Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 3/8 uku. 21
  • Barua Kutoka kwa Mtakia-Mema

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Barua Kutoka kwa Mtakia-Mema
  • Amkeni!—1992
  • Habari Zinazolingana
  • Sikukuu na Maadhimisho
    Shule na Mashahidi wa Yehova
  • Kanuni za Adili Zinazostahili Staha
    Mashahidi wa Yehova na Elimu
  • “Wokovu Una Bwana”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2002
  • Mtoto Wako Atasema Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 3/8 uku. 21

Barua Kutoka kwa Mtakia-Mema

HIVI karibuni barua ilipokewa kutoka kwa mtakia-mema mmoja katika nchi ya Kiafrika ambako kazi ya Mashahidi wa Yehova imepigwa marufuku. Mtu huyo aliandika hivi:

“Bwana Mpendwa,

“Nitaanza moja kwa moja na jambo lenyewe; Nataka tu kuwakumbusha kwamba utendaji wa kanisa lenu hauruhusiwi na serikali ya humu. Jinsi hilo linavyoniudhi!

“Sipati tena Amkeni! langu kwa ukawaida. Lakini nawaambia, Amkeni! ndilo labda gazeti zuri zaidi ambalo nimepata kujua. Linawashauri wasomaji jinsi ya kujiongoza kwa mafanikio na usawa, kihalali na kiroho. Ni chombo cha ajabu.

“Mimi naamini kwamba hakuna mwalimu yeyote wa chuo kikuu anayejua mengi au hufundisha katika njia hiyo ya undani. ‘Mapadri’ wetu ndio wabaya zaidi. Na hali serikali yetu inasema haya magazeti na mengine kama haya, ambayo yanaelimisha watu sana, ni marufuku. Kwa nini? Kwa sababu wachapishaji hawaisalimu bendera. Sawa.

“Lakini swali ni hili: Mtu akisalimu na huku anafuja za nchi, anakubali hongo, anaepa kodi, anaua kimakusudi, na kadhalika, je, mtu huyo aweza kusemwa kuwa mwaminifu? Hivyo ndivyo ‘Wakristo’ wetu hufanya. Wanasalimu bendera kwenye uwanja wa paredi na hata kuzipeleka mahali pao pa ibada wakazisalimu huko. Wakristo eti! Najua mimi si mkamilifu wala hata si mwema machoni pa Mungu. najua hivyo. Lakini kwa asili hivyo sivyo inavyopasa kuwa

“Ninyi Mashahidi hukataa kusalimu bendera, kutiwa damu mishipani, Krismasi na Ista na kwa mkazo mkubwa hata zaidi mwakataa uhalifu, kufuja pesa, hongo, kuua kimakusudi. Na mwakataa uzinzi na uasherati. Taja maovu yote, na hakika Mashahidi watakataa katakata.

“Natumaini na kuomba kwamba serikali itafahamu kosa ililofanya na kulipa kanisa lenu uhuru wa kufundisha.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki