Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 1/22 uku. 31
  • Mto wa Barafu wa Arjentina Usio na Kifani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mto wa Barafu wa Arjentina Usio na Kifani
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Kufanya Bara Kame Litoe Mazao
    Amkeni!—2001
  • Kuvua Samaki Kwenye Barafu
    Amkeni!—2004
  • Majumba Yenye Kumetameta ya Baharini
    Amkeni!—1995
  • Antaktika Bara Lililo Hatarini
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 1/22 uku. 31

Mto wa Barafu wa Arjentina Usio na Kifani

“Lazima uende ukauone.” “Ni mojapo maajabu ya ulimwengu.” Tulikuwa tumetumwa Buenos Aires kusaidia kujenga vifaa vipya kwa ajili ya tawi la Watch Tower Society, lakini ni kitia-moyo kama hicho kilichosukuma mume wangu nami tusafiri kwenda National Park of Glaciers kusini mwa Arjentina ili kuona mto wa barafu usio na kifani uitwao Perito Moreno.

Hatimaye tukawasili kwenye Milima Andes, miinuko yao ya chini ilikuwa imefunikwa na miti. Barabara ilikuwa ikiendelea kandokando ya mkono wa Riko wa Ziwa Arjentino. Upesi tukafika mwisho wa peninsula ambapo njia ya maji hupindika kuingia ndani ya ziwa. Katikati ya mfereji ukatokea Perito Moreno wenye kuvutia—Ukuta wa theluji wa upana wa kilometa zaidi ya nne na kimo cha meta zaidi ya 50. Waonekana kuvutia kama nini!

Mto huu wa barafu, Perito Moreno, waweza kusonga mbele kwa kadiri ya meta 4 kwa siku au meta 450 kwa mwaka! Hatungeweza kujizuia kupiga picha jua lilipokuwa likimeremeta juu ya chembe za buluu. Kwa nini buluu? Kwa sababu ya uzani wa barafu, hakuna hewa inayobaki katika chembe cha barafu, hivyo mto huo wa barafu huwa na rangi ya kibuluu yenye kuona ndani. Jambo jingine lililonasa uangalifu wetu ni sauti zisizo za kawaida. Tulikuwa tukisikia mngurumo wa kilometa za mraba 195 za mto huo wa barafu ukiteremka polepole bondeni na sauti ya kuvunjika kwa vipande vikubwa vya barafu vikivunjika kutoka kwenye uso wa mto huo wa barafu. Vipande hivyo vilipiga maji kwa sauti kama ya ngurumo.

Kila miaka michache kusonga mbele kwa Perito Moreno huziba njia ya asili ya mkono wa Riko ya kuingiza maji yao ndani ya Ziwa Arjentino. Kwenye upande mmoja, maji hayo yaliyozuiwa huinuka juu kuanzia meta 20 hadi 35 kupita usawa wayo wa asili. Hatimaye, msongo wa maji hushinda barafu nguvu, nao Perito Moreno hutokeza tamasha yenye kustaajabisha maji hayo yabubujikapo.

Yale maji matulivu ya ziwa hugeuzwa kuwa bahari yenye kuchafuka. Hilo huendelea kwa saa nyingi. “Vipande vikubwa mno vya barafu, vikubwa zaidi ya jengo la orofa 15 huvunjika kutoka kwenye ukuta wa mto wa barafu na kuanguka kwa kishindo chenye kuziba masikio,” yafafanua maelezo ya habari ya televisheni La Cuerra Del Hielo. “Kila mtu hupiga makelele na kuruka-ruka, akifuatana na uthibitisho huu usiosadikika wa nguvu za asili.”

Tulikuwa na furaha kama nini kwamba marafiki wetu walituhimiza tuje tuone Perito Moreno!—Imechangwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki