibika ikiwa ningejitokeza kwa ghafula nikiwa nimetumia virembeshi.” Kwa hiyo, wewe unaweza kufanya nini? Mstari huo wa Biblia unaendelea: “Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.”
Ndiyo, chagua “wakati wa kufaa” uzungumze mambo na wazazi wako. (Mithali 25:11) Kwa utulivu eleza hisi zako katika jambo hilo. Eleza kwa nini hilo ni la maana kwako, na kwa ufupi ueleze jambo lililo akilini mwako hasa. Wahakikishie kwamba hutaki kuonekana mtu wa mitindo wala kupita kiasi katika sura yako na kwamba unathamini maoni na uamuzi wao. Labda watabadili akili zao au wakubaliane nawe kwa kiwango nusu.
Kwa upande mwingine, huenda wakakata shauri kwamba wewe hauko tayari kutumia virembeshi. Lakini huu sio mwisho wa ulimwengu. Fanya yote uwezayo kufanya sura yako iwe bora chini ya hali hizo. Kwa mfano, utunzaji mwema wa ngozi unaweza kupunguza matatizo ya rangi ya ngozi. “Ikiwa ngozi yako siyo laini,” ashauri Jane Parks-McKay mshauri wa urembo, “ondoa fikira za watu kwenye hiyo kwa . . . kuvalia nguo inayokufanya uonekane maridadi sana—kitu chochote cha kuondoa fikira kwenye sehemu iliyo hasi.” Kusimama vizuri, kucha zilizotunzwa vizuri, nywele safi yenye kung’aa—mambo haya yote yanaweza kukufanya uonekane vizuri kabisa kwa kujipaka au kutojipaka virembeshi!
Ingawa hivyo, namna gani ikiwa wazazi wako wanakupa kibali cha kujipaka virembeshi? Makala ya wakati ujao itazungumzia utumizi unaofaa wa virembeshi.
[Maelezo ya Chini]
a Baadhi ya majina yamebadilishwa.
[Picha katika ukurasa wa 21]
“Msichana yule amejipaka virembeshi. Mimi nitaweza lini?”