Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 6/8 uku. 29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • KUTOJUA KUSOMA KWA ULIMWENGU
  • KUTUMIA MNO DAWA ZA KUMALIZA MAUMIVU
  • MAHUSIANO MAPYA YA SOVIET-VATICAN
  • VITA VYA AFRIKA
  • WATOTO WALELEWA KWA AJILI YA DHABIHU
  • Sehemu ya 2—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya Dunia
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
  • Mwisho wa Enzi—Je, Ni Tumaini kwa Wakati Ujao?
    Amkeni!—1996
  • Ufalme Uliojengwa Juu ya Mchanga, Mafuta, na Dini
    Amkeni!—1992
  • Mashahidi wa Yehova Katika Ulaya Mashariki
    Amkeni!—1992
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 6/8 uku. 29

Kuutazama Ulimwengu

KUTOJUA KUSOMA KWA ULIMWENGU

“Watu bilioni moja [1,000,000,000] katika ulimwengu hawawezi kusoma—hata majina yao wenyewe, kwa ujumla,” lasema gazeti Asiaweek. “Na kutojua kusoma na kuandika hakupungui, kama ambavyo watu wengi walioelimika wanavyopenda kufikiri.” India yaongoza ulimwengu ikiwa na watu milioni 290 wasioweza kusoma wala kuandika, ambapo China yafuata ikiwa na milioni 250. Katika nchi nyingi, wavulana wanaelekea zaidi kupata elimu kuliko wasichana. Uwiano wa dunia yote ni mtu wa kiume 1 katika 5 asiyeweza kusoma, ikilinganishwa na 1 katika 3 kwa watu wa kike.

KUTUMIA MNO DAWA ZA KUMALIZA MAUMIVU

Ofisa mmoja wa Australia hivi karibuni alitangaza kwamba ‘Waaustralia hutumia dawa za kumaliza maumivu milioni elfu nne kila mwaka,’ kulingana na The Courier Mail. Hangaiko kuu ni kwamba hesabu yenye kuongezeka ya watoto wa shule, hasa wasichana, wanakuwa wazoevu wa kutumia dawa hizo. Idara ya Elimu ya Australia imetayarisha kitabu Painkillers: A Student Workbook kitawanye kwa shule zote za taifa. Kusudi la kitabu hicho ni “kujaribu kupunguza uhitaji wa watoto wa shule kutumia dawa ili kukabiliana na matatizo,” likasema The Courier Mail. Tabibu mmoja alisema kwamba “wasichana wengi wamekua wakifikiri wanapaswa kumeza tembe kwa ajili ya kila ugonjwa.” Pia aliorodhesha ugonjwa wa chembe nyekundu za damu, kuvimbiwa, na maumivu ya tumbo kuwa athari ziwezazo kutokezwa na matumizi mabaya ya dawa za kumaliza maumivu. Yeye apendekeza kunywa maji, kulala mapema, kufanya mazoezi, kutembea katika hewa safi, na vyakula vya ukawaida vyenye kuslisha mwili kuwa masuluhisho ya badala kwa ajili ya maumivu ya kichwa na maumivu madogo madogo.

MAHUSIANO MAPYA YA SOVIET-VATICAN

Mkutano kati ya Papa John Paul 2 na rais wa Soviet Mikhail Gorbachev Desemba 1989 umefanya mwaka 1990 kuwe mahusiano rasmi kati ya Vatican na Soviet Union kwa mara ya kwanza tangu yale Mapinduzi ya Kirusi ya 1917. Yakielezwa na mnenaji wa Vatican Joaquim Navarro kuwa “mahusiano ya kutangulia yale ya kibalozi,” mapatano hayo yataka Vatican ilibadilishane mwakilishi mwenye cheo cha apostolic nuncio na mwakilishi wa Soviet mwenye cheo cha balozi maalumu. Yasemekana Gorbachev alimwahidi papa uhuru wa dini utahakikishwa na Soviet Union.

VITA VYA AFRIKA

“Yawezekana kwamba watu milioni tatu au zaidi walikufa kwa sababu ya vita vya Afrika wakati wa miaka kumi iliyopita,” kulingana na gazeti Lesotho Today. Makadirio ya vifo katika Vita vya Ethiopia ni kuanzia “kati ya 500,000 na milioni moja.” Lesotho Today laongeza kwamba yawezekana idadi ya watu maskini mashambani ndiyo imetaabika zaidi, likieleza kwamba “Waafrika wapatao milioni tisa hadi 12 walikoseshwa makao na vita, wakawa wakimbizi au wakahamishwa.” Kulingana na The Star la Johannesburg, Afrika Kusini, maisha zikadiriwazo kuwa 600,000 zimepotezwa katika Musumbiji wakati wa vita ya wao kwa wao, miongoni mwao wakiwa watoto 380,000. Hiyo ni zaidi ya mara kumi ya hesabu ya vifo vya Waamerika katika Vita ya Vietnam.

WATOTO WALELEWA KWA AJILI YA DHABIHU

Uchunguzi mbalimbali katika zoea la ibada ya Kishetani katika sehemu mbalimbali za Afrika Kusini waonyesha kwamba mnaso wayo kwa vijana unaenea sana. Hata hivyo, kulingana na Saturday Star, gazeti moja la Afrika Kusini, “familia nzima nzima—akina baba, akina mama na watoto—”wanahusika, na waabudu fulani wa Shetani ni “wataalamu wa kazi wenye cheo kikubwa katika jumuiya.” Polisi wanachunguza mazoea ya kutumia watoto vibaya, kulala kinguvu, kufanya ngono na wanyama, na kuuawa kwa watoto wachanga. Waliokuwa waabudu wa Shetani hapo zamani wamefunulia polisi wa Cape Town kwamba watoto wachanga 11 wameuawa kisherehe wakati wa miaka mitano iliyopita na kwamba watoto hao walilelewa hasa kwa ajili ya dhabihu, likasema Saturday Star.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki