Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 10/22 kur. 24-25
  • Umaridadi Wenye Kuvutia wa Opali

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Umaridadi Wenye Kuvutia wa Opali
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kutafuta Opali
  • Kupata Umaridadi Wayo
  • Mambo Yanayoathiri Bei
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2008
  • Kutafuta Hazina ya Aina Tofauti
    Amkeni!—1993
  • Yehova Afungua Mioyo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Ongeza Rangi Fulani Kwenye Maisha Yako
    Amkeni!—1991
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 10/22 kur. 24-25

Umaridadi Wenye Kuvutia wa Opali

Na mleta habari za Amkeni! katika Australia

SHAIRI moja lipendwalo sana lasema kwamba ‘almasi ni rafiki mkubwa zaidi wa msichana.’ Lakini si almasi pekee ziwezazo kustaajabisha wenyeji wao wenye kuchachawa. Kwani, kwa ajili ya rangi mbalimbali zenye kuvutia na umaridadi wa ajabu, ile opali yenye rangi nyingi haina kifani!

Opali ni aina ya silika isiyo nyangavu. Kwa muundo wayo wa kikemikali, hiyo hufanana sana na changarawe ya kawaida. Hata hivyo, ina maji katika muundo wayo wa kimadini. Karne nyingi zilizopita, jelisilika yenye umajimaji ilipenya ikaingia katika nyufa na mianya katika miamba. Maji hayo yalipokauka, jeli hiyo hatimaye iligeuka ikawa ngumu na kuwa opali.

Kutafuta Opali

Lakini kuondoa opali kutoka kwenye makao yayo ya miamba si kazi rahisi. Mara nyingi hiyo hupatikana katika sehemu za nusu-jangwa zilizo mbali ambako joto kali, mamiriadi ya nzi wenye kuvuma, na uhaba wa maji mara nyingi hufanya maisha yasifurahishe. Na kama ilivyo na jitihada nyingi za utafutaji, kwa sehemu kubwa mafanikio hutegemea nasibu.

Zaidi ya hayo, asilimia 95 ya opali zote zinazogunduliwa huwa ni opali za kawaida. Hazivutii na hazina thamani. Kati ya zile opali zilizochimbwa zinazobaki, ni asilimia ndogo sana inayofanyiza opali zenye thamani, au opali ambazo ni vito.

Kwa hiyo ingawa watafutaji fulani wamethawabishwa kwa kupata mali nyingi, wengine wengi wamechimba bila mafanikio. Sururu, kolego, na nyundo zimekuwa vyombo vya kazi vya mtafutaji kwa miongo mingi ya miaka. Kwanza, yeye huchimba shimo jembamba katika ardhi ngumu iliyo kavu mpaka afikie tabaka ya udongo ambako opali huelekea kupatikana. Kisha achimba kwenda upande, akiwa na taa mkononi, akitafuta mng’ao wa rangi unaoonyesha kwamba amepata njia ya opali.

Mtindo huo umebadilishwa na vifaa vilivyo ghali zaidi. Baadhi ya makampuni ya kibiashara ya opali sasa hufikia tabaka ya opali kwa kuchimba ardhi kwa trekta zilizo kubwa. Mashimo mengi zaidi sasa huchimbwa kwa kekee kubwa za mashine ambazo hujengwa juu ya malori. Mashine za hali ya juu za kuchimba mashimo pia hutumiwa katika kufuata tabaka ambazo opali huelekea kupatikana.

Kupata Umaridadi Wayo

Bila shaka opali isiyolainishwa ni tofauti sana na ile imekwisha kumalizwa. Ni lazima ile opali isiyo laini ikatwe na kulainishwa. Hivyo, hiyo yaweza kutumika vizuri katika pete, vipuli, na johari nyinginezo. The World Book Encyclopedia chaeleza hivi: “Kwa sababu umaridadi wa opali umo katika mmweko wayo wa rangi za ndani, huwa haikatwi ka-mwe ikiwa na sura yenye vipande-vipande, kama almasi. Badala ya hivyo, hiyo hukatwa ikiwa na sura ya mviringo wenye uanana.”

Jinsi opali hutoa maonyesho yayo ya rangi-rangi yenye kustaajabisha ilikuwa fumbo kwa miaka mingi. Hata hivyo, kwa kupitia darubini za elektroni, wanasayansi wameanza kugundua siri za opali. Almasi hutokeza rangi zake kwa kupitia mpindo, yaani, kwa kupindika kwa nuru katika uso wa kito hicho. Muundo wa ndani na wa nje wa opali hupasua nuru, ukiipasua nuru hiyo katika rangi nyingi ndani ya jiwe hilo.

Kitabu Australian Opals in Colour chaonelea hivi: “Kito hicho kikizungushwa, rangi zote zitabadilika. Sisi huita hiyo ‘mchezo wa rangi’ na ni uwezo huo wa kubadili rangi nyakati zote unaozipa opali ule uvutio wa wazi.”

Mambo Yanayoathiri Bei

Lakini, kabla ya kununua opali wapaswa ung’amue kwamba si opali zote zilizo opali kamili. Opali michanganyiko-miwili huwa ni tabaka nyembamba, au ngozi laini ya opali yenye thamani kubwa iliyoshikanishwa kwa opali ya kawaida. Opali michanganyiko-mitatu hufanana na opali michanganyiko-miwili, lakini ili kuzilinda zisikwaruzwe, quartz (aina ya jiwe gumu) isiyo na rangi huongezwa juu. Ingawa hizo zaweza kuwa maridadi sana, kitabu Australian Opals & Gemstones—Nature’s Own Fireworks chaonya hivi: “Opali michanganyiko-miwili au michanganyiko-mitatu hazipasi kutumbukizwa ndani ya maji, sabuni, kileo au visafishi vyenye kutokeza mawimbi mengi sana, kwa sababu hizo zina tabaka nyembamba na zimeshikanishwa kwa saruji.

Jambo jingine la kuathiri bei ni rangi ya msingi au ya kichini-chini ya jiwe hilo. Opali nyeusi kwa kawaida huwa ndiyo aina ghali sana ya opali. Hiyo huitwa nyeusi kwa sababu ya msingi wayo wenye rangi ya nyeusi-nyeusi, lakini jiwe lenyewe lina rangi tofauti-tofauti za ajabu ambazo ni kama hazina kikomo. Opali yenye rangi nyeupe-nyeupe, au ambayo ni nyeupe kwa kawaida huwa si ghali. Ingawa aina hiyo huwa na msingi wenye rangi yenye kufifia-fifia au nyeupe, hiyo bado hutokeza rangi zilizo nyangavu—nyekundu-nyeupe, nyekundu, rangi ya kijani kibichi, na buluu. Wenye umuhimu vilevile katika kuamua thamani ya opali ni rangi ya msingi ya moto (kwa kawaida nyekundu huwa ghali kuliko ya rangi ya kijani kibichi au buluu) na nakshi ya rangi.

Lakini hata iwe ni opali kamili yenye kung’aa au opali ya hali ya chini kidogo ya michanganyiko-miwili au ya michanganyiko-mitatu, kito chenye rangi ya moto-moto au ya buluu ya kiasi, opali ni kitu maridadi sana kwako kutazama na kufurahia.

[Picha katika ukurasa wa 24, 25]

Karibu asilimia 95 ya vito vya opali hutoka Australia

[Hisani]

Picha: Kwa hisani ya Huduma ya Habari za Nje ya Australia

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki