Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 10/8 uku. 31
  • Moto Ukosapo Kudhibitiwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Moto Ukosapo Kudhibitiwa
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Faida na Hasara za Moto
    Amkeni!—2002
  • Moto! Je, Utatumia Kizima-Moto Kipi?
    Amkeni!—2001
  • Kuzuia Moto Nyumbani
    Amkeni!—1992
  • Wakati Moto Utishapo Umati
    Amkeni!—1990
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 10/8 uku. 31

Moto Ukosapo Kudhibitiwa

Na mleta habari za Amkeni! kutoka Ghana

MOTO. Unapodhibitiwa, ni mtumishi wa maana. Lakini unapowaka bila kudhibitiwa, unaweza kuwa jitu lenye kuharibu linalomeza kila kitu njiani mwalo—mwanadamu, mnyama, miti, mimea.

Katika 1983 moto wa kichaka katika Australia uliharibu majimbo ya Australia Kusini na Viktoria. Zaidi ya watu 70 waliuawa, kutia na kuangamizwa kwa ng’ombe 36,000, kondoo 320,000, na zaidi ya makao 2,000.

Mwaka uo huo, mioto ya vichaka katika Ghana iliharibu asilimia 72 ya kilometa za mraba 238,000 za nchi hiyo. Watu angalau 29 walikufa; wengine 34 walijeruhiwa.

Kiasi kidogo cha mioto ya vichaka husababishwa na mambo ya asili, kama vile umeme. Mingi yayo husababishwa na mwanadamu. Katika Ghana kisababishi kikuu cha mioto ya vichaka ni kugema tembo ya mnazi. Wafanyakazi huwasha moto vibunda vya kuni ili kutia joto minazi, ikifanya utomvu wa minazi utoke. Hata hivyo, mara nyingi moto huo huenea kwa aksidenti, na moto wa vichaka unatokea.

Katika nchi fulani za Afrika, ni kawaida kwa kikundi cha wawindaji kuzunguka kichaka na kukiwasha moto ili kutoa wanyama ambao huenda wakawa ndani yacho. Wale wanaotafuta asali ya nyuki wa mwituni hutumia moto ili kuwafukuza nyuki kutoka kwenye mizinga yao. Nyakati nyingine wao hawachukui hatua ya kuzima mioto wanayowasha.

Katika Afrika ya tropiki, wakulima wengi hutumia njia za ukulima za kufyeka na kuchoma. Wao hufyeka kichaka katika eneo moja wanalokusudia kulima na kuchoma kile kinachobaki. Ukikosa kudhibitiwa, moto huo waweza kuenea haraka.

Katika maeneo fulani, wachungaji huchoma nyasi zilizokauka kwa kuamini kwamba, wakati msimu wa mvua ujapo, nchi itahuishwa tena, na kutakuwa na malisho bora kwa wanyama wao. Mioto hiyo inapoachwa ijizime yenyewe—kama inavyotukia mara nyingi—yaweza kuenea kwa urahisi. Wapiga kambi na wafanyakazi wa nje pia huwa na hatia nyakati nyingine kwa kuwasha mioto na kukosa kuizima.

Basi, ni wazi kwamba kutojali ndiko kunakosababisha mioto mingi ya vichaka. Hata hivyo, je, kuna njia yoyote ya kuzuia mioto ya aina hiyo isitukie kamwe? Tahadhari za busara zaweza kuleta tofauti kubwa. Kwa kielelezo, kwa kuweka kizuia moto chenye upana wa meta 5 hadi 10 kuzunguka moto wowote uliowashwa kondeni, unaweza kukomesha mweneo wa moto kwa mashamba ya karibu. Kuzima kabisa mioto yote ambayo umewasha ni ulinzi mwingine wa maana. Kumbuka, kuzuia moto wa kichaka ni rahisi zaidi ya kupambana nao.

Watu fulani huamini kwamba kama wakosaji wangepewa adhabu kali zaidi, hilo lingezuia kutojali na matendo ya uchomaji kimakusudi. Wengine hutoa sababu kwamba njia bora zaidi ya kuzuia mioto ya vichaka ni elimu na nia ya ushirikiano wa wote.

Shughulika na moto kwa staha ifaayo. Kwa kuwa na tahadhari ya kiasi, tunaweza kuepuka kuchokoza mtumishi huyo muhimu ili asiwe jitu lenye kuharibu.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

P. Riviere/Gamma Liaison

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki