Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 4/8 kur. 22-23
  • Utafiti wa Kutumia Wanyama Maoni Yaliyosawazika

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Utafiti wa Kutumia Wanyama Maoni Yaliyosawazika
  • Amkeni!—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Maoni ya Kibiblia
  • Je, Ni Vibaya Kula Nyama?
    Amkeni!—1997
  • Kufanyia Wanyama Ukatili—Je, Ni Vibaya?
    Amkeni!—1998
  • Je, Mungu Anawajali Wanyama?
    Amkeni!—2011
  • Wanyama
    Amkeni!—2015
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 4/8 kur. 22-23

Utafiti wa Kutumia Wanyama Maoni Yaliyosawazika

INGAWA bei inayolipwa yaweza kubishaniwa, watu walio wengi huamini kwamba utafiti wa kutumia wanyama umetokeza wema mkubwa kwa ainabinadamu. Hata wale wanaotetea jeuri itumiwe kukomesha kujaribia wanyama, wamenufaika na maarifa mapya ya kitiba na taratibu za upasuaji na pia madawa ya kupigana na maradhi.

Martin Stephens wa Chama cha Ubinadamu cha United States alisema: “Ni lazima tufuatie haki na kutambua kwamba kumekuwako manufaa fulani kutokana na utafiti wa kutumia wanyama. Lakini mradi wetu wa mwisho ni kuacha kutumia wanyama kabisa.” (Parade Magazine, Oktoba 9, 1988) “Mimi nakubali,” akasema Vicki Miller, rais wa Chama cha Ubinadamu cha Toronto, “kwamba matumizi fulani mazuri ya wanyama yalifanywa karibu na mwanzo wa karne hii. Udhibiti wa ugonjwa wa sukari ulitokana kwa halali na utafiti wa kutumia wanyama. Lakini hakuna lazima ya hilo sasa kwa kuwa tuna namna zote za tekinolojia zinazoweza kutumiwa badala.”—The Sunday Star, Toronto, Canada.

Mchambuzi uyo huyo aliulizwa jinsi angejibu wale wanaotokeza hoja hii: Ikiwa panya afa ili uhai wa mtoto mchanga uokolewe, inastahili. Ikiwa wanyama hawatumiwi katika utafiti, watoto wachanga wafa ili kuokoa panya. Jibu lake kwenye Globe and Mail la Toronto lilikuwa hili: “Hilo ni suala lenye kugusa moyo, na kwa maoni hayo imekuwa karibu haiwezekani kushinda . . . Lile jambo la panya au mtoto mchanga na unashindwa kila mara.”

Swali hili liliulizwa: “Ikiwa utafiti juu ya mnyama ungeweza kukuokoa wewe au mpendwa kutokana na maradhi yenye maumivu makali au kifo, je! ungeukataa?” John Kaplan, profesa wa sheria kwenye Chuo Kikuu cha Stanford, California, aliandika jibu katika toleo la Novemba 1988 la gazeti Science: “Ni mara chache wale wanaopinga utafiti wa kutumia wanyama wameshikilia kanuni na kuagiza wanaowatibu wasitumie matokeo ya utafiti wa kitiba uliofanywa kwa kutumia wanyama iwapo utanufaisha wapendwa wao au wao wenyewe. Wala hawajawa na nia ya kujikatalia faida za maendeleo yoyote ya wakati ujao kutokana na utafiti wa kutumia wanyama. Twaweza kuvutiwa na kanuni zinazosukuma Mashahidi wa Yehova wakatae kutiwa damu mishipani . . . kwa wale wanaopinga kuwindwa kwa wanyama wenye manyoya kutovaa [mavazi] ya manyoya. Lakini ni lazima tupinge kwa nguvu wazo linaloongoza wale wanaopinga utafiti wa kutumia wanyama wafuatie lengo lao si kwa kielelezo bali kwa kupigana kupitia hoja za udanganyifu ili kunyima kila mtu manufaa hizo.”

“Lazima umma ujulishwe,” akaandika mhariri wa gazeti Science la Machi 10, 1989, “kwamba utafiti wa kutumia wanyama hunufaisha pia wanyama wengine. Kwa kweli, dawa ya chanjo ya sotoka, kiini kinachoua mamilioni ya ng’ombe polepole na kwa maumivu, ilisitawishwa kwa kujaribia wanyama; chanjo hiyo sasa hutumiwa na Shirika la Afya Ulimwenguni kwa mamilioni ya ng’ombe katika Afrika.”

Maoni ya Kibiblia

Kufuatia Furiko la tufe lote katika siku ya Noa, Yehova Mungu alitoa amri hii kwa Nuhu na kwa uzao wake, ambao ni kutia ndani kizazi chetu: “Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa na mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote. Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.” (Mwanzo 9:1, 3, 4) Ngozi za wanyama zingeweza pia kutumiwa kwa ajili ya mavazi. Hilo halingevunja utawala ambao Mungu alimpa binadamu juu ya jamii ya wanyama.—Mwanzo 3:21.

“Ikiwa wanyama waweza kutumiwa kuwa chakula cha kuendeleza uhai wa watu,” liliandika gazeti Amkeni! (Kiingereza) la Juni 22, 1980, “laonekana ni jambo la akili kuwatumia katika majaribio ya kitiba ili kuokoa uhai. Hata hivyo, hicho si cheti cha majaribio yasiyo na mipaka na mara nyingi yasiyo na thamani, ya kurudiwa-rudiwa yanayohusisha mteseko mkubwa.” Hakika, kulingana na maoni ya Kibiblia, ukatili usio na huruma kuelekea wanyama hauwezi kutetewa.—Kutoka 23:4, 5, 12; Kumbukumbu la Torati 25:4; Mithali 12:10.

Madaktari na wanasayansi wengi hukubali kwamba wema fulani umetokana na chama chenye kutaka mabadiliko makubwa cha wale wanaopinga utafiti wa kutumia wanyama. “Mawazo mengi sana yanayotolewa na chama cha masilahi ya wanyama ni yenye kupita kiasi lakini ni ya kweli,” akakubali mwanasayansi mmoja. “Bila shaka uhai na kuteseka kwa wanyama ni jambo la kuangaliwa,” akajulisha rasmi mwanasayansi Mwamerika Jeremy J. Stone. “Maarifa fulani yaweza kupatikana kwa bei kubwa sana,” akakubali mfisiolojia Mwingereza Dakt. D. H. Smith. “Sisi twaafikiana na tamaa ya kufanya utafiti uwe wa maumivu machache, kutunza vizuri na kupunguza hesabu ya wanyama katika majaribio,” akasema Dakt. J. B. Wyngaarden wa Taasisi za Kitaifa za Afya za U.S. Na mteteaji mmoja wa wanyama alikubali hivi: “Hapo kwanza karibu lilionwa ni jambo la kiume kutumia wanyama na kutofikiria lolote juu yalo. Leo, kufikiria juu ya uwezekano mwingine hufikiriwa ndilo jambo linalopasa kufanywa.”

“Uwezekano mwingine” ndilo jambo la maana. Wanasayansi hukubali kwamba huenda wasifikie kamwe hatua kamili ya kuacha kutumia wanyama katika utafiti, lakini inapowezekana daima wao hutafuta uwezekano mwingine. Kwa kielelezo, sungura hawatumiwi tena kuthibitisha kutungwa kwa mimba wa kibinadamu, kwa kuwa utaratibu fulani wa kemikali upo sasa. Panya buku hawatumiwi tena kutenganisha tubercle bacillus. Njia za kuzalisha viini sasa zaokoa uhai wa wanyama hao ambao kama sivyo wangalikufa. Taratibu nyingine za kuzalisha tishu zimetumiwa badala ya kujaribia panya fulani. Na sungura wengi waliokusudiwa kwa ajili ya jaribio lenye maumivu la Draize huenda wakahifadhiwa kwa sababu ya njia nyingine iwezekanayo ya kutumia utando wa yai la kuku kuwa mahali pa kujaribia. Hakika, watu wanaoumizwa na mteseko wa wanyama watumaini kwamba kutapatikana njia nyingine nyingi ziwe badala, na jambo hilo litukie karibuni.

Hata hivyo, njia kubwa zaidi iwezekanayo kuwa badala ya utumizi wa wanyama kujaribia, itakuwa ile Paradiso ya kidunia ambayo imengojewa kwa muda mrefu na ambayo Wakristo wa kweli wamesali kwa ajili yayo. Yehova Mungu, Muumba mwenye upendo, ameahidi kwamba maradhi yote na kifo chenyewe vitaondolewa milele. Katika ulimwengu mpya wa Mungu ulioahidiwa, binadamu na wanyama wataishi milele wakiwa na amani wao kwa wao, na hakuna chochote kitakachowatia woga. Na hakutakuwako maradhi tena na hivyo kusiwe uhitaji wa kujaribia wanyama. Ukatili utakuwa jambo la wakati uliopita.—Isaya 25:8; 33:24; 65:25; Mathayo 6:9, 10.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki