Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 2/22 uku. 24
  • Ripota wa Kiev Asifu Mashahidi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ripota wa Kiev Asifu Mashahidi
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Muungano Unaostaajabisha Ulimwengu
    Amkeni!—1993
  • Walishangaa kwa Yale Waliyoona
    Amkeni!—1992
  • Mikusanyiko Uthibitisho wa Udugu Wetu
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
  • Je, Ulimwengu Utaungana?
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 2/22 uku. 24

Ripota wa Kiev Asifu Mashahidi

OLEKSA KURPAS alisifu sana mkusanyiko uliofanywa na Mashahidi wa Yehova katika Kiev, Ukrainia, Agosti 5 hadi 8, 1993. Aliandika hivi katika gazeti la Kiev Democratic Ukraine katika Agosti 10:

“Stediamu ya Republican haijakuwa na hudhurio kama hilo kwa muda mrefu . . . Ebu wazia watu 64,000 (miongoni mwao maelfu ya wageni) wanaokaa katika hoteli, wanaozuru maduka, wanaosafiri kwa magari ya umma. . . . Mkutano huo wa Mashahidi wa Yehova ulikuwa wa hali ya juu sana. Wasemaji waliokuwa wakitoa hotuba walipigiwa makofi sana (kama zile siku za zamani), na machozi yakanitiririka.

“Si watu wote wanaojua dini hii. Tofauti na dini ya Waorthodoksi, Mashahidi wa Yehova waamini kwamba Yesu Kristo alikuwa Mwana wa Mungu tu, na kwamba roho takatifu ni kani au nguvu ya Mungu, (yaani, hawakubali muungano wa hao watatu katika Utatu Mtakatifu). Wanafundisha kwamba hakuna helo. Baada ya hukumu yenye kuogofya, ulimwengu utageuzwa kuwa paradiso, ambamo watu waadilifu wataishi na wenye dhambi kufa. Waumini wa dini hiyo huweka uangalifu mkubwa kwa familia yao. Hicho ni kitu kitakatifu, msingi halisi wa mambo, kitu kilicho bora zaidi na chenye uchangamfu zaidi ulimwenguni. Wana mtazamo wenye urafiki sana kuelekea ndugu na dada zao (na jambo lenye kutokeza hata zaidi—hata kwa watu wa dini nyingine). Sijapata kuona jambo kama hilo. . . .

“Jambo lenye kupendeza zaidi lilitendeka siku ya Jumamosi, Agosti 7. Siku hiyo katika Mkusanyiko wa Kimataifa wa Mashahidi wa Yehova, idadi kubwa ya watu isiyo na kifani walibatizwa, yaani, 7,402. Kwa ajili ya tukio hilo lisilo la kawaida na lenye umaana sana, vidimbwi vikubwa sita viwezavyo kutunguliwa viliwekwa katika sehemu za mashindano ya mbio ya Stediamu hiyo. Watu 60 waliokomaa kiroho walibatiza kwa kutumbukiza majini wahubiri wapya wa habari njema. Sherehe yote nzima ilichukua muda wa saa 2 na dakika 15. . . .

“Wafuasi hao wapya walipita wakitoka sehemu tano katika stediamu na kupigiwa makofi na wale Mashahidi wa Yehova waliokuwa wakihudhuria mkusanyiko. Idadi ya wale waliobatizwa katika Kiev ilivunja rekodi ya awali iliyowekwa katika 1958 [ya 7,136], katika mkusanyiko wa kimataifa katika New York. Kwa ujumla, Mashahidi wa Yehova wakiwa na tengenezo lenye kufanya kazi vizuri hivyo, kwa hakika, hivi karibuni dini hii itapata nafsi wengi wa Orthodoksi ambao wamekuwa katika dini hiyo kwa muda mrefu.

“Naomba radhi kwa viongozi wa dini mbalimbali, lakini wasipoacha magomvi hayo yao ya kiupuzi miongoni mwao wenyewe, watapoteza mamia ya maelfu ya watu wa kidini. Mkusanyiko huu ulionyesha kwamba inawezekana kwelikweli kupata amani na umoja miongoni mwa watu wa jamii tofauti-tofauti na wa kutoka nchi mbalimbali.”[1]

[Picha katika ukurasa wa 24]

Baadhi ya wale 7,402 waliobatizwa katika mkusanyiko wa Kiev, Ukrainia

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki