Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 2/22 kur. 10-12
  • Wakaguzi wa Usafi wa Angani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wakaguzi wa Usafi wa Angani
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Ukaguzi wa Usafi
  • Doria wa Njia za Angani
  • Uwezo wa Kuona na Ushirikiano
  • Kurudi kwa Tai-Mzoga Mkuu
  • Kuwatazama Ndege—Je, Kwavutia Kila Mtu?
    Amkeni!—1998
  • Tai Ndege-Wanofua-Mizoga
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Mbuga ya Kipekee ya Wanyama wa Mediterania
    Amkeni!—2002
  • Kongoti Ndege Anayeeleweka Vibaya
    Amkeni!—2001
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 2/22 kur. 10-12

Wakaguzi wa Usafi wa Angani

Wakiulizwa wataje ndege ambaye hawangetaka kukutana naye hata kidogo, watu wengi wangesema tai-mzoga.

Hakuna ndege wengi ambao wamesutwa kama tai-mzoga. Ndiye ndege mlaniwa ambaye kivuli chake kibaya huzungukazunguka juu ya wafu na wanaokufa. Kuonekana kwake husemekana kuwa huashiria machinjo, ukiwa, na kukata tamaa. Lakini hayo ni mambo ya ngano tu.

Kwa habari ya mambo ya hakika: Watu wengi wamesisimuliwa na uzuri wa tai-mzoga anaporuka na ile njia yenye huruma atumiayo kutunza vifaranga wake. Pia wametambua fungu lake la maana la kimazingira. Hao humuona tai-mzoga kuwa mwenye fahari na pia wa muhimu sana.

Inakubalika, tai-mzoga wana tabia kadhaa zisizopendeza, licha ya mazoea yao ya ulaji yasiyopendeza. Hakika hawana sura yenye kuvutia, na sauti zao zimeelezwa kwa njia mbalimbali kuwa vilio vyembamba, miteto, miguno, mikoromo, na vilio kama vya nyoka. Hata hivyo, wana sifa zinazowapendekeza.

Tai-mzoga ni ndege ambaye huchukua kwa uzito sana uzazi wake. Kila mwaka “mtoto wa pekee” hupokea utunzaji usiogawanyika wa wazazi wote wawili mpaka aweze kujitunza. Kifaranga mchanga wa tai-mzoga anayekaa akiwa hoi kwa miezi kadhaa juu ya ukingo usiofikilika hakika huhitaji utunzaji wa huruma wa wazazi wote wawili. Kwa kweli, kifaranga mchanga wa tai-mzoga wa Andes lazima alishwe kwa miezi sita kabla ya kuweza kukiacha kioto, kufikia wakati huo “kifaranga” amekua akakaribia kuwa ndege mzima.

Na tai-mzoga wana sifa njema ya kuwa wenye mafaa sana. Ingawa ndege wengi hufaidi ainabinadamu kwa njia moja au nyingine, tai-mzoga hufanya utumishi usio na kifani. Ni wakaguzi wa usafi wa angani.

Ukaguzi wa Usafi

Kuondolea mbali mizoga kila siku si kazi ambayo ingependwa na watu wengi, lakini ni kazi ya maana. Usafi ufaao hutaka kuondolewa mbali kwa mara hiyo kwa miili mifu, iwezayo kuwa vyanzo hatari vya maradhi yenye kuambukia binadamu na mnyama.

Hapo tai-mzoga watambuliwa. Hata nyama yenye viini vya anthraksi au botulini humezwa bila hofu ya kudhuriwa, mpaka kisibakie chochote ila mifupa.

Baadhi ya tai-mzoga hata hufanya kula mifupa kuwa kazi yao ya pekee. Yule tai-mzoga lammergeier wa Ulaya/Esia na Afrika huangusha mifupa kwenye miamba kutoka kimo cha juu. Mifupa ipasukapo, lammergeier hula uboho na vile vipande vidogo vya mfupa.

Kwa tukio zuri, tofauti na wenzao binadamu, wakaguzi hao wa usafi hawajapata kamwe kugoma. Kama kazi ya tai-mzoga ingeachwa bila kufanywa nyanda za tropiki zenye kujaa mizoga inayojaa maradhi ni jambo ambalo lingeonekana mara nyingi sana.

Lakini acheni tufuate kikundi cha tai-mzoga katika siku ya kawaida ya kazi.

Doria wa Njia za Angani

Upesi baada ya jua kuchomoza, tai-mzoga hupaa angani, kila mmoja akashike doria katika eneo fulani. Siku kutwa kikosi chetu cha tai-mzoga hushika doria angani bila kuchoka wakitafuta-tafuta wanyama wafu. Hatimaye wakati mzoga uonwapo na mmoja wao, yeye hupiga mbizi ya ghafula. Hilo huvuta uangalifu wa wale ndege wengine, ambao pia huharakisha kwenda kwenye mzoga huo. Katika muda wa dakika chache, ndege wengi wawasili mahali hapo.

Kabla ya kula, ndege hao hurukaruka kuzunguka mzoga kwa kusitasita. Ijapokuwa sifa yao, wao ni wenye haya kupita kiasi. Hatimaye, mmoja wao huanza kunyafua mzoga, na hiyo ndiyo ishara kwa kikundi chote kishambulie mlo huo. Kuna kuzozana na kulia, kusukumana na kuburutana kwingi, ambako huonekana sana kama mng’ang’ano wa wacheza mpira wa raga. Wenye njaa zaidi, ambao huteta kwa nguvu zaidi kwa kawaida ndio hujilisha kwanza. Ikiwa mzoga ni mkubwa, kutakuwako chakula cha kuwatosha wote.

Kwa muda wa dakika chache, mlo waisha, na wakiacha mifupa tu, kundi hilo lapaa kuelekea angani likaendelee na kazi yao ya kutafuta-tafuta. Maisha ya tai-mzoga si rahisi. Huenda ikachukua siku mbili au tatu kabla ya kupata mlo mwingine.

Uwezo wa Kuona na Ushirikiano

Tai-mzoga wameumbwa vizuri sana kwa ajili ya ukaguzi wa kutoka angani. Mabawa yao makubwa yamebuniwa yafae vizuri sana kwa ajili ya kunyiririka na kupaa, yakiwawezesha kuruka kwa saa nyingi kwa kupiga mabawa kidogo tu. Ni wastadi sana katika kujinufaisha na mikondo ya hewa yenye joto yenye kupaa, ambayo huwasaidia kuendelea kuelea bila jitihada kubwa. Dean Amadon, mwornitholojia (mtaalamu wa ndege) mashuhuri Mwamerika, aliwasimulia kuwa mojapo “wonyesho uonekanao wazi zaidi wa uwezo wa kuruka wa asilia.”

Swali moja lililowatatiza waornitholojia kwa miaka mingi ni, tai-mzoga hupataje mizoga kwa haraka sana?

Jibu likaonekana kuwa muunganisho wa uwezo mkubwa sana wa kuona na ushirikiano. Imehesabiwa kwamba tai-mzoga anayezunguka juu kwenye kimo cha meta zapata 750 aweza kuona kitu ardhini chenye urefu unaopungua sentimeta 13. Lakini hata kwa uwezo mkubwa sana wa kuona kama huo, ingekuwa vigumu sana kwa tai-mzoga aliye peke yake kupata chakula.

Kwa hiyo, ushirikiano ni wa muhimu. Imeonwa kwamba tai-mzoga hujigawanya wakashike doria katika maeneo mbalimbali. Tai-mzoga mmoja akishuka kuelekea mzoga, mruko wake wa ghafula kuelekea chini wenye kupambanulika ndio ishara kwa ndege walio karibu kwamba chakula kinakaribia kupatikana, nao huruka mara hiyo kuelekea upande huo. Vilevile badiliko la mwendo wao linaonwa na ndege walio mbali zaidi, ambao pia huharakisha kwenda mahali hapo. Mfumo wa angani wa kuwasiliana kutoka mbali ni wenye matokeo kwa njia yenye kushangaza sana, sana hivi kwamba kwa mtazamaji yaweza kuonekana kama ndege wote wanawasili karibu kwa wakati uleule mmoja.

Kwa kuhuzunisha, uwezo wao wa kufanya kazi kwa matokeo na utumikaji wao wenye kufaa usioweza kukanwa haukutosha kuhakikishia tai-mzoga ulinzi na kuokoka kwao.

Kurudi kwa Tai-Mzoga Mkuu

Wajapohesabiwa kuwa kati ya ndege wanyafua mizoga wakubwa zaidi na wenye kuvutia zaidi, tai-mzoga wamo katika hatari ya kumalizika katika sehemu nyingi za ulimwengu. Chakula chao cha kawaida kimetoweka kutoka kwenye nyanda, na mara nyingi mizoga wanayopata imetiwa sumu. Kiwango chao cha kuzaa kilicho cha polepole hufanya pia iwe vigumu hesabu yao ndogo kuweza kuongezeka.

Hata hivyo, kuna mafanikio fulani yenye kutia moyo. Programu ya kufuga tai-mzoga mkuu wa Kalifornia kwa njia isiyo ya asili inaonekana kuwa ikifanikiwa, na inatumainiwa kwamba ndege wengi zaidi waweza kurudishwa upesi mwituni. Kwa sababu ya jitihada za wahifadhi Wafaransa, tai-mzoga wa griffoni amerudi tena katika Massif Central, Ufaransa, baada ya kukosekana kwa miaka mingi.

Hivyo, ndege ambaye wakati mmoja watu walipenda kuchukia amekuwa ishara ya jitihada za mwanadamu za kuokoa jamii hiyo ambayo yeye amehatarisha. Bila shaka, mruko wa fahari wa tai-mzoga-mkuu juu ya milima sierra ya Amerika Kaskazini na Kusini ni mwono usioweza kuruhusiwa utoweke.

Wakati uo huo, katika Afrika na Esia, tai-mzoga bado hufanya kazi yao kwa unyenyekevu bila kupata shukrani, ile ya kuwa wakaguzi wa usafi wa angani.

[Sanduku katika ukurasa wa 12]

Rekodi ya Tai-Mzoga

TAI-MZOGA wanahesabiwa kuwa miongoni mwa ndege walio wachache zaidi na walio wakubwa zaidi ulimwenguni. Na pia wameweka rekodi ya kuruka juu zaidi angani.

Tai-mzoga mkuu wa Kalifornia ni mojapo jamii zilizo katika hatari kubwa zaidi ya kuangamia ulimwenguni. Ili kuokoa tai-mzoga huyo asiangamie, jitihada nyingi zinafanywa kupitia programu ya ufugaji miongoni mwa ndege zaidi ya ishirini na nne waliokamatwa. Katika 1986 ni tai-mzoga wakuu watatu tu wa California waliobaki mwituni.

Tai-mzoga mkuu wa Andes, pamoja na korongo wa Afrika, ana mweneo mkubwa zaidi wa mabawa kuliko ndege wote wa barani, wa mita 3. Pia yeye ndiye ndege mla mizoga aliye mzito zaidi, nyakati nyingine akiwa na uzito wa zaidi ya kilo 14.

Tai-mzoga ni warukaji wa kimo cha juu pia. Katika 1973 tai-mziga wa Afrika (Gyps rueppellii) aligongana na ndege ya abiria iliyokuwa ikiruka juu ya Côte d’Ivoire, Afrika Magharibi, kwenye kimo cha juu cha mita 37,000.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 10]

Picha kwa Hisani ya Hifadhi ya Madrid, Madrid, Hispania

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki