Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 5/8 uku. 6
  • Sizo Njia Bora Zaidi za Kufanya Mabadiliko

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Sizo Njia Bora Zaidi za Kufanya Mabadiliko
  • Amkeni!—1992
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mbano wa Kisiasa
  • Upasuaji wa Ubongo na Uchocheo wa Umeme
  • Dawa
  • Ubongo Wako Hufanyaje Kazi?
    Amkeni!—1999
  • Jinsi Unavyoweza Kubadili Namna Ulivyo
    Amkeni!—1992
  • Ubongo Wako Unatatanisha Ajabu
    Amkeni!—1999
  • Jinsi Ulivyo Kiumbe cha Kipekee!
    Je, Kuna Muumba Anayekujali?
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 5/8 uku. 6

Sizo Njia Bora Zaidi za Kufanya Mabadiliko

VIGEZO vya tabia vikiisha kuimarishwa, badiliko linaweza kufanywaje? Ni nani ungeweza kumwendea, na ni njia zipi zinazoweza kutumiwa ili kutokeza maendeleo ya kudumu?

Acheni tuchunguze njia fulani za kupita kiasi zinazotumiwa leo.

Mbano wa Kisiasa

Mamilioni ya watu leo wanaishi chini ya tawala ambazo hutafuta kudhibiti fikira na kanuni za tabia. Serikali hizo hutumia uwezo wazo ili kushurutisha badiliko—nyingine kwa hila, nyingine kwa kulazimisha. Nyingine hutumia njia za ujanja, mara nyingi kutia ndani vitisho, vifungo gerezani, na mateso. Wakidhibiti vyombo vya habari na mifumo mingine ya elimu, wanatafuta kubadilisha mawazo yaliyowekwa zamani kwa yale yanayotakwa na viongozi mashuhuri wa sasa. Upinzani wote unaotokezwa hukandamizwa kwa nguvu. Mtu yeyote anayekataa kuongozwa huenda akatendewa tendo la kutisha ambalo mara nyingi huvunja moyo mtu mmoja mmoja.

Upasuaji wa Ubongo na Uchocheo wa Umeme

Sehemu fulani za ubongo zimetambulishwa kuwa zinaathiri namna moyo wa mtu ulivyo na aina za tabia. Upasuaji wa ubongo unatia ndani kutolewa au kuharibiwa kwa tishu za ubongo katika sehemu hiyo ya ubongo. Ikishatolewa, sehemu hiyo ya ubongo wako haiwezi kufanya kazi tena, na tabia yoyote iliyoongozwa nayo itapotea.

Inasemwa kwamba maelfu ya visa vya upasuaji kama huo vimefanywa, hasa kwa watu wenye tabia ya kuwa wakaidi na hatari kingono. Wengine wemeingizwa ncha za umeme ndani ya ubongo wao, na wakati ulipopitishwa, ulichochea au ukaziba utendaji wa ubongo mahali pale. Inasemekana kwamba hilo hupunguza msukumo unaoathiri tabia inayodhibitiwa na sehemu hiyo ya ubongo.

Dawa

Utumizi wa dawa katika ugonjwa wa akili ni jambo lililosambaa na lenye kuhitajiwa mara nyingi. Kuna dawa za kutuliza, dawa za kuleta usingizi, dawa za kuchangamsha, na dawa za kurekebisha kutosawazika kwa kemkikali katika ubongo. Kuna dawa ambazo pia zimetumiwa kwa kuadhibu katika magereza na nyingine katika vituo vya kurekebishia tabia. Aina mbili za dawa kama hizo ni apomofini na Anektini.

Apomofini imetumiwa kwa wafungwa ambao tabia yao ilionekana kuwa isiyokubalika. Husababisha uchefuchefu mbaya sana na kutapika. Mfungwa huambiwa kwamba ikiwa atakuwa na tabia mbaya tena, atapewa apomofini zaidi. Haya huitwa pia matibabu ya kukirihisha. Anektini husababisha pumu, hisi za kukazwa koo katika mfungwa asiye na tabia nzuri. Anafikiri atakufa. Akikosa tabia tena, anaongezewa Anektini.

Je! hizi ndizo njia ambazo wewe ungetumia kubadili kigezo cha tabia yako?

Nyingi za njia zilizo juu huvunja hiari. Zatia ndani pia uvutano wa watu wenye uwezo juu ya mwenzao lakini bila nia ya kumnufaisha. Je! uwezo wa kisiasa hutafuta manufaa yake mwenyewe au yale ya mtu mmoja mmoja? Katika upasuaji wa ubongo, ni nani hushika kisu cha udaktari? Ni nani hudhibiti kibonyezo wakati uchocheo wa umeme unapotumiwa? Matibabu ya kukirihisha hubaki kwa muda gani? Je! mtoa matibabu aweza kutumainiwa?

Acha tuchunguze njia inayokubalika zaidi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki