Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 10/8 uku. 6
  • Mawazo Yasiyo ya Kweli Ambayo Ni ya Kawaida

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mawazo Yasiyo ya Kweli Ambayo Ni ya Kawaida
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Kuzuia Nyumbani
    Amkeni!—1993
  • Upendo na Haki Katika Ulimwengu Mwovu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2019
  • Jinsi ya Kuwalinda Watoto Wako
    Amkeni!—2007
  • Mashaka Yako Ulimwenguni Kote
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 10/8 uku. 6

Mawazo Yasiyo ya Kweli Ambayo Ni ya Kawaida

Wazo Lisilo la Kweli: Mara nyingi wale watendao vibaya watoto huwa ni watu wasiowajua, wenye akili punguani wanaowatwaa watoto na kutumia nguvu ya kimwili ili kuwatenda vibaya.

Katika visa vilivyo vingi—asilimia 85 hadi 90 kulingana na makadirio fulani—mtenda vibaya ni mtu anayejulikana na mtoto na anayetumainiwa naye. Badala ya kutumia nguvu, mara nyingi watenda vibaya humwelekeza mtoto katika matendo ya kingono hatua kwa hatua, wakitumia kwa faida yao hali ya kukosa ujuzi ya mtoto na uwezo wake mdogo wa kufikiri. (Linganisha 1 Wakorintho 13:11 na Mithali 22:15.) Watenda vibaya hao si watu wenye kichaa wanaopendelea upweke kama inavyodhaniwa. Wengi wao ni watu wa kidini, wanaoheshimiwa, na kupendwa katika jumuiya. Kulingana na Shirika la Upelelezi la Kitaifa la U.S., “kudhania kwamba mtu fulani havutiwi na watoto kingono eti tu kwa sababu yeye ni mwema, huenda kanisani, hufanya kazi kwa bidii, huwa mfadhili kwa wanyama, na kadhalika, hakufai kabisa.” Utafiti wa hivi karibuni wadokeza kwamba haifai pia kudhania kwamba watenda vibaya wote ni wa kiume au kwamba watendwa vibaya wote ni wa kike.

Wazo Lisilo la Kweli: Watoto huwa na fantasia au husema uwongo juu ya kutendwa vibaya kingono.

Katika hali za kawaida, ingawa watoto fulani wadogo wanaweza kuvurugika juu ya mambo madogo-madogo, wao hukosa ujuzi au umahiri wa mambo ya kingono kuweza kutunga uwongo kwa madai ya kwamba walitendwa vibaya. Hata wale watafiti wenye kutilia shaka sana wanakubali kwamba madai mengi ya kutendwa vibaya huwa ya kweli.a Fikiria kitabu Sex Abuse Hysteria—Salem Witch Trials Revisited, kinachokazia madai ya uwongo ya kutendwa vibaya. Kitabu hicho kinaungama hivi: “Kutenda watoto vibaya kwa kweli kumeenea sana na madai mengi ya kutenda watoto vibaya kingono . . . huelekea kuwa ya kweli (labda asilimia 95 au zaidi).” Watoto huona vigumu sana kuripoti juu ya kutendwa vibaya. Wanaposema uwongo juu ya kutendwa vibaya, mara nyingi ni katika kukana kwamba halikutukia hata ikiwa kulitukia kikweli.

Wazo Lisilo la Kweli: Watoto ni wenye kuvutia kingono na mara nyingi kwa mwenendo wao hujiletea kutendwa vibaya.

Wazo hilo hasa lina kasoro, kwa kuwa, linamlaumu mtendwa vibaya kwa yale aliyopatwa nayo. Watoto hawana fikira halisi za kingono. Hawajui utendaji huo unamaanisha nini au vile utakavyowabadili. Kwa hiyo wao hawana uwezo wa kuvutiwa nayo kwa njia yoyote yenye kusudi. Ni yule mtenda vibaya, mtenda vibaya peke yake, anayelaumika kwa ubaya huo.—Linganisha Luka 11:11, 12.

Wazo Lisilo la Kweli: Watoto wanapofunua juu ya ubaya waliotendwa, wazazi wanapaswa kuwafunza waepuke kuzungumza juu ya ubaya huo na ‘wausahau.’

Ni nani anayefaidika zaidi iwapo mtoto anyamaza bila kusema ubaya aliotendwa? Ni yule mtenda vibaya, sivyo? Kwa kweli, uchunguzi umeonyesha kwamba njia isiyo na matokeo zaidi ya kuondoa ule mshtuko wa kutendwa vibaya ni ile ya kukanusha kwa kujikaza kihisiamoyo. Kati ya zile njia tisa za kuwezana na hali hiyo zilizotumiwa na kikundi kimoja cha watu wazima waliookoka kutendwa vibaya waliochunguzwa katika Uingereza, wale waliokanusha, wakaepuka, au wakajikaza kusahau jambo hilo walipatwa na madhara makubwa zaidi ya kihisiamoyo na mtamauko katika maisha ya upevu. Ikiwa wewe ungepatwa na mashambulizi yenye kuhofisha, je, ungependa uambiwe usiseme juu yayo? Kwa nini umwambie mtoto asiseme? Kumruhusu mtoto aitikie kikawaida baada ya tukio baya kama hilo, kama vile kuwa na kihoro, hasira, na kuomboleza, kutampa fursa ya kusahau ubaya huo hatimaye.

[Maelezo ya Chini]

a Katika visa fulani vya talaka, hutukia kwamba wale watu wanaozozana hutumia shtaka la kumtenda vibaya mtoto kuwa silaha.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki