Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 4/8 uku. 4
  • Karne Yenye Njaa ya Habari

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Karne Yenye Njaa ya Habari
  • Amkeni!—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Utafutaji wa Habari Leo
  • Habari Wakati Ujao
  • Gutenberg—Jinsi Alivyounufaisha Ulimwengu!
    Amkeni!—1998
  • Kutosheleza Uhitaji wa Habari
    Amkeni!—2005
  • Kutokeza Fasihi za Biblia Ili Zitumiwe Katika Huduma
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
  • Kuihubiri Habari Njema Katika Lugha Nyingi
    Amkeni!—1991
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 4/8 uku. 4

Karne Yenye Njaa ya Habari

SIKUZOTE watu wametaka habari za mambo yanayoendelea kuwazunguka. Wanapenda kujua mara moja juu ya chochote chenye kutokeza kinachotukia. Mpeleka ujumbe mmoja ajulikanaye sana alikuwa shujaa wa vita ambaye katika 490 K.W.K. alikimbia karibu kilometa 40 hadi Athene akatangaze kushindwa kwa majeshi ya Uajemi. Yaripotiwa alikufa alipowasili baada ya kutangaza ushindi wa kule Marathon.

Leo, televisheni zipatazo milioni 600 na redio milioni elfu 1.4 huleta nyumbani habari za matukio ya ulimwenguni pote yaliyotukia saa chache tu au hata dakika chache zilizopita. Matukio fulani huonekana moja kwa moja, huku yakitukia. Na mamia mengi ya mamilioni ya magazeti, na pia makumi ya mamilioni ya majarida, huchapwa kila siku katika makumi mengi ya lugha ili kutosheleza ulimwengu wenye njaa ya habari.

Uvumbuzi wa Johannes Gutenberg miaka inayopungua 550 iliyopita wa matbaa ya kuchapa yenye herufi zenye kusonga uliwezesha mwenezo wa haraka wa habari zilizochapwa. Hata hivyo, magazeti ya mapema yalienezwa kwa uchache, na kwa sababu ya gharama yayo ya juu, mara nyingi matajiri peke yao ndio walioweza kuyanunua.

Baada ya muda mfupi uhuru wa uchapishaji ukawa suala. Kwa kielelezo, Gazette la Renaudot lilitangazwa katika karne ya 17 kwa kibali cha mfalme wa Ufaransa, na nyingi za habari zilichapwa chini ya uelekezo wa serikali. Ni waandishi wachache wa wakati huo waliothubutu kukaidi mamlaka ya nchi yao.

Utafutaji wa Habari Leo

Mwisho wa karne ya 19 ulitokeza mvuvumko wa vyanzo vya habari, hasa kwa sababu ya matbaa za uchapaji zinazojiendesha na mwenezo mkubwa sana wa magazeti ya kila siku, hasa katika Ulaya na Amerika ya Kaskazini.

Baada ya muda mfupi utaalamu mpya, hasa redio, ulikuwa ukitumiwa kueneza habari kila mahali. Kwa kielelezo, katika 1917, wakati wa Maasi ya Urusi, kisambaza habari za redio cha meli Aurora kilichochea wakaaji wa Petrograd (sasa Leningrad) waasi.

Wakati wa Vita ya Ulimwengu 2, redio ikaja kuwa chombo chenye nguvu cha kuenezea propaganda, hasa kwa Ujerumani ya Nazi. Wakati wa vita hiyo BBC (Shirika la Utangazaji la Uingereza) katika London lilipeleka hewani pia kwa sehemu kubwa ya Ulaya na ulimwengu habari za Mataifa Yaliyoungana.

Ingawa televisheni ilikuwa imejaribiwa kabla ya Vita ya Ulimwengu 2, ukuzi wayo ulipunguzwa na vita. Hata hivyo, upesi ikasitawi kuwa kileta habari. Leo, programu za habari za televisheni hutazamwa na mamia ya mamilioni.

Katika miongo ya karibuni vyombo vya habari vimeanza kutokeza vichapo vingi vya kipekee. Baada ya Vita ya Ulimwengu 2, magazeti ya kila juma yalitangazwa yakiwa yanachanganua habari. Magazeti yanayoshughulikia mapendezi ya vijana, wanawake, watu waliostaafu, wanamichezo, na mafundi wa vitu, bila kutaja magazeti ya mapitio ya programu za televisheni za kila juma, yanauzwa kwa wingi sana. Kwa kielelezo, katika Ufaransa, karibu magazeti mapya 200 hutokea kila mwaka.

Habari Wakati Ujao

Tayari inawezekana kupata data za mabenki kwenye vioo vya video kupitia miunganisho ya mawasiliano ya simu. Mifumo ya kebo na setelaiti sasa hutoa vyanzo fulani vya televisheni (kama katika United States) vinavyoleta taarifa za habari usiku na mchana, na wengine wanatabiri kwamba wakati ujao utatokeza zaidi katika uwanja wa kimataifa. Kwa hiyo, karne ya 20 yaweza ikaitwa kwa kufaa karne yenye njaa ya habari. Lakini je! nyakati zote habari ni za kutegemeka? Je! utumishi tofauti-tofauti wa habari unatoa uhakikisho wa habari za kihaki, za kikweli?

[Picha katika ukurasa wa 4]

Uvumbuzi wa Gutenberg wa matbaa ya kuchapa yenye herufi zenye kusonga ulikuwa hatua kubwa kuelekea uenezaji wa habari na mawazo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki