Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 9/8 uku. 30
  • Juma Lenye Matukio ya Maana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Juma Lenye Matukio ya Maana
  • Amkeni!—1992
  • Habari Zinazolingana
  • Maskini Kimwili Lakini Tajiri Kiroho
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Kuwezana na Mchafuko wa Bahari ya Ainabinadamu Wasiotulia
    1992 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
  • Vijia vya Chini ya Ardhi vya Odessa
    Amkeni!—2010
  • Ripota wa Kiev Asifu Mashahidi
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 9/8 uku. 30

Juma Lenye Matukio ya Maana

ULIMWENGU ulishtuliwa Jumatatu, Agosti 19, 1991, wakati viongozi wa mapinduzi walipochukua mamlaka katika Urusi, na Rais Mikhail Gorbachev akafungiwa nyumbani katika Krimea. Kilometa chache kutoka hapo, katika Odessa yenye uzuri, matayarisho ya mwisho ya mkusanyiko wa Mashahidi wa Yehova ambao ungefanywa mwisho-juma huo katika jiji hilo, yalikuwa yanafanywa. Kwa kusikitisha, mkusanyiko wa Odessa ulifutiliwa mbali na maofisa wa hapo.

Walakini, Mashahidi hawakuzimia roho. Waliendelea na matayarisho yao ya kabla ya mkusanyiko na kumwomba ofisa mmoja wa jiji afanye yote awezayo ili wapate ruhusa. Wawakilishi wa Mashahidi wa Yehova waliambiwa warudi Alhamisi, Agosti 22. Alasiri hiyo, baada ya mkutano wa baraza la jiji, Mashahidi walipewa ruhusa kwa hati iliyoandikwa ili wafanye mkusanyiko na wakatakiwa mema. Katika Moscow, viongozi wa mapinduzi walikuwa wamelazimika kujisalimisha siku hiyo hiyo!

Jinsi hayo yote yalivyotukia upesi! Na ilikuwa ajabu jinsi gani kuona zaidi ya watu 12,000 wamehudhuria mwisho-juma huo! Mnamo Agosti 27, siku mbili baada ya mkusanyiko wa Odessa, wawakilishi wa Mashahidi wa Yehova walimwona Bw. V. K. Simonenko, mwenyekiti wa Halmashauri ya Utekelezi ya Jiji la Odessa, na wakamshukuru kwa kuruhusu mkusanyiko huo ufanywe, na wakampa nakala ya kitabu kipya Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi katika lugha ya Kirusi.

Bw. Simonenko alishukuru kwa ajili ya zawadi hiyo na kusema: “Mimi sikuwapo kwenye mkusanyiko, lakini ninajua yote yaliyotukia humo. Tangu mwanzo wenyewe wa Odessa, sijapata kuona kitu kingine bora kuliko hiki . . . Ninawaahidi kwamba wakati wowote mtakapohitaji ruhusa ya kufanya mikutano yenu, nitakuwa tayari kutoa ruhusa.”

[Chati katika ukurasa wa 30]

MIKUSANYIKO YA URUSI KATIKA 1991

Tarehe Jiji Kilele cha Waliobatizwa

Hudhurio

Julai 13, 14 Tallinn, Estonia 4,808 447

Julai 20, 21 Usolye-Sibirskoye, 4,205 543

Siberia

Agosti 2, 3 Kiev, Ukraine 14,654 1,843

Agosti 3, 4 Lvov, Ukraine 17,531 1,316

Agosti 24, 25 Odessa, Ukraine 12,115 1,943

Agosti 31– Chernovtsy, 14,137 1,126

Septemba 1 Ukraine

Septemba 7, 8 Alma-Ata, 6,802 602

Kazakhstan

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki