Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 12/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Ziara za Binafsi—ni za Kikale?
  • Safari za Utoaji Mimba
  • Panga Ziwe Majembe—Jinsi Gani?
  • Utele wa Sufu
  • Wazazi Fasiki
  • Ustawi wa Kadi za Mkopo India
  • Vijana wa Kifaransa na Kujiua
  • Umama wa Mapema
  • Mapadri Waliooa
  • Malipo?
  • Matumizi Juu ya Watoto
  • Mashahidi Watambuliwa Kihalali Katika Msumbiji
  • Habari Njema Kutoka Urusi
  • Matokeo Yenye Msiba ya Utoaji-Mimba
    Amkeni!—1993
  • Maajabu ya Sufi
    Amkeni!—1992
  • Kutoa Mimba—Si Suluhisho Lisilo na Madhara
    Amkeni!—2009
  • Je, Utoaji-Mimba—Ndio Suluhisho?
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 12/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Ziara za Binafsi—ni za Kikale?

Kwa nini mtindo wa Kiamerika wa kuhubiri evanjeli kupitia televisheni haukukua katika Japani? Bw. Kenji Ishii wa Shirika la Mambo ya Kitamaduni aliliambia Amkeni! kwamba watangazaji wa Japani hawaruhusu programu zinazoomba-omba pesa au kutangaza hewani mafundisho yasiyo ya kisayansi. Hata hivyo, matengenezo ya kidini yamepata njia za akili za kuepa vizuizi hivyo. Mengi hutegemea video, setelaiti za uwasiliano, mitambo ya kompyuta, na mashini za kuwasiliana kwa kunakili ujumbe kwa faksi, ili kueneza imani zao. Kwa wengine, huduma hiyo ya kitekinolojia imechukua mahali pa ziara za binafsi zilizotumiwa na wahubiri katika nyakati za Biblia na ambazo Mashahidi wa Yehova hutumia kwa mafanikio makubwa katika Japani leo. “Tumeng’amua kwamba kufanya ziara za binafsi, ambazo ni mtindo wetu wa zamani wa kimisionari, kumekuwa si wa ki-siku-hizi hata kidogo,” akasema ofisa wa utangazaji wa tengenezo la Kibuddha lenye washiriki milioni sita. Kuhusu utumizi wa ile mashini ya faksi ambayo wao hutumia kutoa sala, Bwa. Ishii alisema kuwa “hii ni kufanya dini kuwa biashara.” “Vikundi vya kidini vinatumia maendeleo ya ki-siku-hizi ili kuchuma pesa.”

Safari za Utoaji Mimba

Kama vile dini, sheria mara nyingi hazifanikiwi katika kuzuia mkondo mbaya wa utoaji mimba. Katika 1989, sheria ilipitishwa katika Jamhuri ya Ailandi iliyozuia utangazaji wa habari kwa chapa kuhusu jinsi na mahali pa kupata utoaji mimba; magazeti kwa mfano, yalipaswa yakomeshe utangazaji wa kliniki za utoaji mimba. Hata hivyo wanawake wengi zaidi na zaidi Waailandi husafiri kwenda Uingereza na visiwa vya Wales ili kutoa mimba. Kulingana na Irish Times ya Dublin, wanawake 981 walifanya safari kama hizo katika miezi mitatu ya kwanza ya 1989. Kwa kipindi hicho hicho katika 1990, idadi hiyo ilipanda kufikia 1,027. Katika sehemu ya Ailandi Kaskazini inayodhibitiwa na Uingereza, sheria ya 1967 ambayo huruhusu utoaji mimba katika Uingereza haitumiki, hivyo Shirika la Mimba la Ulster huelekeza wanawake zaidi ya elfu moja kila mwaka kwenye kliniki za utoaji mimba huko Uingereza.

Panga Ziwe Majembe—Jinsi Gani?

“Tatizo lenyewe ni, unawezaje kuharibu chombo fulani ambacho kimetengenezwa hasa kukinza uharibifu?” lauliza The Wall Street Journal. Kupatana na mkataba wa kupunguza silaha, Urusi sasa yakabiliwa na kazi ya kuangamiza vifaru karibu 40,000. Masuluhisho yaliyodokezwa ya kuharibu vifaru hivyo yametia ndani kulipua baruti ndani yavyo, kuviangusha kutoka juu ili kuviharibu, na kuvitupa kama takataka—bila mafuta, rangi, au mafuta yayo ya breki—ndani ya bahari kuu. Hata wazo lililofikiriwa ni lile la kuvigeuza kwa matumizi ya raia kama vile trekta nzito na magari ya kuzimia moto, lakini “mashine hiyo kubwa yenye mwendo wa pole na yenye kutumia mafuta mengi mno,” ilionwa kuwa isiyofaa. Wenye kuungwa mkono sana ni mpango wa kujenga tanuru ziwezazo kuyeyusha vifaru hivyo na hivyo kutumia chuma hiyo kwa njia nyingine. Kwa sababu tekinolojia hiyo haijakuzwa bado, magari-moshi marefu yalisafirisha vifaru “mashariki kuelekea ng’ambo ya milima ya Urals kwenye vituo vilivyo mbali sana na mamlaka ya ratiba ya mkataba ule na takwa layo kwamba vifaru vipunguzwe na kulipuliwa.”

Utele wa Sufu

Wafugaji kondoo wa Australia, ambao hutoa asilimia 70 ya sufu inayotumiwa kutengeneza nguo ulimwenguni, kwa ghafula wamejipata wakiwa na kondoo wengi mno. Karibu milioni 20 wanaopita kiasi, yaripoti Sunday Correspondent la London, Uingereza. Bei ya kondoo ikiwa imeshuka chini kuwa kadiri ya senti tano kwa kondoo mmoja, wafugaji kondoo wanatumia kiasi kikubwa cha pesa kununua risasi za kuchinjia kondoo kuliko bei za kondoo wenyewe. Kwa nini uhitaji wa sufu la kondoo umeshuka? Correspondent linatoa sababu tatu: Ule mzozo wa Ghuba la Uajemi umesimamisha biashara kati yao na mataifa ya Kiarabu; kupunguzwa kwa wanajeshi ulimwenguni kumepunguza uhitaji wa yunifomu za kijeshi, ambazo kwa kawaida hutengenezwa kwa sufu; na kuongezeka kwa ujotojoto wa tufe kumepunguza uhitaji wa nguo za sufu zenye joto.

Wazazi Fasiki

Mapema katika 1991, gazeti Newsweek liliripoti kwamba kuna watoto milioni saba katika United States wanaoishi na mzazi mlawiti pamoja na mpenzi wa mzazi huyo aliye wa jinsia ile ile. Kulingana na uchunguzi mbalimbali, wengi wa wazazi hawa ni Walawiti wa Kike, wengi wao wakichagua kupata mtoto kwa njia ya uhamilishaji (kutiwa mbegu za kiume). Baadhi ya wataalamu hata huhisi kwamba United States inapatwa na ‘ongezeko la watoto wanaotokana na Walawiti wa Kike.’ Shirika moja la kutangaza kwa chapa limetoa vitabu vya watoto kwa ajili ya watu kama hao. Kitabu kipya cha watoto wa umri wa kutoka miaka miwili hadi sita ni juu ya mvulana anayeishi wakati mwingine na baba yake na mpenzi wa babake wa kiume. Kitabu kwa ajili ya wale wa kutoka umri wa miaka mitatu mpaka minane ni juu ya msichana mwenye “mama wawili.” Vitabu hivyo vimetungwa ili kusadikisha watoto kwamba familia kama hizo ni za kawaida na kwamba ulawiti ni “aina nyingine tu ya upendo.”

Ustawi wa Kadi za Mkopo India

Kampuni kubwa za kadi za mkopo zinaanza kupunguza kule kutotaka kukopa pesa kulikokuwa kwa muda mrefu zoea la jamii ya watu wa kati huko India. Gazeti Asiaweek laripoti kwamba ingawa ni kadi za mkopo 400,000 pekee zinazotumika katika India, washiriki wengi zaidi na zaidi wa jamii ya watu wa kati kiuchumi, wanaofikia idadi ya milioni 150, “wanakubali wazo la kuishi kwa ajili ya leo na kuacha siku ya kesho ijishughulikie.” Hivyo, baadhi ya wanabenki Wahindi wana matazamio mema juu ya wakati ujao. Kama vile mmoja alivyoliambia Asiaweek: “Mtanuo na ukuzi ukiendelea kama ulivyopangwa, India itakuwa soko la 2 la kadi za mkopo ulimwenguni kufikia mwisho wa karne hii—la pili tu kutoka U.S..”

Vijana wa Kifaransa na Kujiua

Kujiua sasa ni kwa pili tu kutoka aksidenti za magari kama kisababishi cha kifo miongoni mwa vijana Wafaransa. Gazeti la Paris Le Figaro laripoti kwamba katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, Ufaransa imepatwa na ongezeko la asilimia 130 katika ujiuaji wa vijana wanaume kutoka umri wa miaka 15 hadi 25 na ongezeko la asilimia 35 miongoni mwa wanawake wa umri huo huo. Ni asilimia 3 tu ya ujiuaji huo inayosababishwa na aina fulani ya ugonjwa mbaya wa akili. Katika mengi ya majaribio ya kujiua miongoni mwa vijana, hakuna tamaa halisi ya kifo, bali, ni kule kutamani sana msaada, kunakokatisha tamaa na wakati mwingine kuleta kifo. Wataalamu huona sababu ya ongezeko la hali ya kukata tamaa kati ya vijana wa leo kuwa mvunjiko wa familia, ufuatiaji wa vitu vya kimwili, na upungufu wa kila siku wa thamani za kijamii na za kiroho.

Umama wa Mapema

“Mmoja kati ya kila watoto saba wanaozaliwa katika Amerika ni mtoto wa mama mbalehe, jumla ya watoto milioni 2.5 kila mwaka,” kulingana na uchunguzi mmoja wa Amerika Kaskazini uliotolewa maelezo katika gazeti moja la Kibrazili liitwalo O Estado de S. Paulo. Brazili imo katika mahali pa kwanza ikiwa na watoto 601,023 waliozaliwa na mama matineja, Meksiko ni ya pili ikiwa na 498,277, na United States ni ya tatu ikiwa na 430,389. Hesabu hizo za juu zilishangaza waanzilishi wa uchunguzi huo, waliokuwa wametarajia kwamba mabadiliko ya kijamii na kiuchumi kwa muda wa miaka 25 iliyopita yangalipunguza mimba za utineja. Namna gani juu ya masuluhisho? Uchunguzi huo ulipendekeza kuwapa vijana vichocheo vya kuwa shuleni kwa muda mrefu zaidi, kufanyia maendeleo hali ya wanawake, na kuhimiza ubikira mpaka wakati wa ndoa.

Mapadri Waliooa

Hivi majuzi, Papa John Paul 2 aliidhinisha kufanywa makasisi kwa mapadri wawili Wabrazili waliooa. “Mapadri hao wapya walitia sahihi hati ambazo kwazo waliahidi kutoendeleza mahusiano ya kingono na wake zao,” laripoti gazeti O Estado de S. Paulo la Kibrazili. Kulingana na gazeti hilo, Aloísio Lorscheider, kadinali wa Fortaleza, akuona “kule kufanya makasisi kwa wanaume waliooa kuwa suluhisho la tatizo la ukosefu wa mapadri.” Kadinali huyo pia alipinga vikali lile takwa la kanisa la kutooa. “Kulingana na Dom Aloísio, useja ni mpango wa ‘kikale’ usio na msingi wa Kibiblia,” lasema gazeti Veja. “Useja haukufanyizwa na Maandiko Matakatifu na, kwa hiyo, sio jambo lisiloweza kukataliwa.” Hata hivyo, Vatikani yaendelea kupendelea zaidi mapadri waseja.

Malipo?

Kulingana na National Catholic Reporter, serikali ya Newfoundland imeahidi kufanya malipo ya kifedha kwa watoto waliodhulumiwa kingono katika makao ya kutunzia watoto yatima ya Mount Cashel. Katika 1975 polisi walipeleleza mashtaka kwamba baadhi ya “Ndugu Wakristo” walioendesha makao hayo walikuwa wakiwadhulumu kimwili na kingono wavulana kwenye makao hayo. Upelelezi huo uliachishwa, na hakuna yeyote aliyekamatwa baada ya wawili wa wale walioshtakiwa kukubali kuondoka Newfoundland na watatu wengine kuondoka kwenye makao hayo ya kutunzia watoto. Hata hivyo, katika 1989, upelelezi ulianzishwa tena; sasa “Ndugu Wakristo” wanane wanashtakiwa kosa la kudhulumu watoto. (Ona Amkeni! ya Novemba 8, 1991, ukurasa 15) Wakili Mkuu Paul Dicks alitangaza rasmi kwamba serikali ilishindwa katika jukumu layo la kulinda yatima wadhulumiwa na itatoa malipo iwapo inafaa. Hata hivyo, yeye alisisitiza kwamba, jukumu la msingi la kufanya upatano lipo juu ya “Ndugu Wakristo” na waajiri wao.

Matumizi Juu ya Watoto

Katika Amerika ya Latini, kati ya watoto milioni 30 walioachwa kutoka umri wa miaka 6 hadi 15, wapatao 2,000 hufa kila siku kutokana na ukosefu wa chakula kinachofaa mwilini au jeuri, laripoti gazeti O Estado de S. Paulo la Kibrazili. Lakini kulingana na James Grant msimamizi wa UNICEF (Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Hazina ya Watoto) kiasi cha pesa kinachotumiwa na ulimwengu katika kupigana na maradhi ya watoto na njaa ulimwenguni pote ni “sawa na kiasi kinachotumiwa kila mwaka na kampuni za sigara za United States katika [utangazaji].” UNICEF inanuia kwamba ni lazima dola 2,500,000,000 zitumiwe mwongo huu ili kuelimisha umma juu ya matatizo ya watoto. Grant asema kwamba ulimwengu hutumia pesa zaidi ya kiasi hicho kila siku kwa silaha na kwamba wanunuzi wa Amerika Kaskazini hutumia pesa zaidi ya kiasi hicho kila mwaka kulisha wanyama vipenzi vyao.

Mashahidi Watambuliwa Kihalali Katika Msumbiji

Utendaji wa kuhubiri wa Mashahidi wa Yehova umeweza kutambuliwa kihalali katika nchi ya kusini-mashariki mwa Afrika ya Msumbiji. Barua moja kutoka kwa Wizara ya Haki, ya Februari 11, 1991, husema: “Mashahidi wa Yehova, kama na mashirika mengine ya kidini, huonea shangwe haki zote na dhamana zilizoandaliwa na Katiba ya Jamhuri ya Msumbiji.” Ilitiwa sahihi na Mkurugenzi wa Mambo ya Kidini wa nchi hiyo. Habari njema hizo zilipokewa kwa furaha na Mashahidi 5,235 walioripoti kuwa walihubiri ujumbe wa Biblia huko Januari uliopita. Walioshukuru pia kwa tangazo hilo la kutambuliwa rasmi walikuwa wajumbe 13,971 waliohudhuria Mikusanyiko mitatu ya “Lugha Iliyo Safi” iliyofanyiwa Msumbiji hivi karibuni, ambapo 357 walibatizwa.

Habari Njema Kutoka Urusi

Katika Machi 28, 1991, Waziri wa Haki alikabidhi wawakilishi wa Mashahidi wa Yehova hati iliyokubali utambulisho halali katika Urusi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki