Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 5/8 kur. 3-4
  • Ubongo Wako Unatatanisha Ajabu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ubongo Wako Unatatanisha Ajabu
  • Amkeni!—1999
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kuchunguza Ubongo Wako
  • Ubongo Wako Hufanyaje Kazi?
    Amkeni!—1999
  • Jinsi Ulivyo Kiumbe cha Kipekee!
    Je, Kuna Muumba Anayekujali?
  • Mtaalamu wa Ubongo Anaeleza Kwa Nini Anamwamini Mungu
    Amkeni!—2017
  • Ubongo Wako Unaweza Kuutumiaje kwa Njia Bora?
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 5/8 kur. 3-4

Ubongo Wako Unatatanisha Ajabu

“Ubongo wa binadamu ni fumbo kubwa sana: inawezekanaje kitu kinachofanana na yai bichi kufanyiza ‘akili’ yako, mawazo yako, utu wako, kumbukumbu zako na hisia zako, na hata ufahamu wako wenyewe?” —Profesa Susan A. Greenfield, The Human Mind Explained.

UBONGO wako huongoza utendaji wa mwili wako. Ubongo hukuwezesha kujifunza mambo mapya, hata lugha mpya, nao huhifadhi na kukumbuka matukio ya maisha yako. Tena mtaalamu wa mfumo wa neva James Bower akiri hivi: “Hatujui kwa uhakika ubongo ni chombo cha aina gani.” Mwanasayansi wa mfumo wa neva Richard F. Thompson akubaliana na jambo hilo: “Bado kuna mambo mengi sana ya kujifunza kuliko yale tunayoyajua sasa.” Upendezi wa kufumbua fumbo la ubongo ni mkubwa sana hivi kwamba Bunge la Marekani lilitangaza miaka ya 1990 kuwa Mwongo wa Ubongo.

Kuchunguza Ubongo Wako

Mikunjokunjo ya utando wa bongo kubwa au utando wa nje wa ubongo, ndiyo inayotokeza zaidi. (Ona mchoro ulio kwenye ukurasa wa 4 na sanduku kwenye ukurasa wa 8.) Utando huo uliokunjamana na wenye unene wa milimeta kadhaa na ambao una rangi ya kijivu na waridi una asilimia 75 hivi za chembe zote za neva za ubongo ambazo ni kati ya bilioni 10 hadi bilioni 100. Lakini wanasayansi fulani wanasema kwamba hata chembe hizo zote za neva hazisababishi ule utata wa ubongo.

Chembe nyingi za neva zina kitu kirefu kama mkia kinachoitwa aksoni. Nyuzi nyingine ndogondogo zinazotoka kwenye chembe ya neva zinaitwa dendira, ambazo hufanana na matawi ya mti unaochipuka. Nyuzi hizo hufanyiza maelfu ya miunganisho kati ya chembe ya kawaida ya neva na chembe nyinginezo za neva. Chembe za neva hata huwa hazigusani. Kwenye pengo lililoko katikati ya chembe hizo, linaloitwa sinapsi, kemikali ndogondogo huvuka, jambo linaloongezea hata utata zaidi wa ubongo.

“Miunganisho ya aina mbalimbali ya sinapsi” katika ubongo wako “yaweza kuwa mingi kuliko idadi ya atomu zinazofanyiza ulimwengu ujulikanao,” ndivyo anavyokadiria mtaalamu mmoja.

Ijapokuwa utando wa bongo kubwa uliojaa chembe za neva ndiyo sehemu ya ubongo ijulikanayo zaidi, namna gani zile sehemu ambazo ziko chini ya utando huo? Kwa mfano, lile eneo linaloitwa corpus callosum ni kiunganishi muhimu kati ya ubongo wa kushoto na ubongo wa kulia. Karibu na hapo pana thalamus (linalotokana na neno la Kigiriki linalomaanisha chumba cha ndani), eneo ambalo hupitisha nyingi za habari ambazo ubongo wako hupokea; hypothalamus (neno la Kigiriki linalomaanisha chini ya chumba cha ndani) linaloshirikiana nalo, ambalo husaidia kudhibiti msongo wa damu na joto ya mwili; na kitu kingine kidogo kinachoitwa tezi pituitari. Tezi hiyo bora hudhibiti mwili wako kwa kuachilia kemikali zinazoitwa homoni, ambazo hudhibiti kemikali nyingine zote zinazotokezwa na matezi ya mwili. Kisha kuna pons, ambayo hushughulikia habari zinazohusu miendo yako, na medula, ambayo hudhibiti upumuaji wako, mzunguko, mapigo ya moyo, na umeng’enyaji wa chakula. Viungo hivyo hufanya hayo yote bila hata wewe mwenyewe kujua kwamba viko!

Ubongo unafanyaje kazi ukiwa na sehemu tofauti-tofauti hivyo? Na unaweza kutumiaje ubongo wako kwa njia bora? Makala mbili zifuatazo zataja mambo yawezayo kuwa majibu.

[Sanduku katika ukurasa wa 4]

Sababu Inayofanya Tusihitaji Kichwa Kikubwa Zaidi

“Kama utando wa bongo kubwa haungekuwa na mikunjokunjo, ubongo ungekaribia kutoshana na mpira wa mchezo wa vikapu, badala ya kutoshana na ngumi mbili zilizokunjwa pamoja.”—Profesa Susan A. Greenfield

[Mchoro katika ukurasa wa 4, 5]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

SEHEMU FULANI ZA UBONGOSEHEMU ZA NDANI

Imechorwa kulingana na ukubwa wake halisi

Utando wa bongo kubwa

Utando mwembamba wa nje wa kila sehemu ya bongo

Bongo kubwa

Ni sehemu kubwa ya mviringo ya ubongo. Inachukua sehemu kubwa ya fuvu

“Visual cortex”

Ubongo wa kisogoni

“Ubongo mdogo.” Huo unapatikana katika sehemu ya chini, nyuma ya ubongo wote

“Pons”

Medula

SEHEMU ZA NDANI

“Corpus callosum”

Tita la nyuzi za neva linalounganisha ubongo

“Thalamus”

“Hypothalamus”

Hudhibiti utendaji wa hiari wa mwili

Tezi pituitari

Picha zimeandaliwa na]

Kwa kutegemea The Human Mind Explained, cha Profesa Susan A. Greenfield, 1996

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki