Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 4/8 kur. 3-5
  • Je! Sayansi Yaweza Kutatua Matatizo ya Karne ya 21?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Sayansi Yaweza Kutatua Matatizo ya Karne ya 21?
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Matatizo Si Machache
  • Kutafuta Njia za Kuwezana na Hali
  • Yakabiliwa na Tatizo Kubwa Zaidi
  • Sayansi—Jitihada Inayoendelea ya Ainabinadamu ya Kutafuta Kweli
    Amkeni!—1993
  • Sayari Yetu Dhaifu—Vipi Kuhusu Wakati Ujao?
    Amkeni!—1996
  • Je! Wanadamu Wanaweza Kuleta Amani na Usalama Wenye Kudumu?
    Amani na Usalama wa Kweli—Wewe Unaweza Kuupataje?
  • Je, Kuna Matumaini Yoyote kwa Dunia?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 4/8 kur. 3-5

Je! Sayansi Yaweza Kutatua Matatizo ya Karne ya 21?

“Sasa kuna ushuhuda mwingi ajabu wa kisayansi unaoonyesha kwamba Mama Dunia hawezi kustahimili kwa muda mrefu zaidi watoto wake wasiojali, walio watukutu.”—The European, Machi 19-25, 1992.

WANAIKOLOJIA wanazidi kuwa na maoni kwamba kinyume cha kuzusha fujo juu ya jambo dogo sana, tisho kwa dunia ni kubwa na linastahili kufikiriwa. Kwa kweli, wanasema kwamba hatua ya haraka ni ya maana sana ikiwa msiba utaepukwa. “Hatuna muda wa vizazi,” akasema msimamizi wa Taasisi ya Worldwatch mwishoni mwa miaka ya 1980. “Tuna muda wa miaka tu, ambayo tunaweza kujaribu kugeuza mambo.”

Wahariri wa kitabu kiitwacho 5000 Days to Save the Planet walikuwa hususa zaidi katika 1990 walipotangaza kitabu chao. Tangu wakati huo siku zimeendelea kupungua. Wakati unaobaki ili kuokoa sayari, kulingana na siku yao ya mwisho, sasa unakaribia siku 4,000. Na kufikia wakati wa kuanza kwa karne ya 21, isipokuwa jambo fulani lisilo la kawaida litukie kabla ya wakati huo, hesabu hiyo itakuwa imepungua kufikia siku 1,500 hivi.

Ni hali zipi zisizo za kawaida ambazo zimetokeza hatari hiyo bayana? Ni matatizo gani yanayozushwa na karne inayokuja?

Matatizo Si Machache

Watu wapendao amani wanashangilia kwamba ile Vita Baridi imekwisha. Lakini lile takwa la kupata na kudumisha amani ya ulimwengu si halisi sana. Rais Mitterrand wa Ufaransa, akizungumza mnamo Januari 1990 kuhusu matatizo ya muungano wa Ulaya, alisema: “Tunaacha ulimwengu usio na haki lakini ulio thabiti, ili tupate ulimwengu tunaotumaini utakuwa wenye haki zaidi, lakini ambao kwa hakika utakosa uthabiti zaidi.” Na The European liliandika: “Bei ya uhuru [katika mataifa yaliyokuwa ya bara la Sovieti] ni kuzidi kwa ukosefu wa uthabiti, ambako kumeongeza hatari ya vita ya nyukilia, ingawa hatari hiyo bado si kubwa.”

Kwa kweli, baadhi ya matatizo yanayokumba ulimwengu sasa hayakujulikana hata kidogo wakati ile Vita Baridi ilipoanza. Ni kama vile 5000 Days to Save the Planet kinavyosema: “Miaka hamsini tu iliyopita mazingira ya ulimwengu yalikuwa bado na usawaziko kwa kiasi kikubwa. . . . Ulimwengu ulikuwa ni mahali pakubwa ajabu, penye uzuri na uwezo mwingi; tungewezaje kupaharibu? Leo tunaambiwa kwamba sayari yetu imo hatarini, kwamba tunaiharibu na kuichafua tukielekea kwenye msiba wa tufe lote.”

Ile iitwayo eti misiba ya asili—mafuriko, dhoruba, matetemeko, milipuko ya volkeno—hutukia kila mahali. Kadiri ambayo binadamu amehusika katika kuharibu mazingira yaweza kubishaniwa. Kuna ushuhuda kwamba katika sehemu fulani, tabaka ya ozoni inayolinda ya dunia imekuwa nyembamba kwa kutisha. Baadhi ya wanasayansi sasa wanaonya kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yanayoweza kuleta misiba, yaweza kuja ghafula badala ya kusitawi hatua kwa hatua.

Kansa, ugonjwa wa moyo, matatizo ya mzunguko wa damu, na magonjwa mengine mengi yametokeza ugumu kwa stadi za kitiba. Kujapokuwa miaka ya maendeleo ya kitiba, magonjwa hayo bado huua. Katika Ulaya pekee, watu wanaokadiriwa kuwa 1,200,000 hufa kwa kansa kila mwaka, karibu asilimia 65 zaidi ya mwongo mmoja uliopita. Kwa sababu ya hofu kuhusu tauni mpya—UKIMWI, ambao umeua wachache sana kwa kulinganisha—vifo hivyo vingi hupuuzwa sana.

Tatizo jingine: Katika muda unaopungua miaka 200, idadi ya watu ulimwenguni imekua kutoka watu bilioni moja hadi kuwa bilioni tano unusu hivi. Kujapokuwa upungufu wa hivi karibuni wa kadiri ya ukuzi wa kila mwaka, wengine wanakadiria kwamba kufikia mwaka 2025, idadi ya watu ulimwenguni labda itakuwa imepita bilioni nane, na kufikia 2050 itakuwa ikikaribia kiasi cha bilioni kumi. Watu hao wote wataishi wapi? Nao watakula nini? Ripoti moja ya UM iliyotolewa katika 1991 ilikadiria kwamba watu bilioni moja tayari wanaishi katika umaskini hohehahe, maisha zao “zikikumbwa na utapiamlo, kutojua kusoma na kuandika na magonjwa kiasi cha kwamba wanapungukiwa na staha ifaayo ya kibinadamu.”

Paul R. Ehrlich, profesa wa uchunguzi wa idadi ya watu kwenye Chuo Kikuu cha Stanford katika United States, aonyesha ukubwa wa tatizo hilo, akisema: “Ilhali idadi kubwa ya watu kupita kiasi katika mataifa maskini huelekea kuyafanya yaendelee kuwa maskini, idadi kubwa ya watu kupita kiasi katika mataifa tajiri huelekea kudhoofisha uwezo wa sayari yote wa kutegemeza uhai.”

Uwezekano wa kwamba mambo yaliyotajwa mbeleni—au mengineyo kama utumizi wa dawa za kulevya, ukosefu wa makao yafaayo, uhalifu, na mizozano ya kikabila—huenda yakazusha msiba wa tufe lote katika siku za usoni zilizo karibu, hufanya kuwe sababu ya kuhangaika kikweli. Tatizo hilo ni dhahiri. Jinsi ya kulitatua si dhahiri.

Kutafuta Njia za Kuwezana na Hali

Hata hivyo, kwa kufikiria uzito wa matatizo hayo, serikali zinatafuta utatuzi, zikitofautiana katika uharaka wa jambo hilo. Kwa mfano, katika jambo la kimazingira, kusanyiko kubwa zaidi la kimazingira lililopata kufanywa lilifanywa Juni uliopita jijini Rio de Janeiro. Kusanyiko la Dunia lililodhaminiwa na UM lilikuwa la pili la aina yalo, likifuata lile lililofanywa mwaka 1972 jijini Stockholm, Swideni. Wakati huo mwanasiasa mashuhuri wa Ujerumani alisema: “Kongamano hili laweza kuwa ndio wakati wa badiliko kubwa kwa wakati ujao wa sayari hii.”

Bila shaka, mkutano wa 1972 ulishindwa kutimiza yale yaliyotazamiwa. Maurice F. Strong, mwelekezi mkuu wa makongamano ya 1972 na 1992, alikiri hivi: “Tumejifunza kwa miaka 20 tangu Stockholm kwamba usimamizi wa kimazingira, ambao kwa kweli ndio wenzo pekee halisi ambao mashirika ya mazingira yanao, ni wa maana lakini hautoshi. Ni lazima uandamane na mabadiliko ya maana katika msingi wa makusudio ya mwelekeo wetu wa kiuchumi.”

Hata hivyo, je, kongamano la 1992 litathibitika kuwa na mafanikio zaidi katika kutimiza “mabadiliko ya maana” kuliko lile la 1972? Na ikiwa sivyo, je, sayari yetu bado itaweza kufanyiwa Kusanyiko la Dunia la tatu katika miaka mingine 20, katika 2012?

Yakabiliwa na Tatizo Kubwa Zaidi

Watu kwa ujumla wanazidi kutilia shaka uwezo wa dini na siasa kutatua matatizo ya ulimwengu. Lakini ikiwa dini haiwezi, ikiwa siasa haiwezi, ni nini kinachoweza kutatua matatizo makubwa ya karne ya 21?

Broshua iliyotangazwa na Wizara ya Utafiti na Tekinolojia ya Muungano wa Ujerumani inaweka suala hilo wazi. “Kutatua matatizo hayo kwahitaji mbinu za kisiasa ambazo zaweza kusaidia si tu kuepuka mabadiliko mengine zaidi yanayoletwa na mwanadamu bali pia kuzuia matokeo mabaya ya mabadiliko ya tufe. Kwa kufikiria utata wa matatizo yanayotukabili, maamuzi ya kisiasa yanayofaa yatawezekana tu yakitegemezwa juu ya uvumbuzi thabiti wa kisayansi na utabiri hakika wa siku zijazo. Hiyo yaonekana kuwa ndiyo njia pekee ya kuepuka matokeo yenye gharama au hata yasiyotakiwa na yenye msiba. Kupatikana kwa habari hiyo ndiko kunakotokeza tatizo kubwa zaidi kwa jumuiya ya kisayansi wakati huu.”

Sayansi imekabili matatizo makubwa hapo mbeleni na imewezana nayo, angalau kwa kadiri fulani. Bado, inafaa kuuliza ikiwa sayansi yaweza kutatua matatizo ya kipekee yanayoletwa na karne ya 21 inayokuja. Je! kuna msingi wa kutazamia mazuri?

Kwa furaha, Amkeni! linatangaza mazungumzo juu ya mambo hayo mazito, yatakayofanywa katika mfululizo wa makala kuanzia na toleo hili. Sehemu ya 1 inafuata.

[Picha katika ukurasa wa 4]

Sayansi yaweza kufanya nini kuhusu uchafuzi, magonjwa, na idadi kubwa ya watu kupita kiasi?

[Hisani]

Picha ya WHO ya P. Almasy

Picha ya WHO ya P. Almasy

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki