Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 8/8 uku. 31
  • “Tatizo Kubwa la Kingono Kati ya Makasisi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Tatizo Kubwa la Kingono Kati ya Makasisi
  • Amkeni!—1991
  • Habari Zinazolingana
  • Waliodhulumiwa Kingono na Mapadri Wakiwa Watoto Wateta Waziwazi
    Amkeni!—1993
  • ‘Aibu Yetu Iko Wazi kwa Ulimwengu Mzima’
    Amkeni!—1991
  • Muono-Ndani Juu ya Habari
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Mungu Huonaje Ibada ya Jumuiya ya Wakristo?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 8/8 uku. 31

“Tatizo Kubwa la Kingono Kati ya Makasisi

“TATIZO kubwa la ngono linararua mfumo mkuu wa fahamu za Kanisa Katoliki, “akasema Jason Berry, mtungaji wa Louisiana aliyepokea tuzo la Shirika la Kikatoliki la Waandishi kwa kuzungumza katika gazeti National Catholic Reporter juu ya jinsi watoto wanavyofanyiwa ngono. Kuhusu matendo ya ngono potovu ambazo watoto wanatendwa na makasisi, Berry aliendelea kusema katika The Washington Post:

“Tangu 1985, hesabu ya visa vingi vya kutenda watoto ngono ambavyo vinahusu mapadri au mabradha vimerekodiwa kotekote Amerika na Kanada. Kama tokeo, maeneo ya maaskofu katika United States yamepata hasara kubwa kwa kushtakiwa mahakamani, na bima juu ya matendo kama hayo imetoweka. Mabadiliko haya yameanza kati ya ripoti kadhaa kwamba mapadri asilimia 10 hadi 20 wa United States huenda wakawa ni walawiti wenye kutenda.”

The Providence Sunday Journal la Kisiwa cha Rhode yasema: “Maaskofu katika mikoa 29 . . . wamekabiliwa na madai ya madhara kutoka kwa waliodhulumiwa kingono na makasisi Wakatoliki, na Kanisa limelipa karibu dola milioni 60 kufikia sasa katika maamuzi na masuluhisho.” Katika Louisiana, padri mmoja alikubali kwamba alikuwa amedhulumu wavulana 35 na akahukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani, ingawa gazeti la Journal lasema ilikuwa wazi kwamba yeye “alikuwa amevamia angaa watoto 75 kwa muda wa miaka 10.” Na kasisi mmoja wa Kisiwa cha Rhode aliungama kuwa ana hatia kwa mashtaka 26 ya dhuluma ya kingono iliyohusu wavulana wachanga.

Uchunguzi uliofanywa katika Covenant House, himaya ya vijana waliotoroka nyumbani katika Jiji la New York, ulifunua kwamba padri aliyekuwa mwenye usimamizi alikuwa amejiingiza katika ukosefu wa adili za ngono pamoja na baadhi ya vijana wa kiume na wavulana wachanga. Na askofu mkuu wa Roma Katoliki wa Atlanta alijiuzulu baada ya kujulikana kwamba alikuwa amekuwa na uhusiano wa kingono na mama mmoja asiyeolewa kwa miaka miwili mfululizo.

Baraza la maaskofu Wakatoliki wa United States lilipokea ripoti juu ya “msiba mkuu” wa madai kwa mapadri juu ya upotovu wa ngono dhidi ya watoto. Ripoti hiyo ya kurasa 100, yasema Journal hiyo, ilieleza kirefu njia ya kupunguza madeni ya Kanisa kutokana na madai ya watu kufikia dola bilioni moja [dola milioni elfu moja] yakitegemea mashtaka 30 yanayobaki.” Mashtaka hayo yanaletwa na wazazi Wakatoliki wa watoto wanaohusika. Na madaktari wa akili wanaotibu wale wadhulumiwa wachanga wa uhalifu huu wanaripoti madhara ya muda mrefu, mara nyingi yenye kudumu.

Neno la Mungu husema juu ya “tamaa za aibu” kama hizo ambazo kwazo wanaume ‘wanawakiana tamaa, wanaume kwa wanaume wakifanya matendo ya haya,’ na kuongeza kwamba “hukumu ya haki ya Mungu” ni kwamba “wanaofanya maneno kama haya wanastahili kufa.”—Warumi 1:26, 27, 32, ZSB; ona pia 1 Wakorintho 6:9, 10.

Bila shaka, sehemu kubwa ya tatizo hilo hutokea kwa sababu ya zoea lisilo la kimaandiko la useja, kukataza mapadri kuoa. Hata hivyo, Biblia, Neno la Mungu, yasema wazi kwamba wale walio katika huduma ya Kikristo waweza kuoa. Kama vile Biblia Douay Version ya Katoliki inavyosema: “Inampasa basi askofu awe . . . mume wa mke mmoja.” (1 Timotheo 3:2) Na pia inasema kwamba ‘kukataza kuoa’ ni ithibati ya kwamba “watu fulani wataondoka kwenye ile imani, wakitii roho za makosa, na mafundisho ya maibilisi.”—1 Timotheo 4:1-3.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki