Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 6/8 uku. 31
  • Kuzuia Moto Nyumbani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuzuia Moto Nyumbani
  • Amkeni!—1992
  • Habari Zinazolingana
  • Faida na Hasara za Moto
    Amkeni!—2002
  • Moto! Je, Utatumia Kizima-Moto Kipi?
    Amkeni!—2001
  • Wakati Moto Utishapo Umati
    Amkeni!—1990
  • Moto Ukosapo Kudhibitiwa
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 6/8 uku. 31

Kuzuia Moto Nyumbani

KAMA vile hadithi hiyo isimuliwavyo, ng’ombe wa Bi. Patrick O’Leary alipiga teke taa ya mafuta-taa katika ghala ya nafaka na kuanzisha moto mkubwa sana wa Chicago katika 1871. Gharama ya mali iliyoharibika na uhai ilikuwa yenye kushtua sana. Kulingana na chanzo kimoja, moto huo uliacha watu 100,000 bila makao, ukaharibu majengo zaidi ya 17,400, na ukauwa watu 250.

Leo, miaka 120 baadaye, teknolojia ya ki-siku-hizi ya kupambana na moto imesaidia kuzuia mweneo mkubwa wa moto. Hata hivyo, moto wa nyumbani unazidi kuwa tisho lenye hatari. Shirika la Kitaifa la Ulinzi wa Moto liitwalo NFPA (National Fire Protection Association) ladai kwamba katika United States, karibu watu elfu tano waliuwawa na moto wa nyumbani katika mwaka mmoja. Kama ilivyorekodiwa katika The Vancouver Sun, NFPA ilitoa madokezo machache ya kusaidia kuzuia moto wa nyumbani. Ni haya:

◻Usiruhusu uvutaji tumbaku nyumbani. Aksidenti za wavutaji ovyoovyo zinaendelea kuwa visababishi vyenye kuongoza vya vifo vya moto nyumbani

◻Usiache vipasha-moto vinavyobebeka vifanye kazi bila mtu wa kuviangalia au ulalapo.

◻Epuka kurundika plagi nyingi kwenye vitundu vya umeme au kutumia kamba zilizochakaa. Tumia tu kipimo kilicho sawa cha fataki.

◻Weka mahali pa moto na bomba la kutokea moshi pakiwa safi.

◻Angalia vigundua moshi kwa ukawada, na ubadilishe betri kila mwaka. Hakikisha kwamba kila mmoja katika familia anatambua sauti ya kigundua moshi.

◻Hakikisha kwamba wote katika familia wanajua njia ya kuepuka moto, na mweke mahali pa kutokea pakiwa wazi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki