Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 8/8 kur. 22-25
  • Sehemu ya 6: Shati Nyeusi na Misalaba ya Swastika

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Sehemu ya 6: Shati Nyeusi na Misalaba ya Swastika
  • Amkeni!—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kuabudu Serikali
  • Ufashisti Watukuza Vita
  • Ufashisti, Muundo wa Kijerumani
  • Kilichofanya Iwezekane
  • Je, Wamejifunza Somo?
  • Mashahidi wa Yehova—Wajasiri Licha ya Hatari ya Wanazi
    Amkeni!—1998
  • Bado Mataifa Hayajajifunza Somo
    Amkeni!—2002
  • Wafalme Washindani Waingia Katika Karne ya 20
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
  • Maovu ya Unazi Yafunuliwa
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 8/8 kur. 22-25

Utawala wa Kibinadamu Umepimwa Katika Mizani

Sehemu ya 6: Shati Nyeusi na Misalaba ya Swastika

NENO “Ufashisti” kwa kawaida hutokeza picha za vikundi vya majeshi ya Kiitalia vilivyovalia shati nyeusi na za askari wapanda farasi wa Kijerumani waliovalia yunifomu za hudhurungi zilizo na misalaba ya swastika. Lakini nchi nyingine zimejionea mambo pia kutokana na Ufashisti.

Wakati wa miaka ya 1930, Ufashisti ulipata umashuhuri katika Hangari, Romania, na Japani. Wakati wa Vita ya Kindani ya Hispania, utegemezo wa Kifashisti ulimsaidia Francisco Franco apate uongozi wa Hispania, ingawa wanahistoria wengi hawaoni utawala wa kidikteta wa Franco (1939-75) kama ulikuwa wa Ufashisti halisi katika muundo. Ule utawala wa kimabavu wa Argentina ulioanzishwa na Juan D. Perón (1943-55), kwa upande mwingine, ulikuwa wa Kifashisti.

Kuabudu Serikali

“Ufashisti” linatokana na neno la Kiitalia fascio na larejeza kwenye mfano wa kale wa Kiroma wa mamlaka. Likiitwa fasces katika Kilatini, lilikuwa ni furushi la fito ambazo kutoka kwazo kengee la shoka lilichomoza, mfano ufaao wa umoja wa watu chini ya mamlaka ya juu kabisa ya serikali.

Ingawa baadhi ya mizizi ya Ufashisti hurudi nyuma kwenye wakati wa Niccolò Machiavelli, si mpaka 1919, au miaka 450 baada ya kuzaliwa kwake, ndipo Benito Mussolini alipotumia neno hilo kwa mara ya kwanza. Ufasiki wa kisiasa wa siku zake, Machiavelli alidai, ungeweza kushindwa na mtawala mwenye uwezo mkubwa, mmoja ambaye angetendesha uwezo bila huruma lakini kwa akili.

Serikali ya Kifashisti inahitaji kiongozi kama huyo mwenye nguvu, mwenye kufikiria faida yake mwenyewe bila kufikiri juu ya kama anaipata kwa njia ya haki, na mwenye uwezo wa kuhimiza ujitoaji na uchangamfu ndipo uweze kufaulu. Kwa kufaa, wote wawili Mussolini na Hitler walijulikana tu kuwa “mtawala”—Il Duce and der Fuhrer.

Ufashisti unainua serikali juu ya mamlaka nyingine yote, ya kidini na pia ya watu wenyewe. Mwanasheria Mfaransa Jean Bodin wa karne ya 16, mwanafalsafa Mwingereza Thomas Hobbes wa ya 17, na pia wanafalsafa Wajerumani wa karne ya 18 na 19 Johann Gottlieb Fichte, Georg Wilhelm Friedrich Hegel, na Heinrich von Treitschke, wote walitukuza taifa. Hegel alifundisha kwamba taifa lina mahali pa uwezo mkubwa na kwamba jukumu la kwanza la mtu mmoja mmoja ni kuwa mtegemezi mwaminifu wayo.

Kwa muundo wazo, serikali zote lazima ziwe zenye mamlaka. Lakini serikali za Kifashisti zimeundwa ili kutumia mamlaka haya hadi upeo, yakitaka utii wa kiupofu. Ukiwaona wanadamu kama zaidi kidogo tu ya watumwa wa serikali, Treitschke alisema: “Si kitu unafikiri nini, bora unatii.” Kwa ufanani, Ufashisti ulichukua mahali pa mbiu ya, “Uhuru, usawa, udugu,” iliyosikiwa wakati wa Mapinduzi ya Kifaransa, ukiwa na wito wa Kiitalia, “Kuamini, kutii, kupigana.”

Ufashisti Watukuza Vita

Kupigana? Ndiyo! “Ni vita pekee inayoleta mkazo mwingi mno juu ya utendaji wote wa kibinadamu na inaweka alama ya cheo juu ya watu walio na ujasiri wa kukabiliana nayo,” Mussolini akasema wakati mmoja, akiongeza hivi: “Vita kwa mwanamume ni kama vile umama kwa mwanamke.” Aliita amani ya kuendelea “kuwa yashusha moyo na kuzuia mema yote ya mwanadamu yaliyo ya msingi.” Katika kusema maneno haya, Mussolini alikuwa anatokeza tu maoni ya Treitschke, aliyebisha kwamba vita ni ya lazima na kwamba kuiondoa ulimwenguni “kungetia ndani kufifia kwa vingi vya vichocheo muhimu na vilivyo bora vya nafsi ya kibinadamu.”

Kando ya habari hii ya vita na utawala wa kidikteta huenda tusishangazwe kujua kwamba wanahistoria wengi hufuatisha mwanzo wa Ufashisti wa kisasa nyuma kwenye Napoléon I wa Ufaransa. Akiwa dikteta wakati wa miaka ya mapema ya 1800, kwa ukubali yeye mwenyewe hakuwa Mfashisti. Hata hivyo, mingi ya miongozo yake, kama vile kuwekwa kwa mfumo wa polisi wa siri na utumizi wa ufundi wa propaganda na ukaguzi ili kudhibiti waandishi wa habari, ilitumiwa baadaye na Wafashisti. Na kwa kweli jitihada yake kurudisha utukufu wa Ufaransa ni kifananishi cha tamaa nyingi mno ya ukuu wa kitaifa ambayo viongozi wa Ufashisti wamekuja kujulikana kwayo.

Kufikia 1922 Wafashisti katika Italia walikuwa na nguvu za kutosha kumweka Mussolini kuwa waziri mkuu, cheo alichotumia upesi kama jiwe la kukanyagia na kuwa dikteta. Kwa mambo yanayohusu mishahara, masaa, na miradi ya kutokeza bidhaa nyingi, kazi ya mtu binafsi iliwekwa chini ya uwezo imara wa serikali. Kwa hakika, biashara ya kibinafsi iliruhusiwa ikiwa tu ilitumikia faida za serikali. Vyama vya kisiasa isipokuwa cha Kifashisti viliharamishwa; vyama vya mwungano wa wafanya kazi vilipigwa marufuku. Serikali kwa ufundi iliongoza njia zote za uwasilishi-habari, ikinyamazisha wapinzani kwa njia ya ukaguzi. Uangalifu wa pekee ulitolewa wa kuwafunza wachanga, na uhuru wa kibinafsi ulipunguzwa sana.

Ufashisti, Muundo wa Kijerumani

“Ijapokuwa upatani wa njia zao kuelekea uwezo,” chasema kitabu Fascism, cha A. Cassels, “Ufashisti wa Kiitalia na Unazi wa Kijerumani zilikuwa tofauti katika tabia na katika mwono wao wa wakati ujao.”

Zaidi ya wanafalsafa Wajerumani waliotangulia kutajwa ambao walitumika kama watangulizi wa fikira za Ufashisti, wengine, kama mwanafalsafa wa Kijerumani wa karne ya 19 Friedrich Nietzsche, walisaidia kuunda namna ya Ufashisti wa Kijerumani wa aina ya pekee. Si kwamba Nietzsche alikuwa Mfashisti, lakini alitaka utawala wa walio bora kabisa, jamii ya watu wasio wa kawaida. Katika kufanya hivyo, hata hivyo, hakuwa akifikiria jamii au taifa moja, walio wa chini zaidi wakiwa Wajerumani, ambao hakuwapenda sana. Lakini baadhi ya mawazo yake yalikaribiana na kile ambacho wenye mawazo ya Usoshalisti wa Kitaifa walikiona kuwa cha Kijerumani kabisa. Kwa hiyo mawazo haya yalitwaliwa, hali mengine yasiyokubaliana na fundisho la Nazi, yalitupwa.

Hitler pia aliathiriwa sana na mtungaji wa Kijerumani Richard Wagner. Akiwa na utaifa na uzalendo wa kupita kiasi, Wagner aliona Ujerumani kama imekusudiwa kufanya jambo kubwa duniani. “Kwa Hitler na wenye mawazo ya Nazi, Wagner alikuwa mashuhuri kikamili,” chasema Encyclopedia of the Third Reich. Chaeleza: “Mtungaji alitoa muhtasari wa ukuu wa Ujerumani. Katika maoni ya Hitler wimbo wa Wagner ulithibitisha utaifa wa Ujerumani.”

Mwandikaji William L. Shirer aongezea: “Hata hivyo, hayakuwa maandishi ya (Wagner) ya siasa, bali michezo yake iliyo ya juu sana ya kuigiza hadithi, ikikumbusha kwa uwazi sana ulimwengu wa Ujerumani wa kale pamoja na miigizo ya ushujaa, miungu ya kipagani yenye kupigana, mashetani yake na majoka, uhasama wenye kumwaga damu wa kikabila na sheria za kikabila za kale, maoni yake ya ajali na uzuri wa upendo na uhai na staha ya kifo, zilizoongoza hadithi za Ujerumani ya ki-siku-hizi na kuifanya iwe na Weltanschauung [mwono wa ulimwengu] wa Kijerumani ambao Hitla na Wanazi, wakiwa na ujiteteo fulani, waliichukua kuwa yao wenyewe.”

Kufikiri kwa wote wawili Nietzsche na Wagner kulifanyizwa na Comte Joseph Arthur de Gobineau, mjumbe wa Kifaransa na mwenye elimu ya tabia ya mataifa, ambaye, kati ya 1853 na 1855, aliandika Essai sur l’iné galité des races humaines (Insha Juu ya Kukosa Usawa kwa Jamii za Rangi za Kibinadamu). Alitoa hoja kwamba mchanganyiko wa aina mbalimbali za kijamii huyakinisha ajali za ustaarabu. Kupunguza ubaguzi wa rangi wa Kiarya kungeongoza mwishowe kwenye anguko, yeye akaonya.

Kufuata ujamii wa rangi mbalimbali na kupinga jamii za asili ya Shemu ambako kulitokana na maoni haya kulikuwa namna kama ya Ufashisti wa Kijerumani. Miongozo yote hiyo ilikuwa na umaana mdogo katika Italia. Kwa hakika, ithibati za kuwako upingaji wa jamii za asili ya Shemu katika Italia zilionwa na wengi wa Waitalia kuwa kionyeshi cha kwamba Hitler alikuwa akichukua mahali pa Mussolini kama nguvu pekee ya Ufashisti. Kwa kweli, kadiri wakati ulivyopita, uvutano wa Hitler juu ya maongozi ya Ufashisti wa Kiitalia uliongezeka.

Katika jitihada za kupata ukuu wa kitaifa, Ufashisti wa Kiitalia na Ufashisti wa Kijerumani ulitazama katika pande tofauti. Mwandikaji A. Cassels anaeleza kwamba “mahali Mussolini angesihi wananchi wake waige matendo ya Waroma wa kale, mapinduzi ya Nazi yaliyokuwa na roho iliyoelekezwa kuchochea Wajerumani, si kufanya tu yale ambayo Wadachi mapandikizi wa kale walifanya, bali pia kuwa hao hao mabingwa wa kabila waliozaliwa katika mwili mwingine katika karne ya ishirini.” Yaani, Ufashisti wa Kiitalia ulitafuta kuupata tena ule ambao waweza kusemwa ni utukufu wa zama zilizopita, kwa kukokota Italia, nchi isiyoendelea kiuchumi, iingie karne ya 20. Ujerumani, kwa upande mwingine, ilitafuta kupata utukufu wa kwanza kwa kurudia mambo ya kale yaliyo ya kihekaya.

Kilichofanya Iwezekane

Katika nchi nyingi, Wafashisti wamepata mamlaka baada ya msiba wa kitaifa, kudhoofika kwa uchumi, au kushindwa kivita. Haya yalikuwa kweli katika Ujerumani na Italia pia. Ingawa wote walikuwa katika pande zenye kupingana katika Vita ya Ulimwengu ya 1, wote walitoka katika mzozano huo wakiwa wamedhoofika sana. Kutoridhika kwa kitaifa, vurugu ya kiuchumi, na kuzidishwa kwa ile vita ya kitabaka kulikumba nchi zote mbili. Inflesheni ya hali ya juu ilikumba Ujerumani, na ukosefu wa kazi ukaongezeka sana. Kanuni ya kidemokrasi pia ilidhoofika, bado ikizuiwa na mila za kijeshi na jadi ya Prussia ya kutumia mamlaka. Na kila mahali kulikuwa na tisho la Ubolshevi wa Kisovieti wenye kuhofiwa sana.

Wazo la Charles Darwin la mageuzi na uchaguano wa kiasili wa aina-aina za vitu vilivyo hai kwa kuondoa vilivyo vinyonge, ulikuwa jambo jingine la maana katika kuinuka kwa Ufashisti. Kitabu The Columbia History of the World chazungumza juu ya “kuamshwa tena kwa Udarwini wa Kijamii katika mawazo ya Wafashisti, yaliyoelezwa na wote wawili Mussolini na Hitler.”

Kitabu Encyclopedia of the Third Reich kinakubaliana na kadirio hili, kikieleza kwamba Udarwini wa Kijamii ulikuwa “wazo kuu katika maongozi ya Hitler ya kuua jamii fulani ya watu kwa mauaji makubwa.” Kwa kupatana na mafundisho ya mageuzi kama yalivyoelezwa na Darwin, “wenye mawazo ya Kijerumani walitoa hoja kwamba serikali ya sasa, badala ya kutumia nishati zayo kuwalinda walio wanyonge, inapaswa kuwakataa wakazi wayo wa cheo cha chini kwa kupendelea lile lenye nguvu, na afya.” Walitoa hoja kwamba vita ni vya kawaida katika juhudi za kuhifadhi wastahilio kubaki kwa kuwapoteza wasiofaa sana, kwamba “ushindi huwaendea walio na nguvu, na walio wanyonge lazima waondolewe.”

Je, Wamejifunza Somo?

Zimekwisha zile siku za vikundi vya Waitalia wenye shati nyeusi na za wapanda farasi Wajerumani wenye kwenda kwa fujo nyingi wakiwa na yunifomu za hudhurungi zenye msalaba wa swastika. Na bado, hata katika 1990, kuna masalio ya Ufashisti. Miaka miwili iliyopita gazeti Newsweek lilionya kwamba katika karibu kila taifa la Magharibi mwa Ulaya, “ule uvutano wenye nguvu wa upande wa kulia kabisa unathibitisha tena kwamba ubaguzi wa rangi usiofichika kabisa na kutumia viwango vya utaifa na kutumia uwezo kimamlaka bado unaweza kupata utegemezo wa kushangaza.” Hakuna shaka kwamba moja ya harakati hizo zenye nguvu sana ni Kikosi-cha-Mbele cha Le Pen cha Jean Marie katika Ufaransa kikiwa na ujumbe ambao kwa msingi ni “kama ule ule wa Usoshalisti wa Kitaifa.”

Je, ni jambo la akili kuweka tumaini katika harakati za Ufashisti mamboleo? Je, mizizi ya Ufashisti—mageuzi ya Darwini, ubaguzi wa rangi, uwezo wa kivita, na utaifa—inafanyiza msingi thabiti ambao juu yao serikali nzuri inaweza kuanzishwa? Au wewe hungekubali kwamba kama vile aina nyingine zote za utawala wa kibinadamu, Ufashisti umepimwa katika mizani na kupatikana umepungukiwa?

[Sanduku katika ukurasa wa 24]

Ufashisti—Je, Msingi Wao Ni Thabiti?

Mageuzi ya Darwini: “Idadi inayozidi kuongezeka ya wanasayansi, na hasa zaidi idadi inayoongezeka ya wanamageuzi . . . hutoa hoja kwamba nadharia ya Darwini ya mageuzi si nadharia ya kweli kamwe kisayansi.”—New Scientist, Juni 25, 1981, Michael Ruse.

Ubaguzi wa Rangi: “Lile bonde kubwa la utofautiano wa jamii za rangi na vikundi mbalimbali vya watu, katika mahali lilipo, ni la kisaikolojia na kishosholojia; si la kurithi kwa wazazi!”—Genes and the Man, Profesa Bentley Glass.

“Wanadamu wa rangi zote . . . wametokana na mwanadamu yule yule wa kwanza.”—Heredity and Humans, mwandikaji wa sayansi, Amram Scheinfeld.

Uwezo wa Kijeshi: “Ule ujuzi, kazi ngumu, na hazina inayomwagwa juu ya hiki . . . kichaa kwa kweli unaduwaza akili. Kama mataifa hawangejifunza vita tena kamwe, hakungekuwa na jambo ambalo ainabinadamu isingeweza kufanya.”—Mtungaji Mwamerika na mshindi wa zawadi ya Pulitzer, Herman Wouk.

Utaifa: “Utaifa hugawanya wanadamu katika visehemu visivyovumiliana. Kama tokeo, watu hujifikiria kuwa Waamerika, Warusi, Wachina, Wamisri au Waperu kwanza, na kujifikiria kuwa wanadamu huwa jambo la pili—ikiwa kwa vyovyote wao hupata kujifikiria hivyo.”—Conflict and Cooperation Among Nations, Ivo Duchachek.

“Mengi sana ya matatizo tunayoona leo ni kwa sababu ya, au ni tokeo la, mielekeo bandia—mingine yayo imechukuliwa bila kujua. Kati ya hiyo ni lile wazo la utaifa usio wa akili pana—‘iwe haki isiwe haki, ni nchi yangu.’”—Aliyekuwa Katibu-Mkuu wa UM, U Thant.

[Picha katika ukurasa wa 23]

Vifananishi vya kale vya kidini, kama vile msalaba wa swastika, na ule usemi, “Mungu Pamoja Nasi,” haukuokoa utawala wa Hitler

Ile “fasces,” kifananishi cha Mussolini cha Ufashisti, inapatikana juu ya sarafu fulani za United States

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki