Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 8/8 kur. 5-7
  • Maadili Yanaelekea Wapi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maadili Yanaelekea Wapi?
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Je! Kila Kitu Kinategemea maoni?
  • Kulaumu Wengine
  • Vijana—Hakuna Dira ya Kiadili Yenye Kuongoza
  • Je! Makanisa Yanaweza Kukomesha Upotovu wa Kiadili?
  • Umuhimu wa Kuwa na Maadili
    Amkeni!—2019
  • Thamani Zinazobadilika Wakati Historia Inapopita
    Amkeni!—1991
  • Kupeperushwa na Maadili Yanayobadilika
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
  • Mwongozo Ulio Mkamilifu wa Kiadili
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 8/8 kur. 5-7

Maadili Yanaelekea Wapi?

KWA karne nyingi Biblia haikutiliwa shaka ikiwa kiwango cha maadili katika nchi nyingi. Ingawa si kila mtu alifuata kanuni zayo za juu, Biblia ilipatia jamii iliyoitambua lugha ya kutumiwa ya kiadili, kiwango cha kuamua tabia. Lakini msimamizi wa chuo kikuu cha Jesuit, Joseph O’Hare aliomboleza hivi: “Tumekuwa na viwango vya zamani ambavyo vimepingwa na kuonwa kuwa vimepungukiwa au kwamba havitumiki tena. Sasa inaonekana kwamba hakuna ishara zozote za kuonyesha maadili.”

Ni nini kilichosababisha maadili yanayotegemea Biblia yasahauliwe? Sababu moja kubwa ilikuwa ni kukubaliwa kwa wingi kwa nadharia ya mageuzi. Kitabu American Values: Opposing Viewpoints chasema: “Kwa utamaduni wote unaojulikana, watu waliamini katika malimwengu mawili: ule unaoonekana, na ule usioonekana. . . . Ule usioonekana ulitoa msingi wa thamani na tabia . . . Ulikuwa chanzo cha ushikamano katika jamii yao. Hata hivyo, karibu na katikati ya karne iliyopita, watu walianza kuambiwa kwamba hakukuwa na ulimwengu usioonekana. Ulimwengu huo haukuwapo wala haukupata kuwapo.” Hasa kutokea wakati huo, kumekuwa na mashambulizi yasiyo na kifani juu ya Biblia na maadili yayo. Ule unaoitwa eti uhakiki wa Biblia na kule kuchapishwa kwa kitabu cha Darwin cha Origin of Species kulikuwa miongoni mwa mashambulizi ya kifalsafa.a

Hivyo mageuzi yalidhoofisha mamlaka ya Biblia katika akili za wengi. Kama vile makala katika Harvard Magazine inavyosema, Biblia ilionekana sasa kuwa “hadithi inayopendeza iliyotungwa tu.” Maadili yakapata pigo kubwa sana. Mageuzi yamekuwa kile ambacho mwanasayansi mashuhuri Fred Hoyle alikiita “kibali cha kuwa na tabia yoyote inayotokea.”

Bila shaka, mageuzi ni sehemu tu ya tatizo hilo. Vita viwili vya ulimwengu vilifanya watu wengi wakatae dini. Yale mapinduzi ya kiviwanda yalileta mabadiliko makubwa ya kijamii—na ya kiadili. Hata hivyo, ukuzi wa haraka wa vyombo vingi vya habari vyenye nguvu umefanya watu waingiwe na maadili mapotovu katika kiwango kikubwa sana.

Je! Kila Kitu Kinategemea maoni?

Basi, si ajabu kwamba watu wengi hawana maadili yanayowaongoza. Wanatangatanga kama meli isiyo na usukani. Kwa mfano, wengi hufuata mwelekeo ambao umeenea sana wa kwamba maadili yanategemea maoni, yaani “maadili mazuri yanategemea watu mmoja mmoja au vikundi vya watu wanaoyafuata.” Kulingana na falsafa hiyo, hakuna maadili mazuri—kila kitu kinategemea maoni ya mtu. ‘Kitu ambacho ni kibaya kwako kinaweza kuwa kizuri kwa mtu mwingine,’ wanaounga mkono wazo hilo la kutegemea maoni ya mtu wanakazia. Kwa sababu dira yao ya kiadili inayowaongoza huelekeza kwenye kila upande, wao ni wepesi wa kutetea kila aina ya tabia kuwa ni nzuri.

Kwa hiyo, tendo ambalo zamani lingetajwa kuwa “dhambi” au “baya” sasa ni “upumbavu” tu. Tendo hilo laweza kutolewa udhuru kuwa “lakirihi” lakini lisishutumiwe kuwa “ukosefu wa adili.” Linatukumbusha siku za nabii wa kale Isaya wakati kulipokuwa na watu “wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza.”—Isaya 5:20.

Kulaumu Wengine

Mwelekeo mwingine wa kiadili ni kulaumu wengine. Adamu alimlaumu Hawa, na Hawa, naye akamlaumu nyoka. Wakosaji wa leo pia hucheza mchezo wa kuepa madaraka, na mara nyingi wanasaidiwa kuchukua madaraka kupitia wastadi wa sheria na wa akili. Makala moja katika U.S.News & World Report ilikemea jumuiya ya wastadi wa akili kwa ajili ya “kuvumbua magonjwa mapya yanayoonyesha wakosaji kuwa wadhulumiwa wasiojiweza.” Kwa kielelezo, inaripotiwa kuwa Shirika la Wastadi wa Akili wa Amerika lilifikiria kwa uzito kuwaona wanajisi kuwa wagonjwa wa ugonjwa ulioitwa “upotovu wa kingono wa unajisi.” Watu fulani walihisi kwamba jambo hilo lingetoa idhini ya kunajisi bila kuadhibiwa. “Wanawake walibisha sana hivi kwamba unajisi ukapatikana kuwa si ugonjwa kamwe.”

Hatukatai jambo la wazi kwamba kutamauka wakati wa utotoni kwaweza kuathiri sana mtu mzima. Lakini ni kosa kudai kwamba mambo yaliyotamausha wakati wa utotoni yanakuwa udhuru wa tabia ya mtu mzima yenye ujeuri na yenye ukosefu wa adili.

Vijana—Hakuna Dira ya Kiadili Yenye Kuongoza

Ule mfadhaiko wa kiadili wa ulimwengu umeacha alama yao hasa juu ya vijana wanaoshawishwa vyepesi. Mtafiti Robert Coles wa Chuo Kikuu cha Harvard aligundua kwamba hakuna hata jambo lolote linaloongoza maisha ya kiadili ya watoto wa Amerika. Wanaongozwa na aina mbalimbali za dira ya kiadili na mifumo ya kanuni. Karibu asilimia 60 ya kikundi cha vijana wenye umri wa kwenda shule waliohojiwa walisema kwamba wanaongozwa na mambo yanayowafanya wafanikiwe au yanayowafanya wahisi vizuri.

Nyakati nyingine shule huchangia mfadhaiko huo wa kiadili. Ebu fikiria programu inayopendwa inayoitwa “values clarification,” (yaani, uchanganuzi wa kanuni) iliyoanzishwa miaka michache iliyopita katika shule za U.S. Mafundisho yayo ya msingi ni nini? Kwamba watoto wanapaswa kuwa huru kuchagua kanuni zao wenyewe za kiadili.

Ubovu wa kiadili kama huo unaonyeshwa wazi katika ono moja la mwanafunzi mmoja wa shule ya Jiji la New York aliyeamua kurudisha kibeti alichookota kilichokuwa na fedha taslimu dola 1,000. Wanafunzi wenzake wa masomo ya kanuni za kiadili waliitikiaje? Walimchokoza na kumkemea kwa sababu ya kufanya hivyo! Na kwa ubaya zaidi, hakuna hata mwalimu mmoja au mkuu mmoja wa shule aliyesifu mwenendo wake wa kufuatia haki. Mwalimu mmoja alitolea udhuru unyamavu huo mkubwa kwa kusema hivi: “Nikichukua msimamo wa chema na kibaya, basi mimi si mshauri wao.”

Je! Makanisa Yanaweza Kukomesha Upotovu wa Kiadili?

Haishangazi kwamba hali mbaya ya kiadili ya ulimwengu imesababisha matokeo mabaya. Wengi sasa wanakazania kurudia kanuni za zamani, jambo ambalo linamaanisha kurudia dini kwa watu fulani. Hata hivyo, makanisa hayana rekodi nzuri ya kuandaa mwongozo wa kiadili. Lile Kusanyiko la Watu Wote la Presbyterian Church (U.S.) lilikiri hivi: “Tunakabili tatizo baya zaidi kwa ukubwa walo na matokeo yalo.” Ni tatizo la aina gani? “Kati ya asilimia 10 na 23 ya makasisi nchini pote wameshiriki katika tabia za kingono au kufanya ngono na wanaparokia, wale wanaowahudumia, wafanyakazi, n.k.”

Hivyo watu wengi wamechoka na dini. Msimamizi wa Baraza la Biashara na Viwanda wa U.S. alielezea jambo hilo kwa ufupi alipotangaza hivi: “Mashirika ya kidini yameshindwa kupitisha kanuni zayo za zamani, na katika visa vingi, yenyewe yamekuwa sehemu ya tatizo [la kiadili], yakiendeleza theolojia ya ukombozi na kuwa na maoni ya kutojihusisha na tabia ya kibinadamu.”

Basi ni wazi kwamba dhamiri ya kibinadamu isiyofundishwa haitoshi kuongoza binadamu. Maadili ya leo yanaelekea uangamivu mkubwa tu. Tunahitaji mwongozo unaotoka kwa mtu aliye mkuu zaidi ya sisi.—Linganisha Mithali 14:12; Yeremia 10:23.

Mwongozo kama huo upo. Unapatikana kwa wote wanaoutaka.

[Maelezo ya Chini]

a Uthibitisho unaosadikisha juu ya vitu vilivyoumbwa unatolewa katika kichapo Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation?, kilichotangazwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.

[Blabu katika ukurasa wa 5]

Kuamini mageuzi kulikuwa sababu moja iliyofanya maadili yanayotegemea Biblia yasahauliwe

[Blabu katika ukurasa wa 6]

‘Kati ya asilimia 10 na 23 ya makasisi wameshiriki katika vitendo vya kingono na wanaparokia, wale wanaowahudumia, wafanyakazi, n.k.’

[Picha katika ukurasa wa 7]

Makasisi wameendeleza mfumo wa kiadili unaotegemea hekima ya kibinadamu badala ya Biblia

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki