Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 2/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Yabisi-kavu Ni Ugonjwa Unaolemaza
    Amkeni!—2001
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2002
  • Tumaini kwa Wale Wanaougua Yabisi-Kavu
    Amkeni!—2001
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2002
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 2/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Ulimwengu Wote Mzima Ni lazima niseme asanteni sana kwa ajili ya ile habari yenye kuduwaza akili katika ule mfululizo “Kufungua Siri za Ulimwengu Wote Mzima.” (Machi 22, 1992, Kiingereza) Lakini ni kwa mamlaka gani tunasema kwamba nyota kubwa nyekundu, pulsa, na mashimo meusi ni hatua katika maisha [na kifo] cha nyota? Isaya 40:26 inasema habari ya nyota kwamba “hapana moja isipokuwapo mahali pake.”

E. W., Sierra Leone

Andiko hilo la Biblia halizungumzi juu ya kama nyota zina mwisho wenye msiba. Badala ya hivyo, linakazia ujuzi na hekima isiyochunguzika ya Mungu. Akiwa Muumba, Mungu ajua hali ya kila nyota moja moja. Hapana ‘zisizokuwapo mahali pazo’ kwa kadiri anavyohusika. (Ona “Mnara wa Mlinzi” wa Septemba 15, 1989, ukurasa 31—Mhariri.

Mapenzi ya Utineja Asanteni sana kwa ajili ya makala “Vijana Wanauliza . . . “Kusemezana Kuna Ubaya Gani?” (Agosti 22, 1992, Kiingereza) Tumekuwa tukiandikiana barua na mvulana mmoja katika kundi letu. Pia tulikuwa tukiongea kwa simu. Hata hivyo, kwa kuwa hakuna yeyote kati yetu aliyekuwa na umri wa kutosha kufunga ndoa, tulikuwa tayari tumeamua kuacha kutumia wakati mwingi kadiri hiyo tukisemezana. Ilinifanya nifurahi kuona katika maandishi kwamba tulikuwa tumefanya uamuzi ufaao.

M. N., Japani

Ilikuwa kana kwamba mlikuwa mmesoma akili yangu! Nilikuwa nimefikiria kwa uzito kuandikiana na wavulana fulani. Nadhani nilikuwa nimejidanganya kufikiria kwamba barua hizo zingekuwa za kuwatia moyo tu. Makala yenu ilifika wakati barabara.

D. B., United States

Nina miaka 12 nami huandikia watu wengi barua. Mmoja wao ni mvulana. Sikudhani kamwe kwamba nina hisia za kimapenzi kwake, lakini siku moja alianiandikia akasema kwamba ananipenda! Makala yenu ilikuja wakati barabara!

E. V., United States

Yabisi Makala yenu “Kujifunza Kuishi Ukiwa na Yabisi (Juni 8, 1992, Kiingereza) ilisomwa kwa upendezi mwingi. Lakini kwa kuwa mimi ni mgonjwa wa yabisi, nilihisi kwamba haikuonyesha kabisa uharibifu ambao ugonjwa huo waweza kusababisha kupitia matokeo mbalimbali: Mkazo, maumivu, uchovu, matatizo ya kupata usingizi, na kushuka moyo. Mlionyesha picha ya mikono iliyolemaa kana kwamba hiyo ndiyo namna mbaya zaidi ya yabisi. Ulemavu wenye kuonekana sio jambo tu tulazimikalo kushughulika nalo. Uvurungu wangu wa mbavu wa kulia umeshuka chini ndani ya mfupa wangu wa nyonga ya kulia, na kwa sababu hakuna mtu anayeweza kuona ulemavu huo, watu hawaukubali. Makala yenu ilitutia moyo “tusitawishe maoni mazuri,” lakini nyakati nyingine ni vigumu kufanya hivyo bila kuungwa mkono na wengine.

M. J., United States

Twathamini maelezo hayo ya kweli. Makala yetu fupi kwa kweli haikuzungumzia mengi. Zaidi ya hilo, ilielekezwa sana-sana kwa wagonjwa wa yabisi wenyewe, wajuao vema matokeo ya ugonjwa huo. Ingawa hivyo, twakubali kwamba marafiki na washiriki wa familia wangefanya vema kujua matokeo yenye kuharibu ya yabisi na wapaswa kujitahidi kuwa wenye msaada na wenye kuunga mkono.—Mhariri.

Asanteni sana kwa kuchapisha makala hiyo. Mimi nina miaka 31 na husumbuliwa sana na maumivu makali ya yabisi. Uchovu umetokeza kushuka moyo, huzuni, na kukatishwa tamaa. Hata hivyo ninaiweza hali kwa sababu mimi hufurahia afya ya kiroho iliyo ya thamani kubwa kwangu.

T. R., United States

Nimekuwa nikingojea mzungumzie habari hii kwa muda fulani, nami nilifurahi sana kuisoma. Nimekuwa nikivumilia maumivu ya yabisi baridi tangu nilipokuwa na miaka tisa. Ujapokuwa uhakika wa kwamba nyakati nyingine mimi huwa miongoni mwa wengine wasioelewa kabisa matatizo yetu, Yehova huonyesha kupendezwa kwake na hututia moyo kupitia makala kama hiyo.

P. C., Italia.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki