Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 1/8 kur. 26-27
  • “Mwendee Chungu”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Mwendee Chungu”
  • Amkeni!—1991
  • Habari Zinazolingana
  • Chungu wa Jangwani Wanaotokeza Asali Tamu
    Amkeni!—2011
  • “Mwendee Chungu”
    Amkeni!—1995
  • Jeshi Lasonga Mbele!
    Amkeni!—2003
  • Watunza-Nyumba Wadogo Walio Hodari Sana
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 1/8 kur. 26-27

“Mwendee Chungu”

“EWE mvivu, mwendee chungu,” akaandika Mfalme Sulemani, “zitafakari njia zake ukapate hekima.” Mtu mvivu—au hata mtu yeyote—aweza kujifunza nini kutokana na chungu? Sulemani aliendelea kusema: “[Ingawa, NW] yeye hana akida, wala msimamizi, wala mkuu, lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.”—Mithali 6:6-8.

Ni wazi mfalme huyu mwenye hekima alikuwa akimrejezea chungu mvunaji. Katika Israeli, kama ilivyo katika mahali pengine pengi, ni jambo la kawaida kuona chungu mvunaji akienda huku na huku, akiwa amebeba mbegu ya ukubwa ukaribiao kuwa kama wake mwenyewe. (Ona kushoto juu.) Yeye hupeleka mkusanyo wa vyakula kwenye akiba ya chini ya ardhi.

Kwa kuwa iko chini ya ardhi, “ghala” hiyo yaweza kuwa na unyevu sana katika majira ya mvua, na mbegu zitachipuka au zishike kuvu zikiachiliwa. Hivyo basi chungu huwa na kazi ya ziada. Mara tu jua lichomozapo, chungu wa kazi hupeleka mbegu kwenye uso wa ardhi ili zikauke zikiwa nje mahali peupe. (Ona juu.) Na kabla jua halijakuchwa, ni lazima chungu wabebe mbegu zote kuzirudisha ndani. Chungu fulani hufanya akili sana kuiuma na kuitoa ncha yenye kukua ya zile mbegu mara tu zikusanywapo au zianzapo kuchipuka.

Kazi ya chungu haiishi kwa kutayarisha chakula. Pia wana kile kikazi cha kutunza wachanga. Ni lazima mayai yawekwe yakiwa vikundi-vikundi vyenye kushikamana. Mabuu walioanguliwa kutoka kwenye mayai ni lazima walishwe. Wenye kutambaa ni lazima wachungwe. Chungu fulani hata huandaa huduma ya kupepea hewa. Kukiwa na joto mchana, wao huwabeba wenye kutambaa na kuwaingiza kwa kina kirefu zaidi chini kiotani. Ubaridi wa jioni ukaribiapo, wao huwapandisha juu tena wenye kutambaa. Kazi nyingi, sivyo?

Jamii hiyo iongezekapo idadi, huwa ni lazima vyumba vipya vijengwe. Chungu wa kazi hutumia taya zao kuchimba na kubeba udongo nje. Kwa kawaida wao hufanya hivi baada ya mvua wakati udongo ni mwororo. Pia wao hufinyanga udongo uwe “matufali” kwa ajili ya miradi yao ya uhandisi-wa-ujenzi wao—kuzijenga kuta na dari za mahandaki na vyumba vyao vya chini ya ardhi.

Yote haya hufanywa na chungu bila “akida, wala msimamizi, wala mkuu.” Namna gani malkia? Yeye hatoi amri yoyote. Hutaga mayai tu naye ni malkia kwa maana ya kwamba yeye ndiye mama ya jamii hiyo. (Ona juu.) Hata wakiwa bila msimamizi wa kuwachunguza au mnyapara wa kuwasukuma, chungu hubaki kwenye kazi yao bila kuchoka. Chungu mmoja alionekana akifanya kazi kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa nne usiku!

Je! wewe waweza kujifunza somo kwa kumtazama chungu? Je! wewe hufanya kazi kwa bidii na kujitahidi kufanya maendeleo katika kazi yako, iwe au isiwe unasimamiwa kuifanya? (Mithali 22:29) Utathawabishwa hatimaye hata ikiwa mwajiri wako haoni ufanyavyo. Waweza kuona shangwe ya kuwa na dhamiri safi na mtosheko wa kibinafsi. Kama vile Sulemani alivyoonelea: “Usingizi wake kibarua ni mtamu, kwamba amekula kidogo, au kwamba amekula kingi.”—Mhubiri 5:12.

Si hayo tu tuwezayo kujifunza kutokana na chungu. Chungu hufanya kazi kwa bidii kutokana na silika. Kwa uhakika, chungu fulani huonwa wakifuata kwa upofu kijia kilichopitiwa na wengine. Wao hujikuta wakizunguka-zunguka mduara, mviringo-viringo, mpaka kuanguka na kufa.

Je! nyakati fulani wewe huwa wahisi kwamba unakimbia mduara, sikuzote ukiwa mwenye shughuli na uchovu bila kufikia mradi wowote kamwe? Ikiwa ndivyo, huu ndio wakati wa kuchunguza kusudi la kazi yako ya bidii na ukadirie miradi yako ina thamani gani ya kweli. Kumbuka shauri lenye hekima la Mfalme Sulemani: “Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.”—Mhubiri 12:13.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki