Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 4/22 kur. 17-19
  • Je! Nihamie Nchi Yenye Utajiri Zaidi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Nihamie Nchi Yenye Utajiri Zaidi?
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Usiamue kwa Haraka
  • Usiamini Kila Kitu Unachosikia
  • Fikiria Manufaa na Hasara
  • Kujifunza Kutokana na Makosa ya Esau
  • Fuata Maamuzi Yako Kadiri Uwezavyo
  • Kumbuka Mahitaji Yako Halisi
  • Linda Urithi Wako kwa Kufanya Maamuzi ya Hekima
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Safari Yenye Kuridhisha Katika Utumishi wa Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2024
  • Je! Wewe Unathamini Urithi Wako?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Kwa Nini Ni Lazima Tuhame?
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 4/22 kur. 17-19

Vijana Wanauliza...

Je! Nihamie Nchi Yenye Utajiri Zaidi?

TARA aliondoka nchi yake ya Trinidad, Sheila aliondoka Jamaika, na Erick aliondoka Suriname. Vijana hao wote watatu walihamia nchi yenye utajiri zaidi. Kwa nini?

“Sisi vijana katika Trinidad,” Tara aeleza, “hushawishwa sana na yale tunayoona katika magazeti na TV. Kwa ubaya, jambo hilo hutupatia maoni ya uzuri wa kupita kiasi wa United States na nchi nyinginezo tajiri.”

Masimulizi ya Sheila inafanana na hayo. “Nakumbuka nikielezwa juu ya fursa nyingi za kazi na elimu ya bure.” Hata hivyo akaongezea hivi: “Sijui ni kwa nini, lakini wale waliokuwa wameenda katika nchi hizo hawakusimulia mambo yote. Labda waliona haya kukubali kwamba mambo si mazuri sana hivyo.”

Na bado watu wanahama. Ripoti moja katika Los Angeles Times ilionyesha kwamba kutokea 1980 hadi 1990, idadi ya watu waliohamia nchi nyinginezo iliongezeka maradufu na inatazamiwa kuongezeka maradufu tena kufikia mwaka 2000. Kila mwaka zaidi ya watu 700,000 huhamia United States. Australia, Kanada, Côte d’Ivore, na Saudi Arabia hupokea kila moja wahamiaji zaidi ya 50,000 kila mwaka, wengi wao wakitafuta maisha yenye ufanisi zaidi.

Ikiwa unaishi katika nchi maskini au inayoendelea, huenda wewe pia ukajiuliza ikiwa wakati ujao wako ungekuwa bora zaidi katika nchi yenye utajiri. Huo ni uamuzi mzito. Waweza kuamuaje kwa hekima?

Usiamue kwa Haraka

Erick kutoka Suriname, aamini kwamba usitende kamwe kwa uharaka lakini kwanza wapaswa utafute habari nyingi uwezavyo. “Hata katika Suriname,” yeye asema, “familia nyingi zina watu wa ukoo katika nchi kubwa-kubwa, na unaweza kupata habari kamili na kujifunza ukweli juu ya hali ya uchumi ya Ulimwengu.”

Kabla hujaamua, kumbuka hivi: “Pasipo mashauri makusudi hubatilika; bali kwa wingi wa washauri huthibitika.” (Mithali 15:22) Kwa hiyo, zungumza waziwazi juu ya maoni yako na wazazi, wazee Wakristo, na wengine wenye ujuzi na wanaokujali.

Usiamini Kila Kitu Unachosikia

Unaposikia ripoti za kuvutia za nchi za mbali zenye utajiri, ni vuzuri kuwa na shaka kidogo. “Mjinga huamini kila neno,” yasema mithali moja yenye hekima, “bali mwenye busara huangalia sana aendavyo.”—Mithali 14:15.

Sheila, aliyeishi Jamaika, alisema hivi: “Mwalimu wangu wa Kiingereza alisisitiza kwamba kuhamia United States lingekuwa jambo bora zaidi ambalo ningefanya. Watu wazima wengine waliniambia kwamba nikihamia Kanada, United States, au Uingereza, ningejifanikisha hata niwe nimechagua kazi gani. Kwa ufupi, ningekuwa mjinga kukataa fursa kama hiyo.”

Je! kuhamia kwake United States kwa kweli kulimsaidia? “Kwa njia nyingi maisha yangu yalipata kuwa bora, lakini rafiki zangu waliobaki Jamaika walifanya maisha zao pia kuwa bora. Mara nyingi unabadilisha tatizo moja kwa jingine. Mara nyingi unakoishi hakutatokeza tofauti kubwa.”

Tara, aliyehamia United States kutoka Trinidad, akubali: “Watu waliona nchi zenye utajiri kuwa nchi za fanaka—za masomo, kazi, kuchuma pesa nyingi zaidi, na kuishi chini ya hali nzuri zaidi. Lakini sasa wengi waliohama wanatambua kwamba hali inakuwa mbaya zaidi kila mahali. Wengine wamerudi nyumbani.”

Fikiria Manufaa na Hasara

Ili ufanye uamuzi unaosawazika, fikiria zaidi ya zile ripoti za kuvutia za mali nyingi katika nchi nyinginezo. Fikiria manufaa na hasara zinazohusika katika kuhama—mambo ya kiuchumi, kijamii, kiadili, na kiroho.

Kwa mfano, huenda hali ya uchumi ikawa mbaya katika nchi unayoishi. Lakini, je, hakuna kazi karibu na nyumbani? “Kule nyumbani,” asema Tara, “wengi sana hawakuwa na kazi, hasa wale ambao hawakuwa na elimu ya juu.” Kwa hiyo alihama; na ndugu zake wakabaki. “Ndugu zangu wadogo wawili walijifunza kutengeneza fanicha na kazi ya mapambo. Sasa wanafanya kazi katika viwanda na hupata kazi nyingi za binafsi kutoka kwa watu wanaopenda kazi zao. Labda hata wanafanya vizuri zaidi huko nyumbani kushinda ninavyofanya hapa katika ‘nchi ya fanaka.’”

Ukihama, inaelekea utakabiliana na tamaduni za kufadhaisha, labda hata kanuni zako za kiadili unazothamini sana zaweza kuharibiwa sana. Je! kuhama kunastahili hatari hiyo? Kisha pia, kufuatia mambo ya kimwili kumeenea sana katika nchi zenye utajiri. Jambo hilo laweza kukuathirije kiroho?

Kujifunza Kutokana na Makosa ya Esau

Ilipofikia kufikiria manufaa na hasara ya maamuzi, Esau wa nyakati za Biblia alikuwa na tatizo kubwa. Mara kwa mara alishindwa kufikiria mambo muhimu sana—hali yake ya kiroho na familia yake. Kwa matokeo, baadhi ya maamuzi yake yakawa yenye misiba.

Biblia inaonya dhidi ya mtu “asiyemcha Mungu [asiyethamini mambo matakatifu, NW], kama Esau aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja.” (Waebrania 12:16) Urithi huo wa mzaliwa wa kwanza ulikuwa mtakatifu. Mungu alikuwa ameandaa fursa kwa familia ya Esau kuwa katika mstari wa ukoo wa Mesiya, ule ufunguo wa wokovu wa wanadamu wote. (Mwanzo 22:18) Na bado “Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.” Aliiuza kwa haraka kwa ajili ya mlo wa dengu! (Mwanzo 25:31-34) Mali yako iliyo takatifu sana ni uhusiano wako pamoja na Muumba wako. Usiuuze, usiudharau, wala kuuhatarisha kwa ajili ya ufanisi wa kimwili.—Marko 12:30.

Baadaye, Esau alipohama kutoka nyumbani alikokulia kuenda bara jingine, alioa wanawake wawili Wahiti. Ndoa hizo huenda zilionekana kuwa zafaa kwa sababu fulani, lakini kiroho zilileta matatizo tu kwa sababu wanawake hao hawakuabudu Mungu wa wazazi wa Esau, Isaka na Rebeka. Wake hao walisababisha ‘uchungu rohoni mwa’ wazazi wake.—Mwanzo 26:34, 35.

Katika nchi fulani ni kawaida kwa vijana kuoa au kuolewa ili tu waingie katika nchi tajiri zaidi. Inaripotiwa kwamba India imekuwa na wenzi 4,000 wanaohamia United States kila mwaka, kukiwa na karibu 10,000 ambao bado wanangojea kuhama. Hata hivyo, ndoa ni zawadi yenye thamani kutoka kwa Mungu. Si kitu cha kutumiwa kivivi-hivi, kuwa tiketi tu ya kuvuka mpaka. Fikiria pia jinsi Yehova na washiriki wa familia waaminifu wangehuzunika ikiwa ‘ungefungwa nira pamoja na asiyeamini, kwa jinsi isivyo sawasawa.’—2 Wakorintho 6:14.

Fuata Maamuzi Yako Kadiri Uwezavyo

Jinsi unavyofuata maamuzi yako kunaweza kuwa kwa maana zaidi kushinda uamuzi wenyewe. Iwe umeamua kubaki au kuhama, jambo kuu ni kufuata maamuzi yako kadiri uwezavyo.

Ukibaki: Usiwachambue wale wanaohama. Uamuzi wao ni jukumu lao wenyewe. (Warumi 14:4; Wagalatia 6:4, 5) Jifunze kuthamini mazuri na mafaa ambayo ni ya kipekee katika nchi yako. Kuza upendo zaidi kwa watu na hisia-mwenzi kwa jitihada zao na magumu yao.

Ukihama: Tanguliza mambo yafaayo kwa hekima unapojifunza desturi mpya na labda lugha mpya. Usijiingize katika kufanya kazi muda mrefu ili kupata vitu vya kimwili ambavyo hukuhitaji awali. La sivyo, upesi utakuwa na shughuli mno kwa mambo ya kiroho.

“Ni jambo la maana sana katika ulimwengu wa leo kuwa na kazi,” akiri Sheila. “Hata hivyo, familia, rafiki, na mambo ya kiroho ni yenye umaana zaidi. Mambo yote yakishindwa, hayo ndiyo hutuendeleza.” Biblia inatuonya kwa hekima dhidi ya ‘kuutumia ulimwengu huu sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.’ (1 Wakorintho 7:31) Wale ambao kwa kweli hufaulu huweka mahangaiko yao ya kazi na pesa mahali pafaapo—nyuma kabisa ya mahitaji ya familia na mambo ya kiroho.

Chagua rafiki wapya kwa uangalifu. Erick asema: “Dumisha urafiki na wale wanaoendeleza mtindo wa maisha unaojenga.”

Kumbuka Mahitaji Yako Halisi

Mambo tunayohitaji kikweli kwa ajili ya furaha hayabadiliki. “Hata tuwe tunaishi wapi,” aonelea Sheila, “matakwa ya Yehova kwetu yanabaki yaleyale.” Matakwa hayo ni yapi? Yesu aliyadhihirisha kwa maneno haya machache: “Wenye furaha ni wale wanaona uhitaji wao wa kiroho.” “Msisumbuke” juu ya kuwa na chakula au mavazi ya kutosha. Tanguliza “ufalme wake, na haki [ya Mungu], na hayo yote mtazidishiwa.”—Mathayo 5:3, NW; 6:31, 33.

Kuishi kwa kufuata kanuni hizo kunaweza kukusaidia kupata maisha bora katika nchi yoyote.

[Picha katika ukurasa wa 18]

Nchi zenye utajiri zaweza kuonekana kuwa zavutia kushinda vile zilivyo kikweli

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki