Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 1/8 kur. 16-18
  • Ufalme Uliojengwa Juu ya Mchanga, Mafuta, na Dini

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ufalme Uliojengwa Juu ya Mchanga, Mafuta, na Dini
  • Amkeni!—1992
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Saudi Arabia—Yale ya Zamani na Yale Mapya
  • Makka, Kaaba, na Kurani
  • Maisha ya Ki-Siku-Hizi Katika Saudi Arabia
  • Kasoro Huwa Haikosi Katika Kila Jambo
  • Sehemu 14: 622 W.K. na Kuendelea—Kunyenyekea Penzi la Mungu
    Amkeni!—1990
  • ‘Ole, Ole, Jiji Lile Lililo Kuu’
    Amkeni!—1994
  • Uislamu—Njia Inayoongoza kwa Mungu kwa Unyenyekevu
    Jitihada ya Ainabinadamu ya Kutafuta Mungu
  • Utamwambia Nini Mwislamu?
    Huduma Yetu ya Ufalme—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 1/8 kur. 16-18

Ufalme Uliojengwa Juu ya Mchanga, Mafuta, na Dini

NI NCHI gani iliyo na ukubwa kama wa Ulaya Magharibi, ina idadi ya watu milioni 12 pekee, na karibu yote ni jangwa? Ni ufalme gani ulioanzishwa katika 1932, ukagundua mafuta mengi sana katika 1938, na ukawa mfanyizaji mkubwa wa mafuta yasiyosafishwa ukiwa wa tatu duniani? Ni ufalme gani huichukua Kurani kuwa katiba yake na pia wenye miji miwili ya Kiislamu na misikiti yenye kustahiwa zaidi?

Jibu la maulizo hayo yote ni Ufalme wa Saudi Arabia, unaotawalwa na Mfalme Fahd Bin Abdul Aziz. Ukichukua sehemu ya kilomita za mraba 2,240,000 unachukua sehemu kubwa ya peninsula ya Arabia, Bahari ya Shamu ikiwa upande wa magharibi, Bahari ya Arabia upande wa kusini, na Ghuba ya Arabia upande wa Mashariki.

Nilikujaje kupendezwa na nchi hii ya Waarabu? Niliona katika gazeti mwaliko wa maonyesho katika Jiji la New York kwa udhamini wa serikali ya Saudi Arabia. Nilipendezwa kujua mengi zaidi juu ya utamaduni huu tofauti na njia ya maisha. Na kwa sababu labda singefika kamwe Saudi Arabia, nikaona kwa nini nisiruhusu Saudi Arabia ije kwangu?

Saudi Arabia—Yale ya Zamani na Yale Mapya

Punde tu nilipoingia sehemu ya maonyesho, niling’amua kwamba kila kitu kiliundwa ili kuufanya umma uhisi vema kuhusu nchi hii ya Kiarabu. Kila mahali kulikuwako wanafunzi wanaosomea U.S. wa chuo kikuu cha Saudi waliotumika kama waelekezi wenye ujuzi. Wote walivalia thobe asilia, vazi refu jeupe ambalo hufanana na joho na hufikia miguuni. Kila mmoja pia alivaa ghutra au kitambaa cha kichwani chenye miraba-miraba, kilichoshikiliwa kichwani kwa kamba nyeusi yenye kuzunguka mara mbili. Wote walizungumza Kiingereza kizuri na kujibu maulizo yetu yote kwa njia ya fadhili.

Nikifuatia kwenye sebule isiyokuwa na mwangaza mwingi, ambayo ilikuwa na picha za familia ya kifalme ya Saudi na pia onyesho la slaidi nyingi za mambo mbalimbali ya Saudi Arabia, nilizuru sehemu ambayo ilionyesha maisha ya kikawaida ya Waarabu na Mabedui. Hema ya Mabedui weusi ilionyeshwa pamoja na vitu vyao wanavyotumia katika maisha yao ya kuhamahama. Hata hivyo, kukiwa na maendeleo ya tekinolojia ya ki-siku-hizi, mtindo-maisha wa Mabedui, pamoja na mapokeo yao ya ukaribishaji wageni, unaendelea kutoweka.

Sehemu iliyofuata ya utalii ilikuwa ni ukumbusho wa kani ya kidini ambayo huelekeza na kudhibiti maisha ya Saudi Arabia—Uislamu.a

Makka, Kaaba, na Kurani

Kitabu kitakatifu cha Kiislamu, Kurani, “huonwa kuwa ndicho sheria ya [Saudi Arabia] na huandaa thamani za kimaadili na uelekezi,” yasema broshua moja rasmi. Kitabu kimoja kidogo husema: “Ufalme huu huunda sera zake za kijamii, kisiasa, na kiuchumi katika mwangaza wa mafunzo ya Kiislamu.” Ingawa kulikuwa nakala za kurani zilizoandikwa kwa mikono kwenye maonyesho, jambo kuu katika sehemu hii ilikuwa ni mji wa kuzuru wa Makka (Kiarabu, Makkah) likiwa na msikiti walo mkubwa na Kaaba ikiwa katikati. Hayo yalionyeshwa kwa vifananishi vikubwa vikubwa.

Kaaba, jengo kubwa la kyubiki lililojengwa kwa mawe na kufunikwa kwa nguo nzito nyeusi, inafafanuliwa na kichapo kimoja cha Kiislamu kama “mahali pa ibada ambapo Mungu alimwamuru Abrahamu na Ishmaeli kujenga zaidi ya miaka elfu nne iliyopita.”b Hivyo Uislamu (kuanzia na nabii Muḥammad katika karne ya saba W.K.) hudai kuwa umeunganishwa na Abrahamu, mzee wa ukoo mwanzilishi wa dini ya Kiyahudi na Ukristo. Hiyo basi ni mojapo dini tatu kubwa zenye kuabudu Mungu mmoja.

Kwa kweli Kaaba imo katikati ya uwanja mkubwa ulio wazi ambao hufanyiza sehemu ya msikiti mkubwa wa Makka. Kwenye ziara za kila mwaka (ḥajj), zaidi ya Waislamu milioni moja hukusanyika humo kuomba na kuzunguka Kaaba mara saba. Kila Mwislamu anayejiweza huliona kuwa jukumu kufanya safari hii angalau mara moja maishani. Maonyesho hayo yalitia ndani kifananishi cha msikiti mkubwa wa Medina (Kiarabu, Madinah), mahali pa maziko ya Muḥammad.

Yenye kupendeza zaidi ni ile milango mizito yenye madoido ya Kaaba ambayo ilionyeshwa. Kwa kawaida, ni Waislamu pekee ambao huweza kuona hiyo, kwa sababu ni wao tu wanaoruhusiwa kuingia ndani ya msikiti wa Makka. Ilikuwa vigumu kuamini kwamba ilikuwa ya asili mpaka mwelekezi alipoeleza kwamba ilikuwa milango iliyotumiwa kutoka 1942 hadi 1982, wakati ilipobadilishwa kwa mingine mipya. Imefanyizwa kwa dhahabu na fedha na kurembeshwa kwa vibapa vya dhahabu ambavyo vilikuwa vimeandikwa mistari ya Kurani katika Kiarabu. Lililokuwa limeangikwa kwenye ukuta ni kiswah, au pazia nyeusi nzito, lililotumiwa kuifunika Kaaba, likiwa limepambwa kwa manukuu zaidi ya Kurani kwa dhahabu.

Maisha ya Ki-Siku-Hizi Katika Saudi Arabia

Mbele zaidi katika kutalii kwetu, kulikuwa na vifananishi vya mandhari ya barabara za kawaida, mafundi wakifuma mikeka na wengine wakigeuza chuma kuwa vifaa vya kutumika nyumbani. Mafundi wengine walikuwa wanafanya kazi ya ngozi ya kutengeneza sapatu za Kiarabu zilizo za kawaida. Mwingine alikuwa anatengeneza vizimba vya nyuni vilivyotengenezwa kwa mbao na vilivyo sahili. Hali mwingine alikuwa anaunda vyungu kwa kutumia gurudumu la kuendeshwa kwa mguu.

Hatimaye nilikuja kwenye sehemu ambayo ilitokeza juu ya matimizo ya Saudi Arabia ya kisasa. Ilikuwa wazi kwamba kugunduliwa kwa mafuta kulikuwa kumebadili uchumi wa Saudi na kiwango cha maisha cha taifa. ARAMCO (Kampuni ya Mafuta ya Arabia na Amerika) iligundua akiba kubwa ya mafuta katika 1938. Violezo vya machupa yenye mafuta hayo meusi vilionyeshwa. Broshua moja ya kampuni yasema: “Aramco sasa ina zaidi ya wafanyakazi 43,000, karibu visima 550 vyenye kutoa mafuta, ina mabomba ya mafuta yenye eneo ya kilometa 20,500 na zaidi ya vituo 60 vya kutenganisha mafuta na gesi.”

Basi haishangazi kwamba kukiwa na msingi imara wa kiuchumi jinsi hiyo, broshua za habari zaweza kusema kwamba Saudi Arabia hutegemeza shule 15,000 na vitovu vya elimu vinavyotumikia wanafunzi zaidi ya milioni 2.5. Elimu ni ya bure kwa kila mtu hadi kwenye chuo kikuu. Na kuna vyuo vikuu saba.

Bila shaka, mafuta si ndilo tu jambo la lazima sana katika Saudi Arabia. Miradi mikubwa ya kunyunyizia mimea maji imekamilishwa, na kilimo kimestawi kufikia hatua ya kwamba nchi hiyo huuza samaki, ndege wa kufugwa, ngano, tende, mboga za majani, na bidhaa za maziwa na nyinginezo za ukulima katika soko la nchi za nje.

Kasoro Huwa Haikosi Katika Kila Jambo

Nilimaliza ziara yangu ya “Saudi Arabia” ya saa tatu nikiwa nimevutiwa sana na mambo makubwa ambayo nchi hiyo ndogo kwa ulinganisho imeweza kutimiza. Nilishangaa jinsi mambo yangalikuwa tofauti kama kila taifa lingekuwa limebarikiwa ivyo hivyo na akiba ya petroli au mali nyingine mbalimbali iliyo na thamani yenye kutakwa ulimwenguni kote.

Ingawa niliona ziara hiyo ikiwa yenye kuelimisha sana, niliona pia mambo yaliyoachwa nje katika nyanja za kidini. Sikujifunza lolote juu ya jiwe halisi la Kaaba, jiwe jeusi lililotoka kwenye nyota ambalo hustahiwa na Waislamu ambao huzuru Makka. Kabla ya kuanzishwa kwa Uislamu, jiwe hilo “lilistahiwa kama kago [hirizi],” asema Philip K. Hitti katika History of the Arabs. Pokeo ni kwamba wakati Ishmaeli alipokuwa anajenga Kaaba upya, alipokea jiwe hilo jeusi kutoka kwa malaika Gabrieli.

Jambo jingine lililoachwa nje katika maonyesho hayo ni kwamba sikupata rejezo lolote kwa migawanyiko miwili mikubwa ya Uislamu, yaani Sunni na Shia. Mgawanyiko huu hurudi nyuma hadi wakati wa waandamizi wa Muḥammad na msingi wake huwa juu ya utofautiano wa mafafanuzi juu ya ni nani hasa walio warithi waandamizi wake wa kiroho—je, mstari huo unafuatia ukoo wa Muḥammad kama ambavyo Waislamu wa Shiite hudai au inategemea uchaguzi rasmi kama ambavyo Wasunni walio wengi hudai? Wasaudi wako katika sehemu ya farakano ya Wahhabi wa shule ya Hanbali, shule imara zaidi ya zile nne za Waislamu wa Kisunni.

Wenye kuonekana wazi ulikuwa ni ukosekano wa wanawake wa Kiarabu, katika maonyesho hayo. Nilidhania tu kwamba ukosefu huo ulikuwa kwa sababu ya mafafanuzi ya sheria ya Kiislamu juu ya daraka la wanawake katika maisha ya umma.

Nilipokuwa nikiondoka kwenye maonyesho hayo, nilikumbushwa sana juu ya kwamba kasoro huwa haikosi katika kila jambo. Nje kwenye barabara, kulikuwa na walalamishi wa Kiarabu wakitoa vikaratasi vyenye kutoa hoja za matendo ya ukatili na ukosefu wa haki katika Saudi Arabia wakilaumu ukosefu wa demokrasi katika nchi hiyo (hakuna wafanya sheria au bunge). Ilinifanya nitambue kwamba kwa watu fulani, mchanga, mafuta, na dini havikamilishi kila kitu. Lakini angalau nilikuwa nimepata picha ya wazi zaidi juu ya maisha katika Saudi Arabia na matokeo ya Uislamu juu ya watu wake.—Imechangwa.

[Maelezo ya Chini]

a Ili kupata habari zote za Kiislamu, ona kitabu Mankind’s Search for God, kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc., 1990, sura ya 12, “Islam—The Way to God by Submission.”

b Hakuna rejezeo katika Biblia kuonyesha tukio hilo wala kwamba Abrahamu alikuwa katika Makka ya kale.—Mwanzo 12:8–13:18.

[Ramani/Picha katika ukurasa wa 16]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

SAUDI ARABIA

Makka

IRAN

IRAQ

SUDAN

Bahari ya Shamu

Bahari ya Uarabuni

[Picha katika ukurasa wa 17]

(kutoka kushoto) Milango ya Kaaba, msanii Mwarabu, na kurembesha maandishi ya Kiarabu

[Hisani]

David Patterson

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki