Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 12/8 uku. 30
  • Kuihubiri Habari Njema Katika Lugha Nyingi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuihubiri Habari Njema Katika Lugha Nyingi
  • Amkeni!—1991
  • Habari Zinazolingana
  • Kutokeza Fasihi za Biblia Ili Zitumiwe Katika Huduma
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
  • Kuchapisha Vitabu vya Biblia Ili Kumsifu Mungu
    Mashahidi wa Yehova—Wanafanya Mapenzi ya Mungu kwa Umoja Ulimwenguni Pote
  • Msaada Mkubwa wa Kutafsiri
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Kutunza Mali za Bwana-Mkubwa
    Huduma Yetu ya Ufalme—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 12/8 uku. 30

Kuihubiri Habari Njema Katika Lugha Nyingi

WAKATI Yesu alipotoa ishara ambayo ingetia alama siku za mwisho, moja ya sehemu zayo ilikuwa ile kazi ya duniani pote ya kuhubiri habari njema ya Ufalme. (Mathayo 24:14) Ili kuelewa ni kwa sababu gani kuhubiriwa kwa duniani pote katika mataifa yote katika lugha nyingi hakukutendeka kabla ya kizazi hiki, na kwa nini kunaweza na kunatendeka sasa, ni lazima tuangalie historia. Kama vile kamusi ya Webster inavyoeleza, haikuwa hadi kwenye karne ya 15, miaka zaidi ya 500 tu iliyopita, ndipo Gutenberg akawa mbuni wa kupiga chapa kutokana na chapa zenye kusongeka. Kutoka chanzo hiki, mwanadamu alisitawisha njia za kutokeza kurasa zilizochapwa katika kiasi kikubwa kwa ajili ya ugawaji mwingi.

Ni vizuri kukumbuka kwamba kabla ya ubuni wa mtambo wa kupigia chapa, Biblia ilikuwa kitu adimu sana kwa vile ingehitaji kunakiliwa kwa mkono. Kunakili kwa mkono kulikuwa kwenye kuchosha na ghali. Kubuniwa kwa chapa zenye kusongeka na mtambo wa kupiga chapa kulikuwa hatua kubwa sana ya kusonga mbele katika kufanya iwezekane kuchapa Biblia na fasihi zenye kutegemea Biblia katika lugha zote.

Tangu 1914 kumekuwako na maendeleo makubwa ajabu katika uchapaji na utangazaji, kukiwa na mitambo ya ofseti hatimaye ikichukua karibu kazi yote ambayo ilikuwa hapo awali ikifanywa na mitambo yenye chapa za chuma.

Katika miaka ya karibuni zaidi, majilio ya kompyuta pia yamezidisha mwendo wa njia hii. Herufi, alama za lafudhi, na taswira nyingine zingeweza kuchorwa, na kuingizwa katika kompyuta, na kufanywa zipatikane kwa matumizi ya haraka kwa mguso tu wa chapa iliyo kwenye kisehemu cha kupigwa kwa vidole katika kompyuta. Hii imefanya iwe rahisi kuchapisha habari kwa ajili ya watu wa lugha zote kuzunguka ulimwengu.

Katika 1979 Watchtower Society ilianzisha ile inayoitwa mradi wa MEPS. MEPS ni herufi-mfupisho wa “Multilanguage Electronic Phototypesetting System.” Mashirika ya kibiashara yalikuwa yakitokeza kompyuta kwa ajili ya lugha zilizoteuliwa tu mahali ambako fedha walizotoa zingeleta faida. Utendaji wa Sosaiti ni tofauti. Biblia husema kwamba habari njema lazima ijulishwe rasmi kwa “kila taifa na lugha na jamaa.”—Ufunuo 14:6.

Kupitia nyingi za ofisi za Sosaiti katika sehemu zote za dunia, uchunguzi katika tabia za lugha ulifanywa. Orodha ya herufi na lafudhi zote zilizohitajiwa ili kuchapa fasihi katika lugha iliyofanywa na kila tawi ilihitaji kutokezwa. Pia zilizohitajiwa ni kanuni za mgawanyo wa maneno kwa kila lugha. Kila herufi na lafudhi ilipasa kuchorwa, kuingizwa ndani ya kompyuta, na kutengenezwa. Hii ilitia ndani miaka ya kazi yenye kujitoa. Matokeo ni kwamba ujumbe wa Ufalme unaweza sasa kuchapwa katika lugha nyingi sana kuliko awali, na hesabu yaendelea kuongezeka.

Mwanzoni Sosaiti ilibuni na kuunda mtambo wa kompyuta na programu za kompyuta zao wenyewe. Mashahidi wa Yehova kutoka sehemu zote za ulimwengu walikuja kusaidia mradi huu. Kulikuwako kubadilishana kwa stadi na pia kitia moyo. (Warumi 1:12) Ilikuwa kama ugeuzi wa yaliyotokea katika Mnara wa Babeli. Baada ya mafundisho maalumu, vifaa, pamoja na wafanya kazi stadi, walitumwa kwenye matawi kuzunguka ulimwengu. Matokeo ni mfumo wa utangazaji wenye kurekebika kwa urahisi unaotumika katika nchi zaidi ya mia moja na visiwa vya bahari, wenye vifaa vizuri vya kutokeza vichapo vya Sosaiti katika lugha karibu 200 kwa sasa.

Katika hizi siku za mwisho zilizotabiriwa, habari njema ya Ufalme wa Mungu kwa kweli inahubiriwa katika mataifa yote na lugha nyingi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki