Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 3/8 uku. 31
  • Mrukaji-Ghafula Mwenye Ukimya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mrukaji-Ghafula Mwenye Ukimya
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Manyoya ya Bundi
    Amkeni!—2009
  • Bundi-Hudhurungi Aliye Kwenye Ukuta wa Hadrian
    Amkeni!—1995
  • Bawa la Bundi
    Je, Ni Kazi ya Ubuni?
  • “Mkazi wa Msituni Mwenye Kuvutia Kuliko Wote”
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 3/8 uku. 31

Mrukaji-Ghafula Mwenye Ukimya

IKIWA umepata kutembea vichakani usiku, huenda umekwisha sikia mlio wenye huzuni wa warukaji-ghafula wenye ukimya—bundi. Kwa kuwa kuna angalau aina 145 za bundi ulimwenguni pote, watu wengi waweza kumsikia bundi. Huenda ukampata bundi wa kawaida wa vibanda kotekote katika mabara ya Amerika, Ulaya, Afrika, na sehemu nyingi za Esia, kutia na Tasmania na sehemu nyinginezo za Australia. Ni nini hufanya bundi awe tofauti?

Kwanza kabisa, ni uso na macho yake. Umbo la uso hutofautiana katika aina hii na ile, lakini kwa kawaida ana “kichwa kikubwa, kipana na manyoya kama kisahani kidogo yaliyo kando ya macho yake. . . . Hayo hurudisha sauti kwenye matundu ya masikio ya bundi” (The World Book Encyclopedia) Tofauti na macho ya ndege wengi, macho ya bundi hutazama mbele; hawezi kuyasogeza katika matundu yayo. Hivyo, bundi hulazimika kusogeza vichwa vyao ili kutazama vitu vinavyosonga. Na wanaweza kugeuza vichwa vyao katika karibu duara kamili!

Jambo jingine lililo tofauti katika warukaji-ghafula hao wa usiku ni umbo lao la manyoya linalofanya waruke karibu bila sauti yoyote. Wanapoona mawindo yao kwa macho au kwa masikio makali, wanaweza kurukia-ghafula kwa ukimya mlo wao unaofuata. Wanasemwa kuwa “miongoni mwa ndege muhimu sana kwa wakulima” kwa sababu wao huangamiza wanyama aina ya panya ambao mara nyingi huharibu mimea.

Kitabu Book of North American Birds chasema: “Bundi ulimwenguni pote . . . wameonwa katika tamaduni zote kuwa ndege waleta bahati mbaya na kifo.” Mshairi Mwingereza wa karne ya 14 Geoffrey Chaucer alimwita bundi wa vibanda “nabii wa ole na bahati mbaya.” Biblia husema juu ya bundi katika mistari saba, kutia na rejezo la Isaya kwa nyumba za Babuloni zilizoharibiwa, ‘zilizojaa bundi.’—Isaya 13:21.

Bundi mkuu hula sana. Chanzo kimoja chasema: “Katika pindi chache, inasemekana kwamba ndege huyo hata huruka-ghafula na kushambulia watu wanaovaa kofia za manyoya, kwa wazi wakifikiri kofia hizo ni mawindo hai!” Ingawa alitangazwa kuwa ndege mchafu chini ya Sheria ya Musa, ubuni usio na kifani wa bundi huonyesha Muumbaji asiye na kifani.—Mambo ya Walawi 11:16, 17.

[Picha katika ukurasa wa 31]

Bundi mkuu—macho makali, masikio makali, na mrukaji wa ukimya

[Hisani]

Picha: Kwa Hisani ya Kituo cha Uhifadhi wa Wanyamapori cha Green Chimneys, Brewster, NY

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki