Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g90 9/8 kur. 22-23
  • Je! Wakristo Wapaswa Kutumia Tasbihi (Rozari)?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Wakristo Wapaswa Kutumia Tasbihi (Rozari)?
  • Amkeni!—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mariamu na Tasbihi
  • Sala na Tasbihi
  • Jinsi ya Kumfikia Mungu
  • Je, Usali kwa Bikira Maria?
    Amkeni!—2005
  • “Tufundishe Sisi Kusali”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • “Tazama! Kijakazi wa Yehova!”
    Igeni Imani Yao
  • “Tazama! Kijakazi wa Yehova!”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1990
g90 9/8 kur. 22-23

Maoni ya Biblia

Je! Wakristo Wapaswa Kutumia Tasbihi (Rozari)?

“MARIAMU na Tasbihi ndizo njia bora kabisa za kumfikia Mungu Mweza Yote katika sala.”—Jean.

“Kama wewe ungehitaji msaada kutoka kwa Mariamu, huo ungeweza kupatikana kwa matokeo mazuri kabisa kupitia utumizi wa Tasbihi. Mimi singeenda popote kamwe bila huo!”—Kevin.

“Sisi tulifundishwa kwamba ni lazima usali kwa Mungu kupitia Mariamu.”—Jeannine, ambaye hapo kwanza alikuwa mtawa-mke wa Kikatoliki.

Je! kuna msingi halisi kwa hilo tegemeo hakika juu ya Tasbihi? Je! Mungu, Kristo, au Mariamu walipendekeza utumizi wayo? Historia na Neno Takatifu la Mungu husema nini juu yayo?

Watu walio wengi ambao hutumia Tasbihi huamini kwamba asili ya zoea hilo ilikuwa Ukristo. Hata hivyo, ushuhuda wa kihistoria hufunua kwamba zoea la kukariri sala kwa moyo na kuzihesabu katika uzi wa shanga lilitokea kabla ya kuanza kwa Ukristo. Kikieleza juu ya asili ya Tasbihi, The World Book Encyclopedia huripoti hivi: “Shanga za sala zina asili ya kale, na labda zilitumiwa kwanza na Wabuddha. Wote wawili Wabuddha na Waislamu huzitumia katika sala zao.” The Catholic Encyclopedia hukiri kwamba shanga za sala zilizoelewa kila mahali na watu wasio Wakristo kwa karne nyingi na zikatumiwa muda mrefu kabla Kanisa Katoliki halijachagua kutumia Tasbihi.

Mariamu na Tasbihi

Mariamu huitwa “Malkia wa Tasbihi Takatifu.” Yeye ndiye hutambuliwa kuwa aliwashauri Wakatoliki ya kwamba “Salini kwa Tasbihi.” Tasbihi iliyo ya kawaida kabisa, “Ile Tasbihi ya Mbarikiwa Bikira Mariamu,” hufuatishwa nyuma kuwa ilianza kwenye karne ya 12 W.K. na ikafikia namna yayo kamili katika karne ya 15. Tasbihi na Mariamu huambatana pamoja, kwa maana Mariamu aonwa kuwa ndiye mwendelezaji wa Tasbihi na ndiye hupewa umaana mkubwa kabisa katika sala.

Kwa nini kuwe na mkazo wote huo juu ya Mariamu na Tasbihi? Kwa kujibu, wenye mamlaka Wakatoliki huelekeza kwenye yale ambayo malaika Gabrieli alimwambia Mariamu: “Shangilia, O binti mwenye upendeleo mwingi! Bwana yu pamoja nawe.” (Luka 1:28, The New American Bible) Mariamu alithamini kwamba sehemu yake katika kuchukuliwa mimba na kuzaliwa kwa Yesu, ingawa ilikuwa ya maana, ilikuwa na umaana mdogo ilinganishwapo na cheo kilichokwezwa ambacho kingepokewa na Mwana ambaye angemzaa. Kwa habari yake, malaika Gabrieli aliendelea kusema hivi: “Itakuwa kubwa fahari yake naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu Zaidi. Bwana Mungu atampa kiti cha ufalme cha Daudi baba yake. . . . Utawala wake utakuwa bila mwisho.”—Luka 1:32, 33, NAB.

Angalia kwamba uangalifu ulipasa kuelekezwa, si juu ya Mariamu, bali juu ya Mwana ambaye yeye angemchukua mimba—Yesu. Yeye ndiye angekuwa mkuu na kutawala akiwa Mfalme. (Wafilipi 2:9, 10) Hakuna jambo lasemwa juu ya kuweka Mariamu awe “Malkia wa Tasbihi Takatifu.” Hata hivyo, Mariamu alipokea baraka; akawa mama ya Yesu.—Luka 1:42.

Mariamu hakuwa mwanamke mtaka makuu, mwenye kutafuta umashuhuri. Alifurahi na kutosheka kuwa mwabudu mnyenyekevu wa Mungu Aliye Juu Zaidi. Nia yake ya usikivu na ujitiisho yafunuliwa na itikio lake kwa malaika Gabrieli wakati Mariamu aliposema hivi: “Mimi ndimi mjakazi [mtumishi] wa Bwana.” (Luka 1:38, The Jerusalem Bible) Muda wote wa maisha yake, Mariamu alithibitika kuwa mwanamke wa imani, mpenda uadilifu, mwanafunzi mshikamanifu na mwaminifu wa Yesu Kristo aliyejiunga na waabudu wenzake katika kusali kwa unyenyekevu kwa Mungu Mweza Yote. Wakristo wa mapema walisali pamoja na Mariamu, wala hawakusali kwake.—Matendo 1:13, 14.

Sala na Tasbihi

Wakristo huona sala kuwa uandalizi wenye kuthaminika sana wa Muumba—zawadi halisi ya kutunzwa sana. Sala ni usemi wenye staha kwa Mungu Mweza Yote. Yapasa kutoa hisia zetu za ndani kabisa na mawazo yenye kuhisiwa moyoni. “Sala yapasa kuwa wonyesho wa urafiki wa mtu pamoja na Mungu,” yasema New Catholic Encyclopedia. Kumtolea Mungu maombi rasmi hakupasi kamwe kuwe desturi isiyo na maana, wala haitupasi kufuatilia mno fungu fulani la maneno tupendeleayo sana yaliyokaririwa moyoni.—Mathayo 6:7, 8.

Je! Tasbihi huchangia sala zenye umaana jinsi hiyo? Jeannine aliona kwamba kukariri maneno ya “Salamu Mariamu” katika Tasbihi “kulikuja kuwa mrudio-rudio wenye kufanywa bila ufahamu.” Kurudia maneno yale yale katika Tasbihi hakukumleta karibu zaidi na Mungu. Lydia, mwanamke mwingine aliyekuwa mtawa Mkatoliki, alisema hivi: “Mimi sikupata jambo lolote lenye mafunzo katika kuikariri Tasbihi. Mimi ningalipendelea kusoma vitabu juu ya dini.” Sala za kurudia-rudia hazina kusudi lenye mafaa, kwa kuwa Mungu ameahidi hivi: “Kabla hawajaita, mimi nitajibu.” (Isaya 65:24, NAB; Mathayo 6:7, 8, 32) Mungu Mweza Yote huthamini na kujibu maombi rasmi ambayo husemwa kwa kusudio lifaalo na ambayo hutoka katika moyo mweupe wenye kufuata haki. Tasbihi haisaidii mtu kumfikia Mungu kwa sala zenye umaana, zenye kuhisiwa moyoni.—Zaburi 119:145; Waebrania 10:22.

Jinsi ya Kumfikia Mungu

Njia pekee ya kuweza kumfikia “Msikiaji wa sala” ni kupitia Yesu Kristo. (Zaburi 65:2, NW) Yesu alifundisha wazi hivi: “Mimi ndimi Njia, Ukweli na Uhai. Hakuna mtu awezaye kuja kwa Baba isipokuwa kupitia mimi.” (Yohana 14:6, JB) Mariamu hakualikwa ashiriki daraka hili na kutumikia akiwa mpatanishi. Kama Mariamu angalikuwa amepewa pendeleo hilo lisilo na kifani, hakika Yehova angalijulisha jambo hilo.—Waebrania 4:14-16; 1 Yohana 2:1, 2.

Tasbihi na ukariri wa sala zenye kukumbukwa kwa moyo vilianza nje ya mabara yenye kudai kuwa ya Kikristo. Kusali kwa Mariamu hupuuza yale ambayo Yesu alifundisha, kwamba “hakuna mtu awezaye kuja kwa Baba isipokuwa kupitia [yeye].” Hivyo, Tasbihi na Mariamu siyo njia ya Mungu ya kumfikia Yeye katika sala.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki