Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 4/8 kur. 26-27
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • AMRI ZA MAVAZI YA SHULE
  • SAA YASOGEZWA NYUMA TENA
  • TAKWIMU ZENYE KUSHTUA
  • “WAKATI BORA ZAIDI KWA WEZI”
  • WALIOUAWA NA MABOMU YA ATOMIKI
  • Bucharest—Jiji Lenye Majengo ya Kale na ya Kisasa
    Amkeni!—2009
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1996
  • Vita ya Ulimwengu ya Kwanza na Mwanzo wa Huzuni Mbalimbali
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
Amkeni!—1991
g91 4/8 kur. 26-27

Kuutazama Ulimwengu

AMRI ZA MAVAZI YA SHULE

“Wanafunzi wamepigwa, wakapigwa risasi na kunyang’anywa makoti yao ya ngozi na ya manyoya ya bata bukini, mikufu ya dhahabu nzito, viatu vya kimtindo-mtindo na vitu vingine vyenye thamani,” laripoti The Wall Street Journal. “Mwanafunzi mmoja wa shule ya juu katika New York aliuawa kwa ajili ya koti lake. Mwingine katika Detroit, alipatikana amekufa akiwa bila koti na viatu vyake.” Kwa sababu ya jeuri na unyang’anyi ulioongezeka, maofisa katika majiji makuu ya United States yote wamekuwa wakiomba kuwekwe amri zenye kupiga marufuku nguo za kimtindo-mtindo au zenye kutaka mavazi rasmi ya shule yavaliwe. Mingine imetaka wanafunzi wachukue mikoba ya vitabu yenye kuonyesha kilicho ndani ili kuzuia uchukuaji wa silaha zilizofichwa shuleni. “Hata hivyo wanafunzi wengi, wakiwa na uhakika kwamba endapo jambo fulani lenye jeuri litatokea litampata mwingine, hukinza amri za mavazi kuwa ni pigo juu ya utamaduni na uhuru wao wa kujionyesha walivyo katika mtindo,” lasema Journal. Katika kutoa maelezo, ofisa mmoja wa shule asema hivi: “Jamii yetu yote imekuwa yenye kufuatia vitu vya kimwili kupita kiasi. Pupa yaonyeshwa kuanzia ofisi ya juu zaidi ya umma hadi kwenye mabarabara.”

SAA YASOGEZWA NYUMA TENA

Kwa miaka 43 ile “Saa ya Siku ya Maangamizi” ya Bulletin of the Atomic Scientists imeonyesha hali ya usalama wa kimataifa kuhusiana na vita ya nyukilia. “Uwezekano wa vita ya nyukilia kuanzia Ulaya umepungua sana sana,” likataarifu gazeti hilo katika Aprili. “Ijapokuwa mafanikio si hakika kwa vyovyote, hii ndiyo iliyo nafasi kubwa zaidi katika miongo minne ya kuumba ulimwengu ulio salama, wenye kukalika. Kwa sababu hiyo, twarudisha nyuma mikono ya saa ya Bulletin na dakika nne, isimame dakika 10 kabla ya usiku wa manane.” Hata hivyo, huko siko kurudishwa kwa nyuma zaidi kwa mikono hiyo. Katika 1963 na katika 1972, mikono hiyo ilikuwa imewekwa kwenye dakika 12 kabla ya usiku wa manane wakati mapatano yalipotiwa saini kati ya United States na Soviet Union, ijapokuwa Vita ya Maneno iliendelea. “Pambano hilo lilikuwa la maneno kwa maana tu kwamba Vita ya Ulimwengu 3 haikutokea,” lasema Bulletin. “Wakati wa miaka 45 iliyopita karibu vita 125 vilipiganwa, watu zaidi ya milioni 20 wakauawa.”

TAKWIMU ZENYE KUSHTUA

“Ulimwengu leo una mabilionea 157, labda mamilionea milioni 2, na watu milioni 100 wasio na makao,” aandika Alan Durning, mtafiti mkuu wa gazeti World Watch. “Una nusu bilioni [500,000,000] wanaokula mno, na hesabu iyo hiyo ya wale ambao hawali cha kutosha kuweza kuendelea kuishi. . . . Haki ya mgawanyo wa mapato ni mbaya zaidi leo kuliko wakati mwingine wowote tangu rekodi zianze kutunzwa. Watu bilioni moja walio matajiri zaidi hutumia bidhaa na utumishi angalau mara 20 zaidi ya wale watu bilioni moja walio maskini zaidi. . . . Sisi binadamu hutumia dola 200 kwa mwaka kwa kila mwanamume, mwanamke na mtoto kwa mambo ya vita, lakini twaelekea kutoweza kupata dola 1 ambayo kila mmoja wetu angegharimika ili kuokoa watoto milioni 14 wanaokufa kila mwaka kutokana na maradhi madogo kama kuhara.” Kulingana na kadirio moja la Taasisi ya Worldwatch, watu wapatao bilioni 1.2 huishi katika ufukara—asilimia 23.4 ya jumla ya idadi ya watu ulimwenguni.

“WAKATI BORA ZAIDI KWA WEZI”

“Wakati bora zaidi kwa wezi, wavunja nyumba, walanguzi wa madawa ya kulevya, na wakosaji wengine” kushiriki katika utendaji wao mbalimbali usio halali katika wilaya ya Attica ya Ugiriki “ni saa za alasiri za Jumapili,” lasema gazeti ya Athene Elefterotypia. Kwa nini? Kwa sababu mapolisi karibu 3,800 na maofisa 500 huwa wameelekezwa wakati huo kudumisha “hatua za utengemano na usalama” kwenye michezo ya mpira na mashindano mengine ya riadha. Na ikitukia Jumapili pia ndiyo ile ya mechi “Kuu,” kikosi hicho huongezewa polisi 700 na maofisa 100. Gazeti hilo laongeza hivi: “Kuwapo kwa wawakilishi wa polisi kwenye kila mechi ya riadha ni jambo la lazima zaidi ya wanariadha wenyewe.”

WALIOUAWA NA MABOMU YA ATOMIKI

Ni watu wangapi barabara wamekufa kwa sababu ya mabomu ya atomiki yaliyoangushwa Hiroshima na Nagasaki katika 1945? Kulingana na uchunguzi mmoja uliofunuliwa na Wizara ya Afya na Masilahi ya Japan, vifo 295,956 vimehusishwa na mabomu hayo kufikia 1988. Kati yao, watu 25,375 katika Hiroshima na 13,298 katika Nagasaki walisemekana walikufa siku mabomu hayo yalipolipuliwa; wale wengine wamekufa tangu wakati huo, wengi siku chache baada ya kulipuliwa kwa mabomu hayo, ikiwa ni kwa sababu ya maradhi yenye kutokezwa na mnururisho. Jamaa za waliokufa wamelaumu serikali kwa kungojea mno kabla ya kufanya uchunguzi huo. Kuongezea hayo, “haukushughulika hasa na pande zote za ulipuaji wa mabomu hayo wala jumla ya hesabu ya wale waliokufa kwa sababu yayo,” asema Yoshio Saito, kaimu wa katibu-mkuu wa Shirikisho la Japan la Matengenezo ya Watesekaji wa Mabomu ya Atomiki na Haidrojeni.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki